Vyombo vya Habari huu ndio msimu wa kuvuna pesa za wanasiasa, msiwatangaze bila kulipwa kwanza

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,905
Matangazo ya biashara ni moja ya eneo muhimu kwa vyombo vya habari.

Sasa hivi tunaelekea uchaguzi mkuu wanasiasa kutwa watakuwa. Wakiita vyombo vya habari kukitangaza biashara zao za kisiasa wanakogombea. Hilo ni tangazo la biashara. Vyombo vya habari anzeni kuchaji pesa.

Wakiwaalika walipe gharama za waandushi na watangazaji na wakitaka warushwe iwe taarifa ya habari au kuandikwa kwenye gazeti walipie. Hiki ni kipindi muafaka cha media kutengeneza pesa
 
YEHODAYA leo umeandika lamaana sana. Kumbe ndio maana CCM kila chombo cha habari ni wao tu maana washawahonga kwa kuwanunua . Hongereni sana aisee. Nimeamini mwizi akikosa chakuiba anajiibia mwenyewe.
 
YEHODAYA leo umeandika lamaana sana. Kumbe ndio maana CCM kila chombo cha habari ni wao tu maana washawahonga kwa kuwanunua . Hongereni sana aisee. Nimeamini mwizi akikosa chakuiba anajiibia mwenyewe.
Sio kununua media ni kuwalipa haki yao. Kujitangaza ugombea Ni tangazo la biashara unatafuta soko ili ukapate mamilioni kwa nini usilipie hilo tangazo. Wafanyakazi wa media wanalipwa mishahara. Unataka wajitolee bure? Kipindi hiki media isiyochaji pesa ikifa ijilaumu yenyewe.
 
Sio kununua media Ni kuwalipa haki Yao . Kujitangaza ugombea Ni tangazo la biashara unatafuta soko ili ukapate mamilioni kwa Nini usilipie Hilo tangazo.Wafanyakazi wa media wanalipwa mishahara. Unataka wajitolee bure ? Kipindi hiki media isiyochaji pesa ikifa ijilaumu yenyewe
Unaelewa wajibu wa media kwenye nchi/duniani?
 
Kwa maana hiyo sisiemu peke yake ndio watakuwa wanatangazwa maana wao ndio watu wa kutoa hela
 
Fair kabisa. Kwa hivyo na sisi wasomaji/watazamaji/wasikikizaji tuanze kulipwa na media hizo, maana wao si wanapata pesa kupitia sisi?
 
Kupanua wigo wa Rushwa..
Media sio Charity organization Wewe, ndio maana Wana leseni za biashara na Kodi wanalipa.Kulipwa kwa kazi zao Ndio. Kunawafanya waendelee kuwepo

Kulipwa kwa kazi zao sio rushwa
 
Matangazo ya biashara Ni moja ya eneo muhimu kwa vyombo vya habari

Sasa hivi tunaelekea uchaguzi mkuu wanasiasa kutwa watakuwa. Wakiita vyombo vya habari kukitangaza biashara zao za kisiasa wanakogombea
Hilo Ni tangazo La biashara

Vyombo vya habari anzeni kuchaji pesa

Wakiwaalika walipe gharama za waandushi na watangazaji na wakitaka warushwe iwe taarifa ya habari au kuandikwa kwenye gazeti walipie

Hiki Ni kipindi muafaka Cha media kutengeneza Pesa
Ndiyo wakati wa kuila hela ya CCM kwani vyombo vyote vya habari viko kwa ajili ya CCM na wagombea wake. Sisi tunaonana na wapiga kura ana kwa ana.
 
Basi wangeuza machungwa na vishet studio kama jukumu lao namba moja
Usimpangie mtu afanye biashara ipi nchi huru hii Ndio maana wengine Wako kwenye media business ukienda na tangazo lako la kujinadi sijui udiwani, ubunge au uraisii au kukinadi Chama chako Hilo Ni tangazo la biashara lipia

Hakuna Cha bure media sio NGO Ni business

Kukuweka TV , Radio zao na magazeti Yao lipa
 
Back
Top Bottom