Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 7,129
- 11,372
Kumekuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii zetu miaka hii ya 2000s, japo huko nyuma pia mmomonyoko huu ulikuwepo lakini sio kwa kiwango cha sasa kutokana na kukuwa kwa teknolojia na utandawazi, kila kitu siku hizi hadharani, kamera imekuja kufichua yaliyokuwa yanafichwa na kufanyika kwa siri, sasa hivi hakuna miiko tena mambo ya sirini yanafanywa hadharani bila makatazo yoyote iwe kwa mkubwa au mdogo kila mtu na uhuru wa kujiamulia mambo
Wakati tunakua ukiachilia mbali mila na desturi za makabila mbalimbali, Dini zilitumika katika kukanya na kuwaweka watu katika maadili yaani matendo yaliyo mazuri machoni kwa watu kwa kutumia sheria za kidini ambazo ziliwafanya watu kuwa na hofu na kuogopa kuyaendea au kufanya matendo ambayo hayapendezi machoni kwa watu kama vile wizi, umalaya, ushoga, uvaaji, lugha nk. Dini zilikuwa ndio mbadala wa mila na desturi baada ya kuonekana kupungua kwa ushawishi wa mila za kabila mbalimbali kutokana na kuchanganyika kwa makabila mbalimbali hasa baada ya uhuru
Watu waliishi kistaarabu na kimaadili, mambo ya sirini yalifanyika kwa kificho na ikibainika fulani anafanya kitendo kichafu au kisichopendeza aliadhibiwa kwa kufuata sheria za dini kama muongozo, jamii ilinyooka kiasi kwa kujawa na woga na hofu pia ya adhabu zilizo ahidiwa katika vitabu vya dini
Siku hizi taasisi ya dini nayo inaanza kuishiwa nguvu kwani watu waliowengi hawaamini mambo za Mungu na uumbaji, hii imechangiwa sana na kukua kwa teknolojia na utandawazi, watu hawaamini tena adhabu zilizoahidiwa kwenye vitabu vya dini wala hawawezi kuadhibiana au kukanyana kwa sheria zilizoandikwa kwenye vitabu vya dini kwakuwa hawaviamini
Sheria zinayoaminika kwa sasa ni sheria za ki nchi kwakuwa zinasimamiwa na serikali yenye zana bora kama jeshi, mahakama na magereza hivyo hofu na woga wote ni kwaserikali. Sasa serikali ni watu na wengi wanaongoza kwenye mihimili ya kusimamia mambo ya nchi wengi wao ni either hawana maadili au mfumo unaowaweka hauna au hauzingatii maadili yaani matendo mema yanayopendeza machoni kwa watu
Sheria zinazotungwa na watu wa aina hii zinazingatia maslahi ya kiuchumi zaidi huku mambo mengine ya kimaadili yakiachwa na hata kama yakiwemo kwenye hizo sheria hayafuatiliwi wala kutolewa adhabu pale yanapotendwa. Watu wameachwa waishi watakavyo kwani sheria haiwabani tena kama ilivyokuwa sheria za dini pia kuna mianya mingi yakutokea endapo mmoja akikamatwa au kuhukumiwa ikiwemo rushwa
Swali langu kwa wanajamii, je watu waachwe waishi kama wanyama mwituni? Au nini kifanyike
Karibu katika mjadala