A
Anonymous
Guest
Mimi kwa taaluma yangu ni mwalimu. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikihangaika kutafuta ajira serikalini kupitia Ajira Portal. Nimekuwa nikifanya usaili mara kwa mara, napita hatua ya maandishi hadi kufika hatua ya mahojiano ya ana kwa ana (oral), lakini mwisho wa siku sipati nafasi.
Kinachoniumiza zaidi ni kwamba umri wangu umeenda—nina miaka 35 na zaidi—lakini hali yangu inalinganishwa moja kwa moja na wahitimu waliomaliza vyuo juzi tu. Ukweli ni kwamba, nimekaa mtaani kwa zaidi ya miaka 10 nikijaribu kila njia, lakini bado ninapewa nafasi sawa ya ushindani bila kuzingatia uzoefu na muda niliopambana.
Inakatisha tamaa sana. Unajituma hadi kufika hatua ya mwisho ya usaili, lakini hakuna kinachobadilika.
Vilevile, ninaona changamoto kwa waombaji wenye ulemavu. Wapo wanaofika hadi hatua ya mwisho ya mahojiano na wana vigezo vyote, lakini bado hawapati nafasi. Hii inaumiza zaidi, kwa sababu wanapaswa kupewa kipaumbele au angalau kuangaliwa kwa jicho la ziada kutokana na hali zao.
Kwa kweli hali hii inahitaji kuangaliwa upya.
Mapendekezo yangu:
Kuwe na utaratibu wa kuzingatia umri na muda tangu mhitimu amalize chuo katika mchakato wa ajira.
Mfano, kwa waombaji wenye miaka 35 na zaidi na waliomaliza muda mrefu, vigezo vya ufaulu viwe na mlinganisho tofauti na wahitimu wapya.
Pia soma ~ Sekretarieti ya Ajira: Kuna muda umri unazingatiwa kwenye usaili wa ajira lakini kwanza unatakiwa kufaulu

- Endapo msahiliwa mwenye umri mkubwa atafikisha angalau alama 50 au zaidi katika usaili, apewe kipaumbele, kwa kuzingatia jitihada na muda aliopambana.
- Kwa waombaji wenye mahitaji maalum (ulemavu), endapo wamekidhi vigezo na kupata alama za kutosha (mfano 50 na kuendelea), wasaidiwe kupata nafasi za ajira kama sehemu ya kuwajali na kuwapa usawa wa fursa.