Vyuo vikuu wampendekeza January Makamba kuwa Rais ajaye

Vyuo vikuu wampendekeza January Makamba kuwa Rais ajaye

Dickson Ng'hily

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
473
Reaction score
508
January Makamba.jpg
Caption: Mmoja wa Mashabiki wa January Makamba, akibusu picha ya Mbunge huyo aliyoitumia wakati wa kampeni za Ubunge mwaka 2010.

UMOJA wa viongozi wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania umempendekeza Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba, kuwa ndio anayefaa kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kwakuwa hajawai kuhusishwa na kashfa za rushwa na ufisadi .

Umoja huo unakusudia kutembea nchi nzima kwajili ya kushawishi wananchi kumchagua Makamba katika kinyanganyiro cha na nafasi ya urais katika uchaguzi ujao kwakuwa ndio kiongozi atakayeleta matumaini mapya.

Akitoa tamko la Umoja huo wa vyuo vikuu baada ya kumaliza mkutano wa siku mbili wa viongozi hao wa Vyuo vikuu 21 hapa nchini,Rais wa Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya,Theonest Theophily,alisema Makamba amechaguliwa kutokana na uadilifu na kukubalika na makundi yote yakiwemo wazee,vijana na wasomi.

Tamko hilo limetolewa baada kumalizika kwa mkutano wa siku mbili uliofanyika katika Hoteli ya Maunti Uruguru mjini hapa na kufadhiliwa Asasi isiyo ya kiserikali ya kuondoa Umasikini,Ujinga na Maradhi(FPID) .

Alisema kuwa umoja huo umempitisha Makamba baada ya kupata kura 72 na kuwashinda Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliyepata kura 20 na Mbunge wa Ubungo John Mnyika kura 9 kati ya wajumbe 105 ambao ni viongozi wa Vyuo vikuu hapa nchini waliopiga kura hizo huku kura sita zikiharibika.

Alisema kuwa baada ya kupendekeza majina mengi na matatu kupigiwa kuwa na Makamba kuibuka mshindi walianza kuchambua sifa za Makamba na kuona kama anaweza kuibuka kuwa Rais wa nchi hii na kuona kuwa wala haitajiki kusafishwa kutoka na uadilifu wake.

Alisema kuwa sifa nyingine za Makamba ni pamoja na uwezo na ujasili katika nafasi za uongozi alizoshika ikiwemo ya Ubunge wa jimbo la Bumburi mkoani tanga,uwenyekiti wa kamati ya nishati na madini,ujumbe wa kamati kuu na naibu waziri alinao sasa.

Rais huyo wa Chuo kikuu cha Mzumbe alisema kuwa katika mkutano huo wasomi hao walijadili kwa kina sifa ya rais anayepaswa kuchaguliwa katika uchaguzi ujao bila kujadili itikadi za kisiasa ambaye atawaunganisha watanzania na kutibu uhasama na mgawanyiko ulianza kujitokeza baina ya makundi mbalimbali.

Alisema kuwa katika mjadala huo wasomi hao walitaka kiongozi atakayeenda na wakati wa sasa na mwenye fikra mpya na asiyekuwa na udini wala mkabila na asiyeendeleza siasa za kikanda na asiye kuwa na chuki wala mapambano ya kisiasa na uhasama na kubaini Makamba ndie anayefaa kwakuwa anazo sifa zote.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari endapo viongozi hao wametumiwa na Makamba,alisema kuwa katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali likiwemo hilo na kwamba mpaka sasa hawana mawasilino yoyote na Makamba.

“ Tunataka kuwakikishia hatujatumiwa na mtu yoyote,tulifanya mkutano wetu tumejadili masuala ya elimu na na hili likajitokeza tukajadili na kuweka itikadi zetu pembeni kwa pamoja tukaona makamba ndiye anafaa kuwa raisi wa nchii hana kashfa yoyote,na hivi tunavyoongea nanyi hata yeye hajui suala hili” alisema Theophily.

Alisema wamechoka kutumika na viongozi katika masuala mbalimbali na kwamba hivi sasa ni wakati wa vijana kuongoza nchi hii kwakuwa ndio wamekuwa wakichangia kuleta maendeleo.

Naye mmoja wa viongozi hao Shibanda Mwashibanda,alisema kuwa katika kufanikisha suala hilo wanakusudia kumfata Makamba kumuomba aingie katika kinyanganyiro hicho cha uraisi katika uchaguzi ujao.

Alisema kuwa tayari wameshapanga vijana mbalimbali kuzunguka katika kila kanda kwajili ya kumpigia debe Makamba ili aweze kuchaguliwa kuwa raisi katika uchaguzi ujao.

“ Tumejipanga kila kanda kwa gharama zetu wenyewe ili vijana washambulie kila mkoa kwajiali ya kushawishi wananchi kumchagua Makamba awe rais katika kipindi kijacho” alisema Mwashibanda.

Alisema kuwa muda wa nchi hii kutawaliwa na wazee hivi sasa umekwisha na ahadi zao zisizotekelezeka na kwamba huu ni muda wa vijana kuongoza nchi hii ili kukabiuliana na changamoto mbalimbali zinazojitekeza kila wakati.

Naye katibu wa asasi hiyo ya FPID Francis Ndunguru alisema kuwa asasi hiyo imewezesha viongozi hao kukutana na kujadili mambo yao ikiwemo ya elimu na haina mlengo wowote wa kisiasa wala kutumiwa na chama chochote cha kisiasa.
Source: Ashton Balaigwa; NIPASHE Morogoro
 
Kuna maraisi wengi kuna rais wa masharobaro,rais wa sinza mariaga,kuna rais wa madalali kuna rais wa mapresenter sam misago kuna poor people's president mchomvu kuna rais wa akudo bella kuna rais wa fm akademia nyoshi sasa huyo january wamempendekeza awe rais wa tegeta?
 
Hahahahaha...Kamanda umefanya nicheke mpaka basi....C mihemuko ya vijana? Eti wanataka awe raisi wa Danganyika! tehe tehe tehe tehe tehe tehe......
 
hii tabia ya wanafunzi wa elimu ya juu kujiita wasomi inanisumbua sana, vyama vyao vyote hivyo viongozi wao ni undergraduate halafu wanajiita wasomi!hivi usomi wao huwa ni kitu gani kilicholeta tija kwa jamii, zaidi ya kujumuika kwenye hizo taasisi na kuutafuta huo usomi? Tukirudi kwenye mada huyo waliyempigia kura ameleta mchango chanya upi kwenye serikali? amepitia mapito gani yakuweza kumchunguza kuwa kweli ataweza kuyakabili majukumu ya uraisi, wahenga walisema mkate bila kupitia kwenye tanuri la moto aislani hauwezi kuiva? sasa huyu mtu wao kapitia tanuri gani? URAISI SI LELEMAMA KAMA MADESA NYIE WANAFUNZI MJIITAO WASOMI!
 
Ujumbe muhimu ninaouona hapa ni kwamba WASOMI wetu hawa wanasema CCM ndio chama kinachopaswa kuiongozi Tanzania towards a brighter tomorrow...
 
hii tabia ya wanafunzi wa elimu ya juu kujiita wasomi inanisumbua sana, vyama vyao vyote hivyo viongozi wao ni undergraduate halafu wanajiita wasomi!hivi usomi wao huwa ni kitu gani kilicholeta tija kwa jamii, zaidi ya kujumuika kwenye hizo taasisi na kuutafuta huo usomi? Tukirudi kwenye mada huyo waliyempigia kura ameleta mchango chanya upi kwenye serikali? amepitia mapito gani yakuweza kumchunguza kuwa kweli ataweza kuyakabili majukumu ya uraisi, wahenga walisema mkate bila kupitia kwenye tanuri la moto aislani hauwezi kuiva? sasa huyu mtu wao kapitia tanuri gani? URAISI SI LELEMAMA KAMA MADESA NYIE WANAFUNZI MJIITAO WASOMI!

Tuheshimu maoni ya WASOMI wetu.

Taifa lisilosikiliza WASOMI linajiandaa kuangamia...
 
Walitaja Makamba kawalipa sh'ng ngap?? alafu mbeya hakuna UNIVERSITY...!
 
Tukizilaumu shule za katatutakuwa tunakosea, tukilaumu vyuo vyetu kwa kuwakaririsha wanafunzi na kuwaambia wasome madesa tu napo haitoshi tulaumu mfumo uliopo wa ccm ambao umetoa uzalendo kwa kuua azimio la Arusha na kule leta lile la Zanzibar kiasi kwamba kwamba vijana wanatumika kukidhi haja ya matumbo yao

Hivi hawa wanajiita wasomi wamekaa na kupiga kura kumchagua rais wa nn? nchi vyuo or ? maana na nao ni marais nao. Mbulula wakubwa hao vijana wa Lumumba wakiongozwa na Mwashibanda
 
Baada ya kamati ya vijana wapenda amani Tanzania KVT kumpendekeza January, Zitto, Mbatia na Dr Mwinyi hawa nao wamewathibitishia watanzania na wale waliokuwa na fikra eti KVT wanatumiwa kuwa shutma zao ni za uongo. Wameridhika na utendaji kazi wa January na wameamua kusema kwa sauti moja Ccm Yatosha.
 
hii tabia ya wanafunzi wa elimu ya juu kujiita wasomi inanisumbua sana, vyama vyao vyote hivyo viongozi wao ni undergraduate halafu wanajiita wasomi!hivi usomi wao huwa ni kitu gani kilicholeta tija kwa jamii, zaidi ya kujumuika kwenye hizo taasisi na kuutafuta huo usomi? Tukirudi kwenye mada huyo waliyempigia kura ameleta mchango chanya upi kwenye serikali? amepitia mapito gani yakuweza kumchunguza kuwa kweli ataweza kuyakabili majukumu ya uraisi, wahenga walisema mkate bila kupitia kwenye tanuri la moto aislani hauwezi kuiva? sasa huyu mtu wao kapitia tanuri gani? URAISI SI LELEMAMA KAMA MADESA NYIE WANAFUNZI MJIITAO WASOMI!

Mkubwa swali ulilouliza juu ya usomi wa hawa ndugu zetu wa vyuo vikuu hata mimi nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara bila ya majibu... Nway, Eti wanasema ndo yeye pekee asiyekuwa na scandal...Tehe tehe tehe tehe tehe...Hivi kale ka dada yake kukusanya pesa kwenye kampuni fulani za kumsaidia kaka akisema wamchangie waziri mtarajiwa kalikuwa hakamguzi yeye eeeeh! tehe tehe tehe tehe....
 
Kuna maraisi wengi kuna rais wa masharobaro,rais wa sinza mariaga,kuna rais wa madalali kuna rais wa mapresenter sam misago kuna poor people's president mchomvu kuna rais wa akudo bella kuna rais wa fm akademia nyoshi sasa huyo january wamempendekeza awe rais wa tegeta?

Bora umenena king! Nahisi wanataka kumpa uraisi wa chama cha wanamitindo Tanzania, au kile cha wasanii wa move!
 
Yani siku hizi ndio wanakutana kujadili upuuzi wa aina hii??!
Kweli wanafunzi wenzao ndio waliowatuma?!
Katika matatizo yote walonayo wanafunzi wa vyuo vikuu hili ndio wameona la maana?!

Dah tuna safari ndefu sana.
 
hii tabia ya wuanafunzi wa elimu ya juu kujiita wasomi inanisumbua sana, vyama vyao vyote hivyo viongozi wao ni undergraduate halafu wanajiita wasomi!hivi usomi wao huwa ni kitu gani kilicholeta tija kwa jamii, zaidi ya kujumuika kwenye hizo taasisi na kuutafuta huo usomi? Tukirudi kwenye mada huyo waliyempigia kura ameleta mchango chanya upi kwenye serikali? amepitia mapito gani yakuweza kumchunguza kuwa kweli ataweza kuyakabili majukumu ya uraisi, wahenga walisema mkate bila kupitia kwenye tanuri la moto aislani hauwezi kuiva? sasa huyu mtu wao kapitia tanuri gani? URAISI SI LELEMAMA KAMA MADESA NYIE WANAFUNZI MJIITAO WASOMI!

Ur right
 
Tukizilaumu shule za katatutakuwa tunakosea, tukilaumu vyuo vyetu kwa kuwakaririsha wanafunzi na kuwaambia wasome madesa tu napo haitoshi tulaumu mfumo uliopo wa ccm ambao umetoa uzalendo kwa kuua azimio la Arusha na kule leta lile la Zanzibar kiasi kwamba kwamba vijana wanatumika kukidhi haja ya matumbo yao

Hivi hawa wanajiita wasomi wamekaa na kupiga kura kumchagua rais wa nn? nchi vyuo or ? maana na nao ni marais nao. Mbulula wakubwa hao vijana wa Lumumba wakiongozwa na Mwashibanda

Kamanda naona unapiga 'Pentagon' Tehe tehe tehe tehe.....
 
Yani siku hizi ndio wanakutana kujadili upuuzi wa aina hii??!
Kweli wanafunzi wenzao ndio waliowatuma?!
Katika matatizo yote walonayo wanafunzi wa vyuo vikuu hili ndio wameona la maana?!

Dah tuna safari ndefu sana.
Yaani we acha tu kamanda...Ndo 'WASOMI WETU HAO' Hahahahahahaha.....
 
UMOJA wa viongozi wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania umempendekeza Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba, kuwa ndio anayefaa kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kwakuwa hajawahi kuhusishwa na kashfa za rushwa na ufisadi

Eti kila aliye Chuo Kikuu anajiita msomi! Kwa hiyo hilo genge lao kukutana ndio wametoka na kauli ya kujumuisha waTanganyika wote? Wapuuzi kabisa na ni watu ambao hata hawaijui kesho yao.

Kudhihirisha kwamba ni wapuuzi wa hawaijui kesho yao, wangeweza kuitafuta historia ya Januari Makamba kwa kurudi miaka michache kidogo kwamba, hata elimu yake aliipata ki rushwa rushwa. Utafiti huo unge wapelekea kuona ni jinsi gani J Makamba alitumia rushwa/ ufisadi na kupata majibu ya mitihani ya Kidato cha Nne pale Galanos na kupelekea kufukuzwa na hadi kufutiwa matokeo ya kidato cha nne. Kwa mshangao wa wengi, kaibukia Morogoro akiwa kidato cha sita.

Sasa hiyo HOJA MFU ya kusema j J Makamba hana kashfa yoyote ya ufisadi wameitoa wapi? Hizi elimu za shule za kata ni matatizo matupu. Kama wanao jiita wasomi ndio wanamtafuta raisi wa nchi hii kwa njia hiyo, basi Tanganyika tumeishiwa wasomi.

ZAO LA UFISADI NI FISADI. kwa vile amepata mafanikio kwa njia ya KIFISADI, hawezi kujitenga na UFISADI daima. Kwani UFISADI ndio umemfikisha hapo alipo.
 
Tuheshimu maoni ya WASOMI wetu.

Taifa lisilosikiliza WASOMI linajiandaa kuangamia...

Hivi kila anayepitia Chuo Kikuu tumuite Msomi? utaitwa msomi tu pale utakapokuwa ile elimu uliyopitia imekusaidia kuwa na uelewa wa mambo mengi yakiwemo hayo ya masomo na mengine ya hapa duniani na hasa uraiani , hao vijana sijaona kama ni wasomi kwa sababu kuna kitu wamepungukiwa.
 
Back
Top Bottom