Vyeo katika uislam vinapatikana vipi na vikoje?

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,437
5,103
Huku mtaani naona vijana wanaitana sheikh, mufti, maalimu, na wengine wainaitana akii, je haya ni majina ya waislamu au ni vyeo?

Utaratibu wa vyeu ukoje huko.
 
Sheikh ni yeyote Tu hata wewe unaweza kuwa Shiekh.

Imam ni Yule Kiongozi msikitini.

Mufti yupo mmoja tu Tanzania.

Watu wakiitana mitaani sio waislam.

Inetegemea na umaarufu wako Kwa hao watu.

Si Kareem Benzema tunamuita sheikh?
 
Huku mtaani naona vijana wanaitana sheikh, mufti, maalimu, na wengine wainaitana akii, je haya ni majina ya waislamu au ni vyeo? Utaratibu wa vyeu ukoje hiko?
Hao wanaitana kwa kutainiana,kama mtu akikuta anamwita mwenzake wa umri sawa,mwanangu au babu au mkuu au mshikaji nk.
 
1. Akh (أَخ) ni ndugu kwa Kiswahili, hivyo kila muislamu ni Akh, akiwa wa kike ukht (أُخْت) Dada. Ilitumika zaidi kwa wafuasi wa Muslim Brotherhood, wengine wanaiga.

2. Sheikh (شَيْخ) literally means Mzee. [ii] Mtu aliewahi kuwa au aliepo kwenye ndoa. Akiwa wa kike Shaikha (شَيْخَة). Si vyeo vya kidini.

3. Ustadh (أُسْتَاذ) ni Profesa. Au [ii] Mwalimu. Maana zote hazihusiki na dini ya Kiislamu. Ni lugha tu.

4. Kadhi (قَاض) Jaji. Anaweza akawa Kadhi wa mahkama ya Kiislamu au conventional. Ili awe Kadhi, ni lazima awe na mamlaka ya kutumia nguvu kama alivyo jaji. Anapotoa hukumu ni lazima wahusika wafuate. Mfano Zanzibar wana makadhi wa wilaya, mkoa na Kadhi Mkuu, Kenya wanamwita Chief Kadhi.

5. Mufti (مُفْتِي) Mtu anaejibu masuala ya dini, anaweza kuwa mufti wa dhehebu maalum au mufti wa jumla. Sio lazima achaguliwe na serikali au awe na mamlaka, kauli yake si lazima kufuatwa, inakua ni legal view. Mfano waendesha vipindi vya "uliza ujibiwe" katika vituo redio na televisheni vya Kiislamu, au Mufti Mkuu wa nchi kama Mufti Menk wa Zimbabwe.

6. 'Aalim (عَالِم) ni graduate. Haijalishi dini. 'Ulamaa (عُلَمَاء) laterally ni graduates, just plural. [ii] Scientist. Pia haina mafungamano na dini.

Mfano Baraza la Ulamaa Tanzania, inamaanisha wao minimum qulification kwa memba wao ni a bachelor degree.

7. Imamu (إِمَام) Kiongozi. Akiwa Imamu wa msikiti ni kiongozi anaeongoza swala. Anapatikana kwa kuchaguliwa na waumini wenyewe, vigezo ni elimu ya Qur'an wakiwa sawa anaejua zaidi Sunnah, wakiwa sawa anatangulizwa mwenye umri mkubwa... na vigezo vyengine vinafuata ikiwa watakua wanalingana.
 
Huku mtaani naona vijana wanaitana sheikh, mufti, maalimu, na wengine wainaitana akii, je haya ni majina ya waislamu au ni vyeo? Utaratibu wa vyeu ukoje hiko?
Kwenye uisilamu hakuna cheo
 
Inategemea na kiwango cha ilmu. Na wapo walioenda Makka, wana jina lao.

Umenielewa Usthadhi?
Uongo, haitegemei na elimu. Labda maalim ndio mwalimu.

Sheikh ni mtu yeyote tu mradi awe amebalehe. Mufti kwa Tanzania ni Mkuu wa Bakwata (Inasemwa pia Mkuu wa waislam) Tanzania.

Alieenda Makkah kuhij ni Alhaj au Hajjat kama ni wa kike.
 
....
Screenshot_2023-07-10-17-18-02-289_com.android.chrome.jpg
 
Sheikh ni yeyote Tu hata wewe unaweza kuwa Shiekh.

Imam ni Yule Kiongozi msikitini.

Mufti yupo mmoja tu Tanzania.

Watu wakiitana mitaani sio waislam.

Inetegemea na umaarufu wako Kwa hao watu.

Si Kareem Benzema tunamuita sheikh?
Sio akii ni akhii na maana ya akhii ni ndugu
 
1. Akh (أَخ) ni ndugu kwa Kiswahili, hivyo kila muislamu ni Akh, akiwa wa kike ukht (أُخْت) Dada. Ilitumika zaidi kwa wafuasi wa Muslim Brotherhood, wengine wanaiga.

2. Sheikh (شَيْخ) literally means Mzee. [ii] Mtu aliewahi kuwa au aliepo kwenye ndoa. Akiwa wa kike Shaikha (شَيْخَة). Si vyeo vya kidini.
a watakua wanalingana.
Nzuri , ahsante
 
1. Akh (أَخ) ni ndugu kwa Kiswahili, hivyo kila muislamu ni Akh, akiwa wa kike ukht (أُخْت) Dada. Ilitumika zaidi kwa wafuasi wa Muslim Brotherhood, wengine wanaiga.

2. Sheikh (شَيْخ) literally means Mzee. [ii] Mtu aliewahi kuwa au aliepo kwenye ndoa. Akiwa wa kike Shaikha (شَيْخَة). Si vyeo vya kidini.

3. Ush, wakiwa sawa anatangulizwa mwenye umri mkubwa... na vigezo vyengine vinafuata ikiwa watakua wanalingana.
jazakallah.
 
Back
Top Bottom