Kuna baba nilikua nae, ni mume wa mtu, alikia ananihudumia kwa kila kitu, Mwaka jana aliniambia nimzalie, mimi nikamwambia kama unataka mtoto na mimi basi aninunulie kiwanja na kunijengea. Kweli alifanya hivyo ila wakati nakaribia alisimamishwa kazi mambo yakawa magumu kwani alikua na kesi.
Alitoka lakini alikua hana pesa tena kama mwanzo, ujenzi nyumba ilisimama kwenye lenta, akakata mawasiliano na mimi nimehangaika mpaka kumpeleka ustawi wa jamii.
Kule akasema yeye hawezi nihudumia kwa kuwa hana kazi, kweli alionyesha barua ya kufukuzwa kazi. Lakini anamaisha mazuri mke wake ana Biashara nyingi tu, ana maduka na ni mfanyakazi wa kampuni moja kubwa tu.
Watoto wake wanaishi vizuri tu ila wakwangu ana miezi mitatu ila hajawai mnunulia hata pampasi. Nawaza hivi naweza kumpeleka mke wake ustawi wa jamii ili amhudumie mtoto wa mume wake. Nilishampigia huyo mama ili kumuomba matumizi lakini aliishia kunitukana, nafanyaje kwani hata biashara ni mwanaume wetu ndo alimfungulia.
copied but ni real life story