Vyuo 10 Bora Tanzania 2019

Hebu mliotupia vazi kubwa na kofia pembe 4 UDSM coz ya computer science nyoosha mkono juu tujuane
 
Bado haujanipatia ufumbuzi wa shida yangu mkuu, je haiwezekani kuvigawanya kulingana na kada husika?
.
Haya sasa mfano mimi Mkulima wa SUA nimebisha kuwa UDSM sio chuo bora kuliko SUA utakuwa na hoja za kunipinga?

Ukinisoma vizuri hapo juu utapata jibu lako. Soma vizuri sehemu ya kwanza. Na halafu sehemu ya pili. Haya siyo mambo ya kubisha tu na hayafanyiki kienyeji. Utaonyeshwa vigezo vilivyotumika na data zote.

Of course SUA kitakuwa chuo bora katika kada ya Kilimo lakini hii hakuifanyi kuwa chuo bora kuliko UDSM katika ujumla wake kwa kuangalia criteria zingine ambazo baadhi yake nimezitaja hapo juu. Ndiyo maana kwa kawaida kunakuwa na ranking za aina mbili kuu. Ranking za jumla (kama alizotaja mleta mada) na rankings za kada moja moja. Kwa hiyo utakuta Top 10 kwenye Agriculture, Top 10 kwenye Medicine, Top 10 kwenye Engineering, Top 10 kwenye Social Sciences n.k.

Na unapotaka kuomba chuo, ranking za jumla hazitakusaidia sana bali rankings za program moja moja. Kama unataka Kilimo nenda SUA. Medicine MUCHS.....japo kwa kuangalia criteria za jumla UDSM ni nambari wani.
 
kuna factors nyingi huwa wanaangalia hawakurupuki ww kama umesoma vyuo vya Kata shauri yako tambua point zako hazikukutosha kwenda ud au sua
Wewe uliyeenda una Nini cha ziada.Mbona Bash boy hajasoma UD na anamaisha mazuri kuliko Mtz yoyote yule.
 
Sasa mimi mtu wa Sheria chuo cha Muhimbili, SUA n.k vinakuaje vyuo bora kwangu?
.
Hizi orodha huwa na tabu nazo sana kuanzia zile za mwanafunzi bora kitaifa, shule bora kitaifa n.k
.
Ungetenganisha kulingana na kada mfano vyuo bora vya masomo ya sanaa ukavitaja vyuo bora vya masomo ya science ukavitaja ila unataja kiujumla hivyo maana yake nini?
Msitusumbue mwishowe mtataka mwanafunzi mwenye nidhamu anatoka chuo gani.hii ni general classification ukion unaongoza kwenye law juwa umeshindwa kwenye sports na bookkeeping.
 
Inakuaje udsm jalalani walikotoka akina kabudi, mkumbo n.k kiwe cha kwanza, au wamekariri? Toa udsm hapo juu weka SUA
 
Nimetembea Tanzania mpaka Pemba sijawahi ona mhitimu wa chuo na. 10 kwenye ofisi yoyote. Hivi wahitimu wake ndio kina Ponda na Mapozeo au kuna wengine wenye point zilizotulia ?
 
Hiyo imetolewa na university link world wide .

Ingia unlink utaona top universities kila nchi.

Kwamba nani katoa sio tija sana. Hoja aliyoitoa mdau ina nguvu. Chuo cha ardhi au udaktari unapokilinganisha na chuo cha utawala bila kuwa na vigezo makini na kuangalia maeneo gani unalinganisha sio sahihi.
 
Hivi ni kwa nini siku zote vyuo bora huwa ni vya serikali lakini shule bora za olevel na advance ni za private hasa za kanisa?
 
Sasa mimi mtu wa Sheria chuo cha Muhimbili, SUA n.k vinakuaje vyuo bora kwangu?
.
Hizi orodha huwa na tabu nazo sana kuanzia zile za mwanafunzi bora kitaifa, shule bora kitaifa n.k
.
Ungetenganisha kulingana na kada mfano vyuo bora vya masomo ya sanaa ukavitaja vyuo bora vya masomo ya science ukavitaja ila unataja kiujumla hivyo maana yake nini?
Hapo ndipo sintofahamu inapoanziaga, kwa mfano chuo bora kwa upande wa Mass communication kwa East Africa nzima ni SAUT, MUHAS afya, sasa mtu akigeneralize tu inakuwa haileti maana. Ni vyema hawa wanaotoa orodha ya ubora wa vyuo wawe wanaeleza ubora wake upo katika nyanja ipi hii itawasaidia wake wanaotaka kuomba vyuo.
 
Una mawazo mazuri sana Mkuu,
labda nikuulize,hapa Tanzania Kuna specialization za Vyuo?
Vyuo vikuu vya science ni vipi?
sababu siku hizi hata suo unakuta wana Business Administration,Muhimbili wa Science ya Binadamu wakati Udsm wana science ya Engineering vitu,Udom wana vyote...science,sanaa,biashara nk,Mzumbe wana Biashara,sheria,social science nk,sasa hebu naomba utoe Muongozo wako ili wasomaji tuelewe criteria zipi unataka ziwekwe ktk kutofautisha vyuo vikuu?
Wengine wanaangalia number of Phd,wengine researches published,Internationala journals,nk nk
Ngoja nimsaidie kidogo, vyuo vikuu vya science ni Dar es salaam institute of Technology DIT, ATC Arusha, MUST Mbeya, Hawa ndio miamba kwenye hizo nyanja.
 
Back
Top Bottom