Vyombo vya ulinzi mmewashindwa Panya Road?

Vyombo vya ulinzi mmewashindwa Panya Road?

Wenzako wapo bize kusaka malaya kila kona mpaka wanaua watu.

Hayo ya panya road wanaona siyo tatizo la kiusalama. Tatizo kubwa ni wale wanaojiuza miili yao.

Nchi ina vichaa wengi hii
Ndo nguvu imeelekezwa huko Sasa hivi?
 
Wanaume mnashindwa kuji organize mkaacha usingizi wa masaa machache ili kuwatia adabu hao madogo? Polisi haiwezi kufika Kila mahali kwa muda mnaotaka nyinyi mambo mengine yapo ndani ya uwezo wenu
Shida ni kujiandaa mkuu.pia wengi wanaishi kivyaovyao.salamu imeisha

Imagine umepiga ma kvant huko ukarudi saa 5 ukikurupushwa saa 8 unaweza pambana?
 
Halafu hilo eneo ninakumbuka halina Kituo cha Polisi.

Eneo lote la Goba Mpakani wanatumia Kituo cha Polisi Makabe ambacho kipo Kata ya Mbezi.

Kuna wakati kilikuwa kinajengwa Kituo cha Polisi Goba Mpakani na sijui kama kimeisha.

Ila ubinafsi wa watu wa Dar es Salaam kunawafanya wahuni kutamba bila sababu.

Mwanaume ni mlinzi wa familia. Inakuwaje unakosa panga ndani, huna rungu na huna mbinu za kupambana?

Haya inakuwaje mnashindwa kushirikiana kuwakabili hao wajinga?
Ukiwa na panga halafu wenzako wapo 20 Wana mapanga apo mcha Glock tu
 
Watu wa dar bana
Juzi mmewazodoa watu wa chuga kwa kupekeshwa na ally dangote, leo imekuaje?
Sie watu 50.nyie mtu mmoja.panya road ni akina ally dangote 50 wanaoluvamia Kwa mkupuo
 
Na risasi zote zipo huko pia

Tatizo la panya road ni matokeo ya mikakati mibovu ya viongozi kushindwa kuwapatia fursa na hamasa vijana wawe busy na uzalishaji
Risasi??!
Msako wa machangudoa
 
Kuna jamaa yang aliwaacha waingie uwani kabisa akiwa anawaona kwenye camera kakaaa kimya walivyoingia watano 5 aliwalamba ote risasi alafu kimya asubuh polis wakafata mizoga yao.

Wawili walilambwa za miguu wengine kiunoni walobakia hai sjui kama wako mpaka leo.

Hao mkiamua kuwashughulikia ni kitendo cha masaa tu mtandao ote unamalizwa sababu wanajulikana na wanapokaa panajulikana.

Upumbavu wa mkoa huu ni kwamba kila mtu anajifanya ana maisha yake ya wengine hayamuhusu mpaka yamkute ndo mtu anaweza kuja kukugongea mlango
 
Maisha ya maeneo mengi yanayochipukia ndo yako hivo.kila mtu kwenye geti lake.kuna mitaa mtu akipiga yowe wote wanajaa kusaidia.huko ndo tunakoenda Kila mtu ashambuliwe kivyake,ajihami kivyake.
 
Sasa mkuu
Unaona kabisaa akili za wenye dhamana zilipoelekea. Wanashindwa kukaa chini na jamii kusaka suluhu ya pamoja dhidi ya panya road wao wanawasaka wanawake wanaojiuza miili yao
Unatuletea kiongozi kama chalamila Kwa Jiji kama dar..tutarajie Nini?
 
Back
Top Bottom