Vyama Washirika wa UKAWA vyadhihirisha kuwa ni vyakikabila, Kikanda na kidini

Kama zitto tu kawashinda anawapukutisha kila anakopita hayo maji marefu ni maji gani labda maji ya chai ya basi ya kure arusha.

Endeleeni kudanganywa na kifaranga wenu huyo fahamu zitakapo warejea ndipo mtatambua kuwa mulikuwa mnadanganywa.
 
Mh.Tufe jaribu kuwa na staha.Wewe jama ni muungwana basi Jisikie haya kutamka maneno hayo.Kwa mfano umekutwa kwa bahati mbaya na binti yako mdogo wa miaka 6 unaangalia CD ya ngono halafu akakuambia baba ni aibu kwako na ni dhambi kuangalia huo uchafu.
 
Na huu ndo ukweli wenyewe. James Mbatia baada ya kuona kuwa nje ya uchagani hana mtaji, ameamua kurudi Vunjo kugombana na Mrema

Na Mrema si alitokea Temeke?
Mkuu kelele za nini kama katiba haijavunjwa,hakika Ukawa ni umiza kichwa.
 
Kweli kabisa Mkuu. Dhambi ya ubaguzi itawatafuna hawa ukawa

Ina maana kuwa mumeishiwa kabisa kiasi cha kutokuwa na uwezo,wakuandaa single nyine mpaka mrudie hii ya ukabila,ambayo imeshapitwa na wakati?.
 
Hivi watu hamuwezi kujadili mambo kwa staha kuliko kutukana na kutunga uongo, wenzenu wanajadili watajikwamua vipi kwenye economic crisis na kujadili maswali muhimu ya kuwauliza wagombea nyie mnajadili slaa Kuoa mke WA mtu, hivi hyo ina uhusiano gani na wananchi kupata huduma za msingi na kupunguza umaskini WA kipato..slaa akichukua mke WA mtu we inakuathiri vipi kiuchumi,kimaendeleo? Ifikie hatua tubadirike na tujadiri mambo ya muhimu.
 
Kwani wewe hujui kuwa CCM ni chama cha wakristo? Kama hujui muulize Dr Slaa alikuwa na wadhifa gani pale Vatican wakati akiwa Padre na mwanachama wa ccm, Elimika kuanzia hapo hayo unayosema wewe ni matokeo tu mechi ilishachezwa kitambo! miaka hiyo!!!
 
Wadau amani iwe kwenu.

Hii sasa si siri tena. Ni ukweli ulio dhahiri kabisa ambao hata mtoto mdogo anaweza kuuona.

Ni kwamba, kwa muda mrefu kulikuwa na madai kuwa CHADEMA na CUF ni vyama vya kidini, kikabila na kikanda. Madai haya yamekuwa yakitolewa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini. Cha kushangaza ni kwamba, wenye vyama hivyo wamekuwa wakikanusha kwa nguvu wawapo majukwaani. Wanasema kuwa dhana ya udini, ukabila na ukanda imekuwa ikitolewa na CCM ili kuvidhoofisha vyama hivyo kisiasa. Katika kukanusha madai hayo, baadhi ya vyama kama vile CHADEMA vimejaribu kuchanganya safu yake ya uongozi japo kitakwimu dhana ya udini, ukanda na ukabila inadhihiri.

Mungu si Athumani na waswahili wanasema kuwa pembe la ng'ombe halifichiki. Hivi sasa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD vimegawana majimbo ambayo watasimamisha wagombea wao. Katika mgawanyo huo, ile dhana ya udini, ukanda na ukabila imejidhihiri tena kwa macho angavu. Mathalan, NCCR Mageuzi bado kimeendelea kuwa ni chama cha mkoa wa Kigoma pekee ijapokuwa mwenyekiti wake anataka kugombea jimbo la Vunjo ambalo wakazi wengi ni wa kabila lake. Halikadhalika, CHADEMA imeendelea kutetea majimbo yale yale yenye wafuasi wake wengi ambayo yanakaliwa na wachagga na majimbo ya mikoa ya kaskazini au yale yanayokaliwa na watu wenye asili ya mikoa ya kaskazini. Mathalan, kwa Dar es Salaam, CHADEMA imetaka kusimamisha wagombea kwenye majimbo ya Kawe, Ubungo na Kinondoni ambayo kwa kiasi kikubwa yanakaliwa na watu wenye asili ya mikoa ya kaskazini. Vile vile, CHADEMA wanaonekana kutaka kusimamisha wagombea kwenye mikoa mingi yenye wakazi wengi ambao ni waumini wa dini ya kikristo. Hali hii inawwfanya CHADEMA wasione kuwa maeneo yanayokaliwa na waislam wengi kuwa hayana tija kwao kisiasa au hawana nafasi ya kushinda uchaguzi

CUF kwa upande wake, wao wameendelea kutetea dhana ya kuwa ni chama cha mikoa ya pwani yenye wakazi wengi wa jamii ya kiislam. Mathalan, CUF imetaka kusimamisha wagombea kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Tabora, Tanga na majimbo yote ya Zanzibar ambako wanaamini kuwa ndiko kwenye wafuasi wao. Kwa Dar es Salaam, CUF wameomba kusimamisha wagombea kwenye majimbo ya Temeke na Kigamboni ambako wakazi wake wengi wana asili ya mikoa ya kusini. CUF wanaona kuwa kwenye mikoa yenye wakristo wengi wao hawana mtaji wa kisiasa na kwamba hata wakisimamisha wagombea hawawezi kuchaguliwa kwa vile chama hicho wafuasi wake wengi ni waislam.

Tathmini zaidi inaonesha kuwa mgawanyo huu wa majimbo umekuja kudhihirisha kuwa vyama hivi si vya kitaifa bali vinategemea baadhi ya maeneo tu na watu wenye asili fulani ili kupata ushindi. Jiulize, kama CHADEMA ni chama cha kitaifa, kwa nini hakisimamishi wagombea mikoa ya kusini na majimbo ya Zanzibar? Jiulize, kama NCCR ni chama cha kitaifa, kwa nini kinang'ang'ania kusimamisha wagombea mkoa wa Kigoma tu?

Hakika hii ni aibu kwa siasa za nchi hii. Jiulize, kama ukabila, ukanda na udini unajidhihiri kwenye majimbo ya uchaguzi, vipi wataficha dhana hiyo ikiwa watashinda uchaguzi? Mungu tuepushe na hilo balaa.
hawa dawa ni moja yaani ni kuwanyima kila kitu. wapuuzi hawa!
 
Mh.Tufe jaribu kuwa na staha.Wewe jama ni muungwana basi Jisikie haya kutamka maneno hayo.Kwa mfano umekutwa kwa bahati mbaya na binti yako mdogo wa miaka 6 unaangalia CD ya ngono halafu akakuambia baba ni aibu kwako na ni dhambi kuangalia huo uchafu.
Mkuu oldonyosambu hawa wajamaa wamezoea kupost utumbo humu. Na utumbo hujibiwa kiutumboutumbo tu. Asante.
 
Last edited by a moderator:
Wadau amani iwe kwenu.

Hii sasa si siri tena. Ni ukweli ulio dhahiri kabisa ambao hata mtoto mdogo anaweza kuuona.

Ni kwamba, kwa muda mrefu kulikuwa na madai kuwa CHADEMA na CUF ni vyama vya kidini, kikabila na kikanda. Madai haya yamekuwa yakitolewa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini. Cha kushangaza ni kwamba, wenye vyama hivyo wamekuwa wakikanusha kwa nguvu wawapo majukwaani. Wanasema kuwa dhana ya udini, ukabila na ukanda imekuwa ikitolewa na CCM ili kuvidhoofisha vyama hivyo kisiasa. Katika kukanusha madai hayo, baadhi ya vyama kama vile CHADEMA vimejaribu kuchanganya safu yake ya uongozi japo kitakwimu dhana ya udini, ukanda na ukabila inadhihiri.

Mungu si Athumani na waswahili wanasema kuwa pembe la ng'ombe halifichiki. Hivi sasa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD vimegawana majimbo ambayo watasimamisha wagombea wao. Katika mgawanyo huo, ile dhana ya udini, ukanda na ukabila imejidhihiri tena kwa macho angavu. Mathalan, NCCR Mageuzi bado kimeendelea kuwa ni chama cha mkoa wa Kigoma pekee ijapokuwa mwenyekiti wake anataka kugombea jimbo la Vunjo ambalo wakazi wengi ni wa kabila lake. Halikadhalika, CHADEMA imeendelea kutetea majimbo yale yale yenye wafuasi wake wengi ambayo yanakaliwa na wachagga na majimbo ya mikoa ya kaskazini au yale yanayokaliwa na watu wenye asili ya mikoa ya kaskazini. Mathalan, kwa Dar es Salaam, CHADEMA imetaka kusimamisha wagombea kwenye majimbo ya Kawe, Ubungo na Kinondoni ambayo kwa kiasi kikubwa yanakaliwa na watu wenye asili ya mikoa ya kaskazini. Vile vile, CHADEMA wanaonekana kutaka kusimamisha wagombea kwenye mikoa mingi yenye wakazi wengi ambao ni waumini wa dini ya kikristo. Hali hii inawwfanya CHADEMA wasione kuwa maeneo yanayokaliwa na waislam wengi kuwa hayana tija kwao kisiasa au hawana nafasi ya kushinda uchaguzi

CUF kwa upande wake, wao wameendelea kutetea dhana ya kuwa ni chama cha mikoa ya pwani yenye wakazi wengi wa jamii ya kiislam. Mathalan, CUF imetaka kusimamisha wagombea kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Tabora, Tanga na majimbo yote ya Zanzibar ambako wanaamini kuwa ndiko kwenye wafuasi wao. Kwa Dar es Salaam, CUF wameomba kusimamisha wagombea kwenye majimbo ya Temeke na Kigamboni ambako wakazi wake wengi wana asili ya mikoa ya kusini. CUF wanaona kuwa kwenye mikoa yenye wakristo wengi wao hawana mtaji wa kisiasa na kwamba hata wakisimamisha wagombea hawawezi kuchaguliwa kwa vile chama hicho wafuasi wake wengi ni waislam.

Tathmini zaidi inaonesha kuwa mgawanyo huu wa majimbo umekuja kudhihirisha kuwa vyama hivi si vya kitaifa bali vinategemea baadhi ya maeneo tu na watu wenye asili fulani ili kupata ushindi. Jiulize, kama CHADEMA ni chama cha kitaifa, kwa nini hakisimamishi wagombea mikoa ya kusini na majimbo ya Zanzibar? Jiulize, kama NCCR ni chama cha kitaifa, kwa nini kinang'ang'ania kusimamisha wagombea mkoa wa Kigoma tu?

Hakika hii ni aibu kwa siasa za nchi hii. Jiulize, kama ukabila, ukanda na udini unajidhihiri kwenye majimbo ya uchaguzi, vipi wataficha dhana hiyo ikiwa watashinda uchaguzi? Mungu tuepushe na hilo balaa.

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha! Haaaaaa! Haaaaaaa! Haaaaaa! Haaaaaaa! Nyie CCM ni Wahuni tu; Sasa ukabila na ukanda ukoje hapo? NCCR Mwenyekiti wake ni Mchaga, nguvu ya chama iko Kigoma, ni kwa Wachaga kule Kigoma? Ukabila uko wapi hapo. CHADEMA ina Wabunge Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mwanza, Singida, Kagera, Iringa, Shinyanga, Simiyu na Katavi ispokuwa tu Zanzibar kutokana na sbb za kihistoria. Mikoa yote hiyo inapatikana katika kanda zote za nchi kuanzia Masharki hadi Magharibi, Kaskazini hadi Kusini.
Sasa kwa maoni yako wewe mkuu ukanda, ukabila na udini wa CHADEMA uko wapi hapo?

Hata hivyo, hata mkoa tu wa Kilimanjaro utagundua kuwa CCM ndio ina wabunge wengi kuliko CHADEMA. Kungekuwa na huo ukabila basi CHADEMA ingekuwa inashikilia majimbo yote ya mkoa wa Kilimanjaro. Hali kadhalika Arusha na Manyara CHADEMA hawana majimbo yote, kote huko CCM ina majimbo mengi. Huo ukanda na ukabila uko wapi? CUF nayo ni vivyo hivyo. Kwa hiyo hizo propaganda zenu ni za kupuuzwa na haziwezi kuwasaidia kitu kwa sasa.

Mara nyingi nimekuwa nawambia vijana wa CCM kuwa nendeni shule kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl.Nyerere kule mkasomee namna ya kutengeneza propaganda vizuri kama makada wa zamani. Hizi propaganda mnazotuletea hapa jamvini zinawaabisha tu kwa sbb hazijaandaliwa kwa ustadi. Hata mtoto wa chekechea anaweza kung'amua. UKAWA wamewashika pabaya, na mnachofanya sasa ni kujaribu kutumia propaganda za miaka yote tangu miaka 1990, ambazo kimsingi zilishashindwa kuwaletea matokeo yanayotarajiwa
 
Yeriko, hilo huhitaji kupigiwa mbiu ili ulijue. Huu mgogoro wa kung'ang'ania majimbo kila chama kinataka kusimamisha wagombea kwenye maeneo yake ni ishara tosha kuwa hakuna tena cha ukawa.

Huna hoja.

Jk akiondoka madarakani utakufa njaa
 
Haya ndo madhara ya kunywa viroba. Ndo maana hata hujui mada inahusu nini. TANU waliungana na ASP wakaunda chama kimoja kiitwacho CCM. Baada ya kuzaliwa CCM, vyama vya TANU na ASP automatically vilikufa. Sasa niambie kama muungano wa TANU na ASP unafanana na huu muungano wenu wa UKAWA
Mimi nimekuuliza tu swali ni kwanini waliungana? Kwa kifupi KANU kilikuwa hakina nguvu Zanzibar vilevile ASP ilikuwa haina nguvu bara, Nyerere aliliona hilo na alimshirikisha Karume kabla ya kufariki 1972 lakini Karume hakukubaliana naye, mpaka alivyofariki ...Nyerere akamvizia Abdu Jumbe 1976 na 1977 wakaunganisha vyama. Ujumbe uliokuwepo hapo ni umoja wa kitaifa. kwanza lete fedha ya tuition siwezi kuendelea kufundisha bogus lilokimbia umande

Back
Top Bottom