Vyakula na life style katika umri wa 40+

Vyakula na life style katika umri wa 40+

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
8,588
Reaction score
14,194
Kwa uzoefu wangu mdogo nimebaini Watanzania wengi sana tunapofikisha miaka around 40 tunaanza kupata changamoto nyingi sana za kiafya zinazo weza kuzuilika kutokana na life style zetu.

Ukiachana na kutofanya mazoezi swala la ulaji na aina ya vyakula tunakula lina beba taswira kubwa sana ya changamoto za maradhi kadiri umri unavyokwenda.

Lakini pia kuna swala la kutokufanya mazoezi na mentality za kustaafu zina fanya wastaafu wengi sana kufa mapema au kwa mateso kwa changamoto za kiafya zinazo zuilika.

Naamini hapa JF wapo wataalamu lakini wapo pia ambao wanajua mambo haya kupitia uzoefu nk
Nimatarajio yangu watatujuza mambo haya muhimu tuyaepuka tufurahie uzee wetu.

Karibuni kwa madini na nondo zaidi.
 
Sukari na pressure na heart attack inaweza kuzuilika Kama tukizingatia lifestyle nzuri.

Kula kiasi kidogo usile ukashiba Sana...kwa mfano chapati mbili na bakuli la choroko inatosha kbs..nyama sio nzuri..pendelea sana maziwa mtindi.

Ugali na wali haufai...matembere na kabeji NI mboga nzuri sana..matunda mazuri kbs duniani NI tikitimaji na tango.

Kumbuka kunywa maji Lita zaidi ya nne kwa siku.mazoezi ya kukimbia na ya kutoa jasho NI mazuri...epuka pombe sio nzuri sana
 
Asanteni Mungu awabariki kwa ushauri huu mzuri
Nadhani thread hii idumu kwa ushauri na maelekezo
 
Punguza nyama ongeza mboga za majani, maharage na matunda.

Maji litre mbili kwa siku. Tembea hata kwa nusu saa kila siku.

Punguza pombe

Kama utaweza breakfast pata ndizi mbivu, papai na mayai mawili ya kuchemsha

Lunch ukiweza kupata samaki mzima na mboga mboga

Jioni vijiko viwili vya wali unajazia maharage juu.
 
Mh

Mh,ntaweza kweli hivi mimi!!
 
Daah hapo kwenye kupunguza pombe sasa , mi bila tubia tuwili kwa kweli silali. mazoezi nafaya sana na tayari nimegonga 45. Mungu atusaidie tustaafu na afya zetu
 
Sukari na pressure na heart attack inaweza kuzuilika Kama tukizingatia lifestyle nzuri.

Kula kiasi kidogo usile ukashiba Sana...kwa mfano chapati mbili na bakuli la choroko inatosha kbs..nyama sio nzuri..pendelea sana maziwa mtindi.

Ugali na wali haufai...matembere na kabeji NI mboga nzuri sana..matunda mazuri kbs duniani NI tikitimaji na tango.

Kumbuka kunywa maji Lita zaidi ya nne kwa siku.mazoezi ya kukimbia na ya kutoa jasho NI mazuri...epuka pombe sio nzuri sana
Mbona Babu zenu walikuwa wanakula tena nyama mbichi na waliishi miaka mingi tu-hayo ya kutokula nyama wewe umeyatoa wapi?
 
Huyu dingi ana miaka 71 ona alivyo.
Anakwambia kula mlo mmoja kwa siku, usile vyakula vya kukaanga, pendelea choma na chemsha.

usinywe soda wala juice za kopo, kula matunda natural.
 
Punguza nyama ongeza mboga za majani, maharage na matunda.

Maji litre mbili kwa siku. Tembea hata kwa nusu saa kila siku.

Punguza pombe

Kama utaweza breakfast pata ndizi mbivu, papai na mayai mawili ya kuchemsha

Lunch ukiweza kupata samaki mzima na mboga mboga

Jioni vijiko viwili vya wali unajazia maharage juu.
Vijiko viwili vya wali???? Mbona ntakuwa nalala na njaa kila siku!!!
Im a big fan wa "i love to eat diet " hiyo sukari na pressure mungu tu anisaidie , natembea 3km wastani kila siku , na maji nakunywa 4 plus litters per day
 
Kwakweli tena ukute wali wa nazi
 
Huyu dingi ana miaka 71 ona alivyo.
Anakwambia kula mlo mmoja kwa siku, usile vyakula vya kukaanga, pendelea choma na chemsha.

usinywe soda wala juice za kopo, kula matunda natural.

Maisha hayana formula mkuu na yapo very brutal for those who plan for it.
Corona imeua sana first class pattients , hohehae wengi wame survive,

A 109 years old ww2 us veteran , alifariki akiwa na miaka 112 , a pack of 20 cigarates was his daily dose ,
 
Huyu dingi ana miaka 71 ona alivyo.
Anakwambia kula mlo mmoja kwa siku, usile vyakula vya kukaanga, pendelea choma na chemsha.

usinywe soda wala juice za kopo, kula matunda natural.

Kuna mmoja nilikutana nae kazini ni dada wa Kijamaica, anasema alianza tangu akiwa na miaka 30 aliacha pombe, vyakula vyake anakula organic tu matunda mengi, samaki na mboga mboga, aliacha kunywa chai na kahawa anakunywa chai ya mchai chai tu.
Ukimuona ni kama ame baki pale pale 30 ingawa sasa ana 60.
 
Kuna mmoja nilikutana nae kazini ni dada wa Kijamaica, anasema alianza tangu akiwa na miaka 30 aliacha pombe, vyakula vyake anakula organic tu matunda mengi, samaki na mboga mboga, aliacha kunywa chai na kahawa anakunywa chai ya mchai chai tu.
Ukimuona ni kama ame bali pale pale 30 ingawa sasa ana 60.
Ona huyu babu ana miaka 92 anapiga mazoezi ya kutosha.

Babu anasema hataki kuugua ugua magonjwa ya kijinga kwani hataki kua mzigo kwa watu wengine.

Kwa uzoefu wangu mdogo nimebaini Watanzania wengi sana tunapofikisha miaka around 40 tunaanza kupata changamoto nyingi sana za kiafya zinazo weza kuzuilika kutokana na life style zetu.

Ukiachana na kutofanya mazoezi swala la ulaji na aina ya vyakula tunakula lina beba taswira kubwa sana ya changamoto za maradhi kadiri umri unavyokwenda.

Lakini pia kuna swala la kutokufanya mazoezi na mentality za kustaafu zina fanya wastaafu wengi sana kufa mapema au kwa mateso kwa changamoto za kiafya zinazo zuilika.

Naamini hapa JF wapo wataalamu lakini wapo pia ambao wanajua mambo haya kupitia uzoefu nk
Nimatarajio yangu watatujuza mambo haya muhimu tuyaepuka tufurahie uzee wetu.

Karibuni kwa madini na nondo zaidi.

Bandiko hili la mdau nimelielewa sana [emoji116][emoji116][emoji116]

Kwema Wakuu!

Hatufuatiliani wala hatupangiani maisha. Ila tunakumbushana huku nami nikijikumbusha pia Kwa Nia nzuri tuu. Ili baadaye tusijekujikuta katika Huzuni kuu.

Vijana tunapoambiwa tule na tunywe Kwa nidhamu sio Kwa sababu tunaonewa wivu au kuna mtu anataka kuwa juu yetu Kwa kutupa amri. HASHA! Bali ni kwa faida yetu.

Kisukari na Presha sio magonjwa mazuri Kwa ustawi wa Ndoa zetu. Ukisikia pigo Baya basi ni kukosa nguvu za kiume. Tena Kwa miaka 40 Kwa mwanaume bado ni kijana. Na Kwa bahati nzuri miaka hiyo wengi neema ndio zinazidi kufunguka na wamesha-settle. Sasa ume-settle halafu unajikuta huna nguvu za kiume. Asikuambie mtu inahuzunisha sana.

Presha na kisukari yatakufanya ukose Raha ya maisha sio tuu kwenye ndoa Bali hata katika ulaji wako. Utapangiwa nini ule na kipi usile. Vyakula vizuri utabaki kuvitazama tuu, utakula chukuchuku na michemsho mpaka Ulie.

Ni akheri ujipangie sasa hivi Kula Milo mizuri Kwa kufuata kanuni za Afya ya Mwili. Na ni akheri magonjwa hayo yakupate too late yaani huko miaka ya 80+ lakini sio 40+.

Ni hatari na utateseka Sana. Miaka 80+ huna ulichobakiza, hata wewe mwenyewe utakiri kuwa umekula chumvi nyingi vyakutosha. Lakini sio miaka 40-60. Hiyo ni miaka michache Sana.

Ukiona Taikon anaelezea jambo fulani basi kaa nalo macho, lizingatie Sana. Kwa sababu Taikon nipo kwaajili ya kujenga na wala sio kubomoa.

1. Kula na kunywa vizuri
i. Kula Mbomboga Kwa wingi, kula Protein Kama nyama nyeupe, maziwa, mayai, Kwa wingi,
Kula wanga kidogo Sana. Mfano unapika maharage mengi halafu unakula na wali kidunchu, au ugali kidogo na Samaki au nyama au maharage mengi.

ii. Matunda, pendelea Kula matunda
Kama umeoa, pendelea Ndizi zilizoiva angalau kila siku moja hasa usiku, hii itafanya uume wako kuwa na nguvu kutokana na madini ya Potassium.

Mkeo aweke Kachumburi yenye Nyanya, vitunguu, limao na pilipili hizi zinaongeza Libido.
Safisha figo Kwa Matikiti, matango, usisahau mapapai na maembe, pia machungwa huku utapata vitamini

Weka chumvi kiasi yenye ladha ya Kwa mbali. Usiweke chumvi nyingi. Kuweka chumvi nyingi kuna sababisha hatari ya kupata Presha "Hypertension" ambayo sio nzuri Kwa Afya yako.

Kula Milo miwili ukiwa age ya 25-50 iwe balanced.

iii. Kunywa maji mengi, angalau Lita mbili na nusu mpaka tatu na nusu Kwa siku
Pombe kunywa kiasi Kwa STAREHE sio kujiumiza. Angalau kwa wiki mara moja na hakikisha usinywe mpaka ukazima.

Maji mengi ni dawa kwani yanafanya seli za mwili wako kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi. Maji hupunguza pia sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa na Nuru.

Yaani mtu anayezingatia kunywa maji ngozi yake hung'aa

Pia maji mengi husababisha mtu kutokuzeeka Kwa haraka. Na hii ni kutokana na Uzalishwaji wa seli za mwili kufanyika Kwa ufanisi

2. Fanya mazoezi
Mazoezi hujenga mwili na kuufanya kuwa na Afya, kwani hufanya mzunguko WA damu kufanya kazi vizuri. Kumbuka Damu ndio hubeba virutubisho na kuvisafitisha mwilini. Kumbuka pia ndani ya damu ndio kuna Seli nyeupe zinazolinda mwili dhidi ya magonjwa, Seli nyekundu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kuzipa Seli, tishu na ogani Uhai. Hasahasa Ubongo.

Hii ni kusema mazoezi yanaimarisha ufanyaji kazi WA viungo vya Mwili Kama vile Ubongo. Hii inafanya akili kuwa active.

Aina ya mazoezi

i. Mazoezi ya Mwili

Haya yanalenga zaidi viungo na organ za mwili. Kukimbia, Push-up n.k.

ii. Mazoezi ya Akili/Ufahamu

Haya yanalenga zaidi tafakuri, uchanganuzi, uchambuzi, n.k. haya ni Kwa kusoma Nyaraka na vitabu, michezo na Bangua bongo, Game zinazoshughulisha akili n.k Pia mazoezi ya ubongo hufanyika Kwa kujaribu kufanya vitu vipya ili kutafuta changamoto mpya. Kama ni biashara, au kazi au miradi unaanzisha ili akili ipate changamoto mpya.

iii. Mazoezi ya Kiroho na Nafsi

Haya hulenga zaidi roho na Nafsi yako. Kudhibiti Nafsi yako na matamanio yake, mfano Kufunga Kula na kunywa. Kama unapenda kunywa pombe kujizuia kutokunywa Kwa muda wa siku kadhaa. Kama unapenda Kulala na wanawake, kujizuia hata Kwa miezi sita bila kuchepuka, hayo ni mazoezi ya kiroho na nafsi.

Pia kutoa Zaka au Sadaka Ile inayouma. Ni zoezi la Nafsi au kiroho.

Hii itakusaidia kujidhibiti, pia kuzuia Nyege mshindo au ukosefu wa maamuzi.

3. Mapumziko na Burudani/STAREHE

Angalau Kwa siku ulale masaa yasiyopungua Nane. Starehe au burudani angalau Kwa wiki au Kwa mwezi mara moja. Hii itakufanya usiyachoke maisha na kuyaona hayana maana.

Usingizi utakusaidia kutunza Ubongo wako na hii itakusaidia nyakati za uzeeni kwani utakuwa haupotezi kumbukumbu kijinga jinga.

Kabla watu hawajaona uzee wako wewe mwenyewe utaanza kuuona Kwanza Kwa kujikuta unasahau sahau mambo, na hiyo huanza kutokea miaka 30+ kama hutokuwa mtu wa kuzingatia mapumziko.

Kijana wa sasa unapaswa ujidhibiti mwenyewe ili isijekula kwako ufikishapo miaka 40. Hakuna kitu kibaya Kama kufikisha umri huo yaani 40+ halafu ujikute hauna pesa, halafu magonjwa Kama kisukari na Presha vikupige. Ni hatari Sana.

Kupigiwa nje nje! Yaani mwanamke wako wala hatakuwa na Woga, nawe utakuwa unajua na chakumfanya hauna.

Wale mnaolalamika andiko refu nimewasikia. Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom