Vuai Nahodha rais 2015!

Dr Shein ngekewa ilivyomuangukia kwa Mhe Mkapa hadi sasa kuiongoza Zanzibar TULIVU nadhani busara zitamuongoza kutojitafutia presha zaidi baada ya hapo badala kwenda tu kupumzika nyumbani na kubakia na cheo cha kudumu cha MSHAURI wa taifa kama walivyo Wazee watu wengine ambao ni WAADILIFU kama yeye.
 
Bruce lee sikujua kama ungeniharibia alfajiri yangu hivi kwa kutaja hilo jina. Natoka kidogo kwenye huu mjadala.
 
hizo ni tetezi tu bado mambo ni magumu huko CCM kama sio kupeana madaraka sasa hivi CCM ingekuwa imesambaratika kama KANU huko Kenya maana wanaotajwa wapo wengi mimi naomba tusijadili hili la 2015 bali tuangalie mada yetu

KATBA KATIBA ni njia zipi zitumike kupata katika mpya na tume ya uchaguzi huru?? Nisaidieni wana JF
 
Lolote linawezekana ila usisahau genda - Rose Migiro na Anna Tibaijuka,na hivi ccm inajitahidi 50 50 kwenye nafasi za mmamuzi usijeshangaa wanashindanishwa akina mama peke yao ili kuondoa makundi
 
Itakuwa ni ndoto kwa hali ya sasa Mzanzibar kutawala Tanzania!Never ever!!hili sio shamba la bibi yao!!
 
Sasa naona ile sera ya udini ndio itakapotimia! This is Craaaaaap!
 
Lolote linawezekana ila usisahau genda - Rose Migiro na Anna Tibaijuka,na hivi ccm inajitahidi 50 50 kwenye nafasi za mmamuzi usijeshangaa wanashindanishwa akina mama peke yao ili kuondoa makundi

unakuwa kama huifahamu CCM? Jinsi ccm ilivyotawaliwa na rushwa huyo Migiro na Tibaijuka nani atawapitisha? kamati kuu imetawaliwa na watu wa Lowassa na ndio maana waliweza kumwondoa Sitta kwenye uspika. Mtu anayeungwa mkono na Lowassa atapitishwa kugombea nionavyo mimi na atapigwa chini na mgombea wa CHADEMA. Usishangae sana Sitta akagombea urais kupitia CHADEMA. Na maneno ya mwalimu kuwa mpinzani ambaye atashinda urais atatokea CCM utatimia 2015. Chadema kwa sasa inabidi waanze kuchukua mazoezi/rehearsal ya kutawala nchi. Na kwa kweli napenda mgogoro wa Zitto maana itawapa uzoefu wa kuongoza watu wenye mawazo tofauti.
 
Tumeona Marais wakatolic, waislamu, na Waziri Mkuu mara nyingi ni Mlutheri kasoro Pinda.
2015 ni zamu yetu sisi mnaotuita wapagani, mwone tutakavyoibadilisha nchi hii.
Dini zenu zinawafanya mwe vipofu wa kupendelea na kuchaguana kwa misingi ya dini.
 
Kwa cdm kutwaa urais ninaiona kama ndoto hasa tuhuma za udini na ukabila zimewaharibia,sema wanaweza kuweka changamoto lakini sio kutwaa urais.Kuisafisha cdm tokana na tuhuma za udini itakuwa kazi kama ilivyokazi kwa cuf.Waislam wengi wanaigopa cdm kama ilivyo kwa wakristu wengi kwa cuf.Na hii inaiweka ccm katika nafasi ya kuendelea kutawala kwa muda mrefu ujao
 
Lets deal with the issue which is currently on round table. It's too early to speculate that.
If you are good in that, then tell us who is going to be the Mayor/RC for Dar-es-salaam.
 
QUOTE=KALAMAZOO;Kwa cdm kutwaa urais ninaiona kama ndoto hasa tuhuma za udini na ukabila zimewaharibia,sema wanaweza kuweka changamoto lakini sio kutwaa urais.Kuisafisha cdm tokana na tuhuma za udini itakuwa kazi kama ilivyokazi kwa cuf.Waislam wengi wanaigopa cdm kama ilivyo kwa wakristu wengi kwa cuf.Na hii inaiweka ccm katika nafasi ya kuendelea kutawala kwa muda mrefu ujao

A very polarised analysis!
 
Kwa hali inavyoenda sasa, itakuwa ni vigumu sana kupata Rais wa JMT kutoka Zanzibar miaka ya karibuni mpaka mtazamo wa Wazanzibari wengi na hasa viongozi kuhusiana na mwungano utakapobadilika. Wazanzibari walipoteza nafasi yao Salim Ahmed Salim alipogombea. Huyu Watanzania wengi walikuwa wanamfahamu na hakuna wakati wowote ambapo amewahi kushiriki katika jitihada za kuifanya Zanzibar ijitenga na Tanganyika. Hata kumpeleka Dr Shein kuwa Rais wa Zanzibar ni katika jitihada za Tanzania bara kuzima jitihada za viongozi wa Zanzibar akiwemo Nahodha kuendelea na jitihada zao za kuzidi kuudoofisha mwungano na kuifanya Zanzibar iendelee kujitenga taratibu. Kosa kubwa alilofanya Nahodha ni kushiriki katika kuifanya Zanzibar kuwa dola.

Mazingira ya Mzanzibari kuwa Rais wa JMT wameyaharibu wenyewe kiasi kwamba wanatiliwa mashaka hata ndani ya CCM yenyewe. Viongozi wengi wa kutoka Zanzibar, akiwemo Nahodha ndio ambao wakiwa Zanzibar wamejitahidi sana kuhakikisha kwamba Zanzibar inakuwa automous state. Hawaonekani kuwa ni watu wenye dhamira hasa ya kuiona Tanzania siku moja ikiwa moja yenye watu wamoja.

Mabadiliko ya katiba na tume huru ya uchaguzi ni lazima vitafanyika kabla ya uchaguzi wa 2015, na hivyo CCM haitawezi kuhatarisha hali yake kwa kumweka mgombea ambaye hataungwa mkono hata na wana CCM wenyewe.
 
Tumeona Marais wakatolic, waislamu, na Waziri Mkuu mara nyingi ni Mlutheri kasoro Pinda.
2015 ni zamu yetu sisi mnaotuita wapagani, mwone tutakavyoibadilisha nchi hii.
Dini zenu zinawafanya mwe vipofu wa kupendelea na kuchaguana kwa misingi ya dini.

Mpagani akitawala nchi tumekwisha, maana hata kula nyama za watu mchana kweupe ruksa!
 
Vuai Nahodha kuwa raisi sidhani kama itawezekana hata kama CCM wakimsimamisha.. Ila ngoja tuone utendaji wake Wizara ya ndani kwanza... kuondoa kero ya polisi na trafic na kupunguza mkundikano wa wafungwa magerezani pamoja na vitambulisho vya taifa.

Nasema CCM hawatashinda kwa sababu najua Chadema watashinda 2015... That is for Sure!!
 
Back
Top Bottom