Vyuo vikuu wampendekeza January Makamba kuwa Rais ajaye

Usiseme vyuo vikuu general bhana,sema vyuo vikuu wa kijani kama inavyoonekana pichani!kwanza vijana tunapenda "wababu" waongoze nchi na sio sisi!ikulu na bungeni ni vitu viwili tofauti!tutaingia bungeni lakini si ikulu,panahitaji maturity ya leadership ambayo inapatikana kwa uzoefu mwingi wa kuishi especially over 40"
 
Ujumbe muhimu ninaouona hapa ni kwamba WASOMI wetu hawa wanasema CCM ndio chama kinachopaswa kuiongozi Tanzania towards a brighter tomorrow...

Hata wavuta bangi wana kuwa na kiongozi wao;Humkumbuki Aston Barlet wa "The Wailers"?

Makamba labda nae wanampigia debe awe Rais wa organization kama hizo tajwa juu!
 
Jamani msiumize vichwa vyenu, hao ni Magamba CCM wenyewe kwa wenyewe ndio waliopendekezana. Sidhani kama vyuo vikuu kwa maana ya watu na akili zao wanaweza kutoa pendekezo kama hilo. Hao ni vipofu ndani ya kundi la vipofu wakijipendekeza wakidhani ndio wamepata mwenye macho ya kuongoza kumbe na huyo waliompendekeza naye ni kipofu.
 
Njaa mbaya sana, wamefadhiliwa na voda com gharama zote za mkutano , January aliwasaidia kuwapigia chapuo , unategemea tamko gani? Hivi mkutano wao ajenda ilikuwa wagombea urais au ?
 
Watatembea nchi yote kuhamasisha achaguliwe kuwa Rais! Hizo PESA za kuzunguka watapewa na nani, kama pesa za masomo wanagombana na Bodi ya Mikopo kila kukicha!
 
Samahani hiv hiyo hotel ya Mount Urugulu sio ile inayomilikiwa na Makamba baba?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hivi hao ni wasomi. Wanachekesha sana badala ya kupigania boom lipamde wasome vizuri wao wanaenda kutangaza wagombea uraisi. Shame on them kiukweli akifufuka mwl nyerere atashangaa wasomi wa sasa kama kweli wanafundishwa kuja kusaidia jamii au wanafundishwa kukambenia wagombea urais. Kweli vichwa vya wanafunzi wasomi wetu vina uji.
 
Poleni sana maana mlikuwa mimejiandaa na manguo yenu ya kijani! Kwa kifupi poleni sana hii siyo enzi ya JK! Hatudanganyiki tena! Shame on you!
 
Mwizi wa mitihani ya kidato cha Nne Galanos ambaye hajawahi kukanusha tuhuma anapendekezwa na wanaojiita wasomi wa vyuo vikuu?Intellectual dwarfs!
 
View attachment 107667
Caption: Mmoja wa Mashabiki wa January Makamba, akibusu picha ya Mbunge huyo aliyoitumia wakati wa kampeni za Ubunge mwaka 2010.

UMOJA wa viongozi wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania umempendekeza Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba, kuwa ndio anayefaa kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kwakuwa hajawai kuhusishwa na kashfa za rushwa na ufisadi .


Umoja huo unakusudia kutembea nchi nzima kwajili ya kushawishi wananchi kumchagua Makamba katika kinyanganyiro cha na nafasi ya urais katika uchaguzi ujao kwakuwa ndio kiongozi atakayeleta matumaini mapya.

Akitoa tamko la Umoja huo wa vyuo vikuu baada ya kumaliza mkutano wa siku mbili wa viongozi hao wa Vyuo vikuu 21 hapa nchini,Rais wa Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya,Theonest Theophily,alisema Makamba amechaguliwa kutokana na uadilifu na kukubalika na makundi yote yakiwemo wazee,vijana na wasomi.

Tamko hilo limetolewa baada kumalizika kwa mkutano wa siku mbili uliofanyika katika Hoteli ya Maunti Uruguru mjini hapa na kufadhiliwa Asasi isiyo ya kiserikali ya kuondoa Umasikini,Ujinga na Maradhi(FPID) .

Alisema kuwa umoja huo umempitisha Makamba baada ya kupata kura 72 na kuwashinda Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliyepata kura 20 na Mbunge wa Ubungo John Mnyika kura 9 kati ya wajumbe 105 ambao ni viongozi wa Vyuo vikuu hapa nchini waliopiga kura hizo huku kura sita zikiharibika.

Alisema kuwa baada ya kupendekeza majina mengi na matatu kupigiwa kuwa na Makamba kuibuka mshindi walianza kuchambua sifa za Makamba na kuona kama anaweza kuibuka kuwa Rais wa nchi hii na kuona kuwa wala haitajiki kusafishwa kutoka na uadilifu wake.

Alisema kuwa sifa nyingine za Makamba ni pamoja na uwezo na ujasili katika nafasi za uongozi alizoshika ikiwemo ya Ubunge wa jimbo la Bumburi mkoani tanga,uwenyekiti wa kamati ya nishati na madini,ujumbe wa kamati kuu na naibu waziri alinao sasa.

Rais huyo wa Chuo kikuu cha Mzumbe alisema kuwa katika mkutano huo wasomi hao walijadili kwa kina sifa ya rais anayepaswa kuchaguliwa katika uchaguzi ujao bila kujadili itikadi za kisiasa ambaye atawaunganisha watanzania na kutibu uhasama na mgawanyiko ulianza kujitokeza baina ya makundi mbalimbali.

Alisema kuwa katika mjadala huo wasomi hao walitaka kiongozi atakayeenda na wakati wa sasa na mwenye fikra mpya na asiyekuwa na udini wala mkabila na asiyeendeleza siasa za kikanda na asiye kuwa na chuki wala mapambano ya kisiasa na uhasama na kubaini Makamba ndie anayefaa kwakuwa anazo sifa zote.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari endapo viongozi hao wametumiwa na Makamba,alisema kuwa katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali likiwemo hilo na kwamba mpaka sasa hawana mawasilino yoyote na Makamba.

“ Tunataka kuwakikishia hatujatumiwa na mtu yoyote,tulifanya mkutano wetu tumejadili masuala ya elimu na na hili likajitokeza tukajadili na kuweka itikadi zetu pembeni kwa pamoja tukaona makamba ndiye anafaa kuwa raisi wa nchii hana kashfa yoyote,na hivi tunavyoongea nanyi hata yeye hajui suala hili” alisema Theophily.

Alisema wamechoka kutumika na viongozi katika masuala mbalimbali na kwamba hivi sasa ni wakati wa vijana kuongoza nchi hii kwakuwa ndio wamekuwa wakichangia kuleta maendeleo.

Naye mmoja wa viongozi hao Shibanda Mwashibanda,alisema kuwa katika kufanikisha suala hilo wanakusudia kumfata Makamba kumuomba aingie katika kinyanganyiro hicho cha uraisi katika uchaguzi ujao.

Alisema kuwa tayari wameshapanga vijana mbalimbali kuzunguka katika kila kanda kwajili ya kumpigia debe Makamba ili aweze kuchaguliwa kuwa raisi katika uchaguzi ujao.

“ Tumejipanga kila kanda kwa gharama zetu wenyewe ili vijana washambulie kila mkoa kwajiali ya kushawishi wananchi kumchagua Makamba awe rais katika kipindi kijacho” alisema Mwashibanda.

Alisema kuwa muda wa nchi hii kutawaliwa na wazee hivi sasa umekwisha na ahadi zao zisizotekelezeka na kwamba huu ni muda wa vijana kuongoza nchi hii ili kukabiuliana na changamoto mbalimbali zinazojitekeza kila wakati.

Naye katibu wa asasi hiyo ya FPID Francis Ndunguru alisema kuwa asasi hiyo imewezesha viongozi hao kukutana na kujadili mambo yao ikiwemo ya elimu na haina mlengo wowote wa kisiasa wala kutumiwa na chama chochote cha kisiasa.
Source: Ashton Balaigwa; NIPASHE Morogoro[p/QUOTE]

umepewa sh ngap kwa kampen ya aibu kama hii? au nawe una mahaba na january? wasomi wap hao? acha kuonesha ujinga wako.
 
Badae mtasema lusinde au maji marefu nyie hangaikeni ila rais anajulikana hata kwa watoto wa vidudu kuwa ni dr.......!mtamalizia vijana wa buku 7 lumumba.
 
waambie waache ujinga watanzania milioni 44+ tuchaguliwe raisi na wahuni 80 waliojifungia guest house wakafanya maamuzi yao ya kipuuzi
 
Ni hivi kichwa na tumbo siku zote vitaendelea kuwa tofauti na hakuna chenye uwezo wa kufanya kazi ya mwingine.
Wasomi na "Wasomi wagangaa njaa" wataendelea kuwepo ila watabaki kuwa tofuati kama nuru na giza.
 
hakuna wasomi hapo kwanza hao viongozi wa vyuo vikuu asilimia kubwa wanatoka kwenye chama cha magamba then si kuona hatari kwa matokeo hayo, na fikiri kipimo hicho walicho kuwa wanataka kufanya wangefanya research kwa wanafunzi wote wa vyuo vyao ndio wangepata majibu sahihi.

makamba anaweza kuwa kiongozi mzuri, ila si kwa kiwango cha Zitto Zuberi Kabwe bado ana hitaji muda mrefu sana kujiimarisha hata kwenye chama chake, huyu kijana hawezi hata kumfikia Deo Filikunjombe hawezi kabisa labda wanataka awe rais wa serekali zote za wanafunzi wa vyuo vikuu.

Ila si raisi ya nchi hii ambayo ilisha ongonzwa na Baba wa Taifa ambae alikuwa na sifa zote za uongozi.

Huwa nawasikia mkisema ccm hakuna vijana wasomi. Sasa mkuu hawa wametoka wapi?
 
Nchi hii kuendelea kazi sana. Na dhambi kubwa inayotufanya tuzidi kudidimia ni UNAFIQ hao viongozi wa umoja wa vyuo vikuu ni janga la kitaifa.

Wao wameona urais 2015 ndio dili kubwa badala ya kujadili mustakabali wa nchi yetu kwa kipindi tulichopo, hasa mambo ya ufisadi, mauaji ya raia, na njia nyingne za maendeleo.

Na badala yake.wanakaa kikao na kujadili rais wa 2015... hakika bongo zao zimejaa UJI, na hao.ndio type ya wasomi tulinao ambao kwao; tunategemea transformation ya nchi yetu.

Nasikitika kudema Tz imekwama, na dawa pekee ya kuikwamua ni sisi watz kuacha unafiki. Maana ndani za unafiki ndimo chimbuko ya ufisadi mawazo mabaya n.k

Let we pray for Tanzania hao ndio wasomi tulionao na tunaowategemea.

Cc Nguruvi3 na Jasusi wakubwa saidieni kuokoa dhahama hii Tanzania itazidi kukwama
 
Last edited by a moderator:
mnafikiri nchi ni tarafa, au familia yako nyumbani? bado hana level ya kupewa nchi.
 
Nchi hii kuendelea kazi sana. Na dhambi kubwa inayotufanya tuzidi kudidimia ni UNAFIQ hao viongozi wa umoja wa vyuo vikuu ni janga la kitaifa.

Wao wameona urais 2015 ndio dili kubwa badala ya kujadili mustakabali wa nchi yetu kwa kipindi tulichopo, hasa mambo ya ufisadi, mauaji ya raia, na njia nyingne za maendeleo.

Na badala yake.wanakaa kikao na kujadili rais wa 2015... hakika bongo zao zimejaa UJI, na hao.ndio type ya wasomi tulinao ambao kwao; tunategemea transformation ya nchi yetu.

Nasikitika kudema Tz imekwama, na dawa pekee ya kuikwamua ni sisi watz kuacha unafiki. Maana ndani za unafiki ndimo chimbuko ya ufisadi mawazo mabaya n.k

Let we pray for Tanzania hao ndio wasomi tulionao na tunaowategemea.
Cc Nguruvi3 na Jasusi wakubwa saidieni kuokoa dhahama hii Tanzania itazidi kukwama
Remote hakuna tatizo kubwa kama kuiangalia nchi kama mtu na si watu, kuangalia uongozi kama mtu na si taasisi.

Kinachofanyika hakina tofauti na kile kinachofanywa na watoa ''sadaka'' misikitini na makanisani kwa kauli mbiu ya harambee. Hutawasikia wakisema harambee za kujenga bomba la maji kwasababu huko hakuna watu wenye ushahwishi.

Hawa vijana wanatumiwa kama walivyotumiwa wale wa UDOM ambao wanaamini kwa dhati asingekuwepo bwana fulani basi wasingesoma. Wao wanaamini hivyo kwasababu upeo wao wa kuelewa umeishia hapo.

Lakini pia haya mambo yanapotokea huwa yana maana nyingi.
Hili linaonyesha kiwango cha elimu yetu. Kama viongozi wa kada ya wasomi wanafikiria mtu kuwaongoza kwasababu hana kashfa na wala si maono (vision) hilo ni tatizo.
Wanachotaka kusema hawa vijana ni kuwa mwizi ni yule aliyekamatwa na ngozi si yule aliyeiba ng'ombe

Well, huyu Makamba wanayesema ndiye ameingia Ikulu na JK hadi majuzi alipokwenda kuwa mbunge. Hata sasa hivi ni sehemu ya uongozi wa JK ambao tumeshuhudia taifa likipita katika wakati mgumu sana. Mambo yote yanayohusu madawa yanayoathiri hao vijana J.Makamba ni sehemu ya maamuzi ya Ikulu. Matatizo ya bei za juu za simu ni sehemu ya JM, kushindwa utawala wa sheria JM ni sehemu yake na hata kushamiri ujangili JM ni sehemu ya watu wenye maamuzi.

Nasema ni sehemu yake nikimaanisha alikuwa Ikulu, na sasa ni waziri hivyo historia yake haishii katika kuwa na kashfa lazima aangaliwe ushiriki wake katika mambo mengine ikiwa ni pamoja na failure zake kama alivyoshindwa kushughulikia suala la simucard.

Hoja hapa ni kusema hawa vijana wa siku hizi wasingeweza kufanya yale vijana wa zamani waliyoweza kuyafanya.

Akina Thabo Mbeki, Khama, Neto walikuwa na vijiwe UDSM kubadilishana mawazo na wasomi, sijui ingekuwa siku hizi wangefikiria hata kupita eneo hilo.

Vijana hawajadili matatizo ya kulisukuma taifa mbele, leo muhimbili watu wanaishi kama mazizi ya mbuzi, kwingine hospitali zimekuwa kama maeneo ya kwenda kukutana na kifo na si huduma.

Elimu imekuwa tatizo hakuna vifaa wala motisha kwa wahusika.
Kilimo ambacho leo kingetukwamua ndicho hicho cha jembe la kukokota na punda.
Vijana hawaoni haya wanatumia masaa na masiku kujadili mada potofu na hafifu ya JM.

Tanzania ipo bila JM na hivyo JM ni seheumu ya Tanzania si Tanzania yote.

Tuna tatizo has kwa vijana kuanzia serikali, bungeni na sasa vyuoni sijui mitaani kukoje yarabi.
 
Back
Top Bottom