DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Akizungumza Jumatatu Agosti 18, 2025 Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa Juma Khatibu katika Mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), mkoani Dar es Salaam, Khatibu amempongeza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa hatua ya kuwaleta pamoja viongozi wa kitaifa na watendaji wa vyama kwa lengo la kutoa elimu na kuimarisha msingi wa demokrasia.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi, tunakupongeza sana kwa kazi nzuri ya ulezi wa vyama vya siasa. Umeona umuhimu wa kutukutanisha hapa ili kupitia Sheria ya Gharama za Uchaguzi, jambo hili ni jema kwa sababu linapunguza kasoro katika uchaguzi wetu,” amesema Khatibu.
Amesisitiza kuwa historia inaonesha baadhi ya vyama na wagombea walikuwa na uelewa mdogo walipotakiwa kuwasilisha taarifa za gharama za uchaguzi, jambo lililosababisha kuibuka kwa kasoro kubwa.