Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Mara nyingine ili Magufuli na serikali yake waelewe kwamba wanafanya unyanyasaji usiokubalika kwa vyama vya upinzani, inatakiwa vyama vya upinzani waje na namna ya kutumia unyanyasaji huo kwa faida yao wenyewe. Wafuasi wa vyama vya upinzani wanapaswa kuelewa siku zote wale wanaopigania haki zao wasitegemee kwamba watapewa haki hizo kwenye sahani ya dhahabu. Historia imeonyesha hivyo.
NI wazi kwamba watu wa vyama vya uinzani mnaonewa sana, na ili msikilizwe anzisheni kampeni zenye kulenga kutumia unyanyasaji mnaofanyiwa kwa faida yenu. Imefikia mahali ambapo mnapaswa kufanya dunia yote ijue mnachofaniwa na soon or later dunia nzima itawasikililiza. Hiyo ndio dawa ya serikali ya Raisi Magufuli na CCM dhidi ya uonevu mnaofaniwa.
Tatizo ni kwamba wafuasi wa vyama vya upinzani mmeacha viongozi wenu wawe ndio chambo cha kunyanyaswa, kufungwa nk. Acheni tabia ya kuwatumia viongozi wenu kuwa ndi wawe wa kukamatwa kila siku. Wala msifanye uhalifu - fanyeni mambo katika masses ambayo hayana mshiko kufunguliwa mashitaka.
Kama mkikusanyika mkutano wa siasa polisi wakaja msikimbie. Mnapokuwa katika umati polisi wakapiga mabomu mkaanza kukimbia hapo ndipo wanapowashinda. Polisi wakija laleni chini wote. Acha wapiga picha waionyeshe dunia mnapigwa marungu mkiwa mmelala chini tuone Magufuli atafika wapi. Hao watu wanaowaita mabeberu watawafanyia kitu mbaya tu maana hawataki ujinga kama huo. Watawapiga kiasi, lakini hawatawaua kwa maelfu, wekeni hilo kichwani.
Wakiwakamata leo kesho tena fanyeni hivyo hivyo, na kesho kutwa na kesho yake. Wakimwaga ugali mwageni mboga.
Hamuwezi kubadili mfumo wa unyanyasaji mnaofanyiwa kwa kuwaweka viongozi wenu mbele kuwa watu wa kuwawakilisha katika kunyanyaswa na kuwekwa ndani. Tumieni huku kuwekwa ndani kama namna ya kupinga kuwekwa ndani . Someni historia za mikakati ya kudai haki na jifunzeni katika hayo. Tatizo ni kwamba serikali ya Magufuli na CCM wanatumia uoga wenu wa mahabusu kuwagawanya na kutia ndani mahabusu mtu mmoja mmoja.
Jifunzeni kutumia vyombo vya habari vya nje kuionyesha dunia unyanyasaji mnaofanyiwa. Mnapoitisha mikutano toeni taarifa kwa vyombo vya habari vya ndani na nje - CNN, BBC, Al Jazira, Sky News, DW etc. Waambieni kinachotarajiwa kutokea ili wajiandae vema kutoa taarifa ya matukio kamba hata hayajafanyika. Hamuwezi kubadili mfumo wa unyanyasaji mnaofanyiwa kwa namna ileile mliyotumia kwa miaka karibu mitano sasa.
Nyie ndio mnaendelea kuumizwa. Sasa ni wakati wa kuja na mkakatai tofauti, na hasa sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi. Kama hawataki kuwasikiliza mnapotumia ustaarabu, dawa ni kufanya kilicha haki yenu kwa kulazimisha, na tuone hizo mahabusu wanazowatisha nazo kama zitawasaidia. Kumbukeni haumwezi kusikilizwa kwa dunia kwa kutumia barua.
Imefikia mahali ambapo mambo mnayofanyiwa na serikali ya CCM chini ya Magufuli na vyombo vyake vya dola yanakera hata sisi tusio na vyama vya siasa. Enough now. Nyie ni Watanzania wenzetu. Kosa lenu nini hasa hadi mfanyiwe yote haya, kuwa wapinzani wa CCM?
Hili halivumiliki wala kukubalika tena! Ni lazima kulibadili, kwa namna moja au nyingine