Vurugu kubwa shule ya sekondari Lyamungo leo tarehe 1 March 2018. Shule yafungwa!

VURUGU KUBWA SHULE YA SECONDARI LYAMUNGO LEO HII TAREHE 1 MARCH 2018 HALI SII SHWARI

Hali sio shwari hata kidogo katika shule ya sekondari Lyamungo iliyoko wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, kilichopelekea mkuu wilaya ya Hai kufunga shule hiyo kwa muda kukwepa hasara zaidi, huku ofisini ya mwalimu wa nidhamu na ofisini ya mkuu wa shule vikiharibika vibaya sana.

Vurugu hizi zilianza katika uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo mwanafunzi mmoja mtukutu aliwatukana waalimu na wanafunzi wa shule katika kura alizopiga. Uongozi wa shule pamoja na walimu walishirikiana kubaini mwandiko wa mwanafunzi huyo, ndipo ugomvi ulipoanzia Kitendo cha uongozi wa shule kumfukuza shule mwanafunzi huyo ndio chanzo cha vurugu zote hizo.

Waliofanya vurugu walikua wanapinga huyo mwenzao asifukuzwe shule au walikua wana support?
 
Huo ni utovu wa nidham, mwanafunzi kutukana waalim kwa sababu za kijinga.

Hiyo hasara wazazi wao watalipa.
Wamehisi kua huyo mwanafunzi ndie kawatukana, sababu hapakua na mtaalamu wa kukagua mwandiko would you please think like a living creature
 
Hapo mpaka usikilize story ya upande wa pili ya wanafunzi isiaminike tu stori ya waalimu.

Mimi pia nimesoma hio shule naifahamu kiasi, kuna kipindi cha nyuma tuliandamana, kulikuwa na ugonjwa wa tumbo shuleni, mwanafunzi mwenzetu akaomba ruhusa kwenda nyumbani anaumwa sana tumbo, wakamkatalia, akakaa nje ya ofisi ya waalimu hadi akafariki hapo hapo, walimu wakaizima zima na report kutoka wakadai ni malaria tu.

tuliandamana hadi wakafukuza shule O level wote na kubakisha form IV tu waliokuwa wanamaliza. waliofukuzwa wakapelekwa shule za kata.
Mkuu kumbe na wewe ulisoma hapo nakumbuka tuligoma kula chakula pia nilikuwa form 3 i think, nadhani wanafunzi watakuwa na reason behind sio hiyo tu ambayo imesemwa hapo
 
VURUGU KUBWA SHULE YA SECONDARI LYAMUNGO LEO HII TAREHE 1 MARCH 2018 HALI SII SHWARI

Hali sio shwari hata kidogo katika shule ya sekondari Lyamungo iliyoko wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, kilichopelekea mkuu wilaya ya Hai kufunga shule hiyo kwa muda kukwepa hasara zaidi, huku ofisini ya mwalimu wa nidhamu na ofisini ya mkuu wa shule vikiharibika vibaya sana.

Vurugu hizi zilianza katika uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo mwanafunzi mmoja mtukutu aliwatukana waalimu na wanafunzi wa shule katika kura alizopiga. Uongozi wa shule pamoja na walimu walishirikiana kubaini mwandiko wa mwanafunzi huyo, ndipo ugomvi ulipoanzia Kitendo cha uongozi wa shule kumfukuza shule mwanafunzi huyo ndio chanzo cha vurugu zote hizo.

Katumiwa na ule mchama ambao karibu ufungwe
 
Hapo wengine hawana hata nauli za kwenda makwao RAIA wa kanda ya ziwa mkawachukue ndugu zenu huko moshi wasije wakachomwa kama ndafu
 
Nimekumbuka enzi hizo nipo Mara sekondari tulipigana na maporisi wakashindwa JW wakaitwa ndo ikawa mwisho wa vurugu.niwashauri vijana wasome waache ujuha.
We kweli wa Mara ...hata mwandiko wako unaonesha
 
Sawasawa madogo ,lianzisheni hukohuko shuleni ili lizambae huku mtaani, itaturahisishia April 26/2018
 
MOSI,SERIKALI IHAKIKISHE KILA MZAZI ANALIPA HASARA ILIYOTOKEA HAPO SHULENI ILI WAJUE WAKIWA HAPO KUNA WENGINE KODI WANALIPA ILI WASOME
PILI,SUSPENSION KM SEHEM YA ADHABU WAKAJIFUNZE KUKAA NYUMBANI WAJUE KILICHOWAPELEKA
TATU,WAHAMISHWE WATAWANYWE KILA MKOA WAFUATILIWE MIENENDO YAO KILA MMOJA BAADA YA KUTOKA HUKO
 
Walimu tuna tabia za kusingizia sana wanafunzi hasa ukitokea msala ambao umesababishwa na walim wenyew usikute kuna kitu kipo nyuma ya pazia in a real sense mwanafunzi hawezi andika matusi kwa mwandiko wake wa kawaida,,alafu kwenye kuandika na kila mtu kuchukua karatasi yake alopigia kura utajuajae kama hii yako au sio wakati zote zinakua ,inafanana na zinakua zimefungwa ni uongo tupuu
 
Back
Top Bottom