Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Rais Magufuli: Viongozi Wastaaafu wote katika maeneo yote tutawalinda, watachonga weee, watasema ila mna mchango mkubwa ktk Taifa hili
Rais Magufuli: Leo ilikuwa ni hafla fupi namimi nimeona niongee mafupi, nawashukuru viongozi wote mliofika tupo pamoja.
Rais Magufuli: Mchakato wa Katiba ulifika mahali pazuri sana, kazi imefanyika kubwa, tumefikia mahali pazuri.
Rais Magufuli: Niko pamoja na wanasiasa wenzangu, tutashirikiana, ushauri wao nitaupokea kwa mikono miwili.
Rais Magufuli: Tumeamua kufanya kazi tutashirikiana kufanya kazi na vyama vyote katika kuhakikisha tunatatua kero
Rais Magufuli: Nisingependa kuona mtu yeyote ananichelewesha kutekeleza hayo niliyoyaahidi kuyafanya ndani ya miaka 5
VIDEO: Katazo la Mikutano ya Kisiasa hadi 2020
Rais Magufuli: Ni matumaini yangu Watanzania tunaowaongoza wanataka maendelo, kuona kero zinaondolewa
Rais Magufuli: Uchaguzi umeisha na hakuna aliyeshinda wala aliyeshindwa watanzania wote wameshinda
Rais Magufuli: Kama ofisi ya Tume ya Uchaguzi mtaijenga Dodoma, hata vyama vya siasa vitahamia Dodoma
Rais Magufuli: Kuhamia Dodoma tutakuwa tunamuenzi Baba wa Taifa ambaye alisema Dodoma ndio makao makuu
Rais Magufuli: Nilishuhudia ukubwa wa changamoto hii (kukosa jengo la ofisi) niipoenda kuchukua fomu za urais.
Rais Magufuli: Rais Mstaafu Kikwete kaa upumzike kwa raha zako usisikilize kelele za nje, wewe upo salama.
Rais Magufuli: Nitumie fursa hii kuwapongeza ZEC na wananchi wa Zanzibar kwa kurudia uchaguzi kwa usalama
Rais Magufuli: Wengine wamekosoa ili mradi tu wamekosoa, sishangai maana imekuwa tabia kwao.
Rais Magufuli: Wakosoaji wametoa kasoro za makundi mawili, wengine wametoa mapungufu ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi.
Rais Magufuli: Zipo baadhi ya kasoro zilizojitokeza, jambo hilo lisiwanyime raha.
Rais Magufuli: Uchaguzi ulikuwa wa kipekee sana kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kutumia BVR, ulikuwa na ushindani mkali, wenye mvuto na msisimko
Rais Magufuli: Uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wenye ushindani mkali, ulikuwa wenye mvuto ndani na nje ya nchi.
Rais Magufuli: Mh. Mwenyekiti uchaguzi ni tukio muhimu katika nchi, uchaguzi usipo simamiwa vizuri huwa huleta migogoro ktk nchi.
Jaji Lubuva: Kura ya maoni ya Katiba mpya ipo palepale kilichobadilika ni ratiba tuu sasa naomba nikukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Jaji Lubuva: NEC na ZEC zitaanza kushugulikia kura ya maoni,kuangalia sheria ya kura ya Maoni itakavyofanyiwa marekebisho
Jaji Lubuva: Shughuli hii ya leo ndio hatua ya mwisho ya ukamilishaji wa uchaguzi wa mwaka 2015.
Jaji Lubuva: NEC imeweza kuwa na daftari la kudumu na la kuaminika ambalo linaweza kutumika kwa chaguzi zijazo'-
Jaji Lubuva: Uchaguzi wa 2015 ulimalizika kwa amani, ufanisi, na wengi wanakubaliana uchaguzi ulikuwa huru na wa haki ni wachache tu ndio waliweka mambo yasiyohusika.
Jaji Lubuva: Katika chaguzi nne zilizopita, tumekuwa tukitoa mapendekezo baada ya uchaguzi lakini hayafanyiwi kazi
Jaji Lubuva: Changamoto zilizojitokeza tutajitahidi katika chaguzi zijazo kama Tume ya Uchaguzi NEC kuboresha.
Jaji Lubuva: Kuchelewa kupatikana kwa fedha kwa shughuli za uchaguzi, kutoa elimu kwaajili ya wapiga kura ni changamoto
Jaji Lubuva: Mh.Rais taarifa inaonyesha mchakato mzima toka awali mpaka mwisho wa uchaguzi wa mwaka jana 2015.
Jaji Lubuva: Ripoti ya Uchaguzi anayokabidhiwa Rais Magufuli ipo ktk Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kiingereza
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva akisoma ripoti ya tume mbele ya Rais.
Mkurugenzi NEC Kailima Ramadhan, akitoa taarifa maalum ya tume hiyo kwa Rais.
Rais Magufuli amewasili katika ukumbi Ikulu Dsm katika hafla ya kukabidhiwa ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
===============
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo inatarajia kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2015 kwa Rais John Pombe Magufuli.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw.Ramadhani Kailima kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.
Ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Mwaka 2015 itafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambapo Tume imepewa majukumu ya kuendesha Uchaguzi wa Rais na wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uchaguzi wa Madiwani kwa upande wa Tanzania bara.
Kukamilika kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakamilisha mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuashiria kuanza kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.