Vyeti kuungua moto

Vyeti kuungua moto

Jamani Nivea pole kwa ajali ya moto
Fuata ushauri wa wanajamvi walivyokushauri
 
tujifunze kwa makosa jamani tuwe tuna SCAN vyeti itakua kidigitali zaidi
 
Asanteni sana kwa ushauri na mawzo yakinifu lakini pi aninayo soft copy kwenye emails zangu.
 
Habari wakuu zangu nawasaliimu sana.

Naombeni sanakama kichwa cha habari kinavyojieleza vyeti vyangu vyote vimeungua moto nzungumzia kuanzia form 4 mpaka chuo kikuu sasa nashindwa nianzie wapi kuvipata.Nawaomba mnifungue macho jamani nianzie wapi yeyote aliyewahi kutana na kitu hii anishauri wapendwa.

Je kuna uwezekano wakuvipata upya ?

nawasilisha?
Dada yangu pole sana kwa matatizo yaliyokupata.

Wote walioshauri hapo juu wapo sahihi. lakini zifuatazo ndiyo taratibu fupi zitumiwazo na Baraza la mitihani la Tanzania:

-Nenda polisi ukatoe taarifa ili upatiwe "Police Loss Report"

-Nenda ukatangaze kwenye gazeti la serikali (Habari leo, Daily News), gharama zake huwa ni kati ya Tsh 20,000-25,000. Hii ni mhuhimu incase ikatokea mtu aliokoa au aliokota mzigo/kifurushi kilichokuwa na vyeti vyako wakati wa tukio basi atakurudishia.

-Peleka Baraza la Mitihani nakala halisi ya Police loss Report na Ukurasa mzima wa gazeti lenye tangazo la upotevu wa Vyeti/cheti (Kwa vyeti vya sekondari tu). Unatakiwa kuwa na kitambulisho (ID) chochote amacho ni hai (validi) pamoja na picha moja ya Passport size kwa kila cheti kilichopotea. Ukishakamilisha nyaraka zote hizo tapewa fomu maalumu pale Baraza la Mitihani ambayo utatakiwa kuijaza ili upatiwe "Statement of Results" na sio cheti. Kumbuka hii SOR hutapatiwa wewe mkononi bali itatumwa kule ambako utataka kukitumia cheti/vyeti hivyo kwa wakati huo, baada ya kulipia benk kwenye Necta acc. Tsh 10,000 kwa njia ya rejesta kama ni ndani ya nchi.

Kumbuka cheti hutolewa mara tu, kuanzia sasa utacheza na SOR mpaka uzee wako. Taarifa muhimu unazotakiwa kuwa nazo ni Namba yako ya Mtihani kwa mwka husika uliofanyia mtihani wako na aina ya mtihani uliofanya kama ni CSEE au ACSEE.
 
Asante sana kipenzi kaka yangu mungu akubariki kwa muda na nguvuuliyotumia kunishauri.nin ahili tena
je cheti cha elimu ya juu nilisomea nje ya tanzania nitafanyaje sasa.hizi hizi police report zitanisaidia
 
tujifunze kwa makosa jamani tuwe tuna SCAN vyeti itakua kidigitali zaidi
Scanning haitoshi, hiyo ni nakala kama zilivyo nakala nyingine tu. Wenzetu wanaojua umuhimu wa cheti wanadiriki hata kuweka benki kama pesa ili viwe kwenye usalama. Lakini wabongo hatujali sana sehemu tunazoweweka nyaraka muhimu kama hizo mpaka zitakapopotea au kuliwa na mchwa ndiyo tunajua kumbe kilikuw akitu muhimu sana.
 
Asante sana kipenzi kaka yangu mungu akubariki kwa muda na nguvuuliyotumia kunishauri.nin ahili tena
je cheti cha elimu ya juu nilisomea nje ya tanzania nitafanyaje sasa.hizi hizi police report zitanisaidia
Kama ni cheti kilichopatikana nje ya nchi mamlaka husika iliyotoa cheti hicho itahusika.
 
Sheria gani ? tutajie tafadhali

Sijawahi kusikia wala kuambiwa kwamba kuna sheria inakataza lamination kwenye vyeti original au photocopy. Ila ninachojua huwa kuna angalizo au tahadhari kwamba lamination ikianza kuchoka huingiza hewa au unyevunyevu na hufanya baadhi ya maandishi ku nasia katika plastic na hivyo cheti kufutika.
 
Asanteni sana kwa ushauri na mawzo yakinifu lakini pi aninayo soft copy kwenye emails zangu.

Pole sana Nivea, ukipata hizo police statement, huko chuo hawawezi kukupigia muhuri hizo copy zako at least ku certify kwamba ni copy ya genuine cheti walichotoa wao? Sijui sheria zinasemaje hapo.

Ubarikiwe na Bwana
 
yap,tena hiyo ni mbinu nzuri sana ya kuhfadhi vyeti,zingatia,lamination usifanye kwani hairuhusiwi kisheria

Nahisi sababu ya kutofanyia lamination vyeti unajua vyeti kama vya necta ukivipiga photocopy vinaandika kwenye ile karatasi ya iliyotoka copy copy copy nahisi ndo njia ya kujua cheti halisi sasa ukiki laminate hicho kitu hakitokei kwa unabadilisha hali yake hyo
 
yap,tena hiyo ni mbinu nzuri sana ya kuhfadhi vyeti,zingatia,lamination usifanye kwani hairuhusiwi kisheria.

What??? hii ni news kwangu. Mkuu hili ni kweli??? By the way sasa hata vikimwagikiwa maji uanze kuhangaika daaaa!
Pole sana Nivea
 
Last edited by a moderator:
Dada yangu pole sana kwa matatizo yaliyokupata.

Wote walioshauri hapo juu wapo sahihi. lakini zifuatazo ndiyo taratibu fupi zitumiwazo na Baraza la mitihani la Tanzania:

-Nenda polisi ukatoe taarifa ili upatiwe "Police Loss Report"

-Nenda ukatangaze kwenye gazeti la serikali (Habari leo, Daily News), gharama zake huwa ni kati ya Tsh 20,000-25,000. Hii ni mhuhimu incase ikatokea mtu aliokoa au aliokota mzigo/kifurushi kilichokuwa na vyeti vyako wakati wa tukio basi atakurudishia.

-Peleka Baraza la Mitihani nakala halisi ya Police loss Report na Ukurasa mzima wa gazeti lenye tangazo la upotevu wa Vyeti/cheti (Kwa vyeti vya sekondari tu). Unatakiwa kuwa na kitambulisho (ID) chochote amacho ni hai (validi) pamoja na picha moja ya Passport size kwa kila cheti kilichopotea. Ukishakamilisha nyaraka zote hizo tapewa fomu maalumu pale Baraza la Mitihani ambayo utatakiwa kuijaza ili upatiwe "Statement of Results" na sio cheti. Kumbuka hii SOR hutapatiwa wewe mkononi bali itatumwa kule ambako utataka kukitumia cheti/vyeti hivyo kwa wakati huo, baada ya kulipia benk kwenye Necta acc. Tsh 10,000 kwa njia ya rejesta kama ni ndani ya nchi.

Kumbuka cheti hutolewa mara tu, kuanzia sasa utacheza na SOR mpaka uzee wako. Taarifa muhimu unazotakiwa kuwa nazo ni Namba yako ya Mtihani kwa mwka husika uliofanyia mtihani wako na aina ya mtihani uliofanya kama ni CSEE au ACSEE.

Maelezo hapo juu ni kweli kabisa, nilikumbwa na Tatizo kama la Nivea na nimeendelea kutumia utaratibu hapo juu,

Kitu cha Nyongeza ni kuwa utatakiwa kuwa na Barua kutoka Secondary ulizosoma kutoka kwa wakuu wa shule hizo kuonyesha kuwa ulisoma pale. Barua hizo zinahitajika na watu wa Baraza la mitihani

Pole sana Nivea, kimsingi usiwe disapointed maisha/Professional Career yako itaendelea; ukienda balaza la mitihani utagundua kuwa hili swala linawakumba watu wengi kwa namna tofauti tofauti.
 
Mkuu hiyo ni kweli kabisa, kuna siku nilienda pale Baraza kupata huduma,cha ajabu nilibaini karibia robo yawateja wote wa siku walikuwa wanaomba vyeti vipya, walipokuwa waliulizwa sababu kila mmoja alikuwa akitoa yake, huyu moto, yule kaibiwa, mwingine mafuriko ilimradi ni wengi sana.
 
Kwa maelezo yaho yaliyokwisha kutolewa na wadau, mimi niseme tu pole dada Nivea
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hiyo ni kweli kabisa, kuna siku nilienda pale Baraza kupata huduma,cha ajabu nilibaini karibia robo yawateja wote wa siku walikuwa wanaomba vyeti vipya, walipokuwa waliulizwa sababu kila mmoja alikuwa akitoa yake, huyu moto, yule kaibiwa, mwingine mafuriko ilimradi ni wengi sana.

Ni kweli kabisa mkuu; na nivizuri kufahamu kuwa waajiri nao wanalifahamu hilo, at some points nilipata wasiwasi pale ambapo nilitakiwa kuonyesha Vyeti vyangu kwa kazi niliyopata nje ya nchi, nikafikiria utaratibu wa Statement of Results kwamba 'Je utakubarika na Hawa Internationals'! mambo yameendelea kwenda vizuri kwa utaratibu huo huo; nimesoma Masters kwa utaratibu huo huo, nimebadili Organisations kwa utaratibu huo huo

So in principle, Nivea has Nothing to worry about, but be prepared for some time wastage due to bureaucratic procedures as mentioned. Kwamba pamoja na utaratibu huo na usumbufu huo bado ninakubaliana kabisa na utaratibu uliowekwa kwa kuwa kinyume cha hapo 'Everyone in need of a certificate could have one'!!! ....
 
Sio siri mkuu kuna risk nyingi sana, kwa sisi wa uswazi mende wanaweza kuvigeuza toilet na dinner au madogo wanaweza kufungia vitumbua ikala kwetu. Kama mbwai na iwe mbwai mi sijaacha hata kimoja vyote viko laminated. Sheria zao za kuombea rushwa wapeleke mbele huko.

ndugu zangu kwa hili la lamination msidanganywe...mimi vyeti vyangu vyote ni laminated, na nimetipia sehem nying wkt natafuta kaz, ikiwepo mahakamani, na mwisho nilipata kazi serikalini kwa kupitia procedure zote nikiwa na vyeti vyangu laminated bt sijawahi hata kuulizwa badala yake nilikua nasifiwa kua najua kutunza vyeti.
 
Asante sana kipenzi kaka yangu mungu akubariki kwa muda na nguvuuliyotumia kunishauri.nin ahili tena
je cheti cha elimu ya juu nilisomea nje ya tanzania nitafanyaje sasa.hizi hizi police report zitanisaidia

ulaya hawana longolongo wewe wasiliana nao watakwambia kiasi cha pesa kwaajili ya post cost,mimi nilipoteza cheti changu nilisoma uingereza walinambia nitume passport namba yangu na pesa ya post cost basi nasasa walishanitumia
 
ndugu
zangu kwa hili la
lamination msidanganywe...mimi vyeti vyangu vyote ni laminated, na
nimetipia sehem nying wkt natafuta kaz, ikiwepo mahakamani, na mwisho
nilipata kazi serikalini kwa kupitia procedure zote nikiwa na vyeti
vyangu laminated bt sijawahi hata kuulizwa badala yake nilikua nasifiwa
kua najua kutunza vyeti.

ndio maana nilisema hata mimi pamoja na watz wengne wengi akiwemo JK
tumefanya hvo.Ila ukipatwa na matatizo yanayohusiana na taarifa za
kwenye vyeti then ukapeleka laminated certificates kwa court,hapo ndipo utakapo
jua why lamination is bad
 
Back
Top Bottom