Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,

Japo siku zote Nabii huwa hakubaliki nyumbani, hili nalijua na litabezwa, na nimeisha lisemea humu
TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums

Hii ni thread ya maono ya unabii, na sio utabiri na sio trends reading, ni unasikia tuu sauti inakuambia jambo fulani bila kuambiwa sababu na huwezi kuuliza, hivyo nami naomba kuwaeleza tuu sauti niliosikia na naomba msiniulize kitu kwasababu sio mimi ni sauti!.

Leo nilikuwa naangalia jinsi Bunge la Marekani, the Congress linavyomshughulikia rais wa Marekani, Donald Trump, ambapo azimio la kumshitaki kwenye Bazara la Senate limepitishwa, japo kule Senate itakuwa ni ngumu kwa azimio hilo kupata ile theluthi 2 ya kumuondoa ila kumshitaki tuu rais ni hatua kubwa.

Kuna mchangiaji mmoja akasema hata Tanzania ikithibitishwa rais Magufuli amevunja katiba kwa kuzuia mikutano ya siasa kinyume cha katiba, anaweza kushtakiwa!.

Ndipo nikauliza ni Bunge lipi hilo la kumshitaki Rais Magufuli?, nikauliza kama ni Bunge hili hili la Mhe. Ndugai au ni Bunge lijalo?, na ndio mara ghafla nikasikia sauti from within, ikiniambia kuwa "Spika ajaye ni Mhe. Dr. Tulia Akson. Sauti hiyo ikaniambia japo Mhe. Ndugai, atakuwa anatamani sana kuendelea kuwa Spika, lakini Ndugai hatakuwa kwa sababu fulani, (japo sauti hiyo imenieleza hizo sababu za kwa nini Mhe. Ndugai hataendelea kuwa Spika Bunge lijalo, lakini sio lazima kusema kila unachosikia, kwa sababu sometimes sio kila unachosikia from within ni sauti kutoka kwa Mungu au ni maono, sauti nyingine ni sauti za shetani tuu na sio sauti za Mungu, kama zilivyo ndoto nyingine, ni ndoto za shetani kama ile "ndoto ya Lema", ukisikia sauti ukahisi inaweza isiwe sauti ya Mungu, au ukiota ndoto ya jambo la ajabu ajabu ukahisi jambo hilo sio la kheri, sio lazima uliseme). Mfano ni tangu August 14, 2014 nilielezwa rais ajaye wa Tanzania ni Magufuli, na nilielezwa sababu kwanini ni Magufuli, nami nikaeleza humu lakini sikuzisema.
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums

Hili la kutokusema kila unachokisikia, nimelisisitiza hapa
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa? - JamiiForums

Jambo tangu baada ya Spika Sitta, trends za uspika zimeonyesha kiti cha Spika ni just one term only na term hiyo ikiisha, Naibu Spika ndio huwa Spika. Wakati wa Spika Sitta, Naibu Spika alikuwa Anna Makinda, japo Sitta alitamani kuendelea, aliwekwa pembeni, Naibu wake Anna Makinda akachaguliwa kuwa Spika. Wakati wa Spika Anna Makinda, Job Ndugai alikuwa Naibu Spika, baada ya Makinda kumaliza one term yake, Naibu wake Job Ndugai akawa Spika, hivyo trends zinaelekeza baada ya Spika Job Ndugai, automatically, Spika anayefuatia ni Naibu Spika Dr. Tulia Akson, ila hili sio bandiko la trends za uspika ni bandiko la " Voices from Within".
Sauti, "Voices From Within" ni Nini?.
Voices from within ni sauti kutoka ndani yako, ndani ya moyo wako, ndani ya nafsi yako, ndani ya dhamira yako, yaani unasikia tuu sauti fulani ikikumbia kitu kutoka ndani yako. Sauti hiyo inaitwa moyo, Kiingereza wanaita conscious, au dhamira, mara nyingi hutokea unapotaka kufanya jambo fulani, unajisikia kama kusita sita, au unapotaka kusafiri unajisikia kama roho inakataa, usilazimishe, hicho unachosikia ndio conscious yenyewe, ni sauti ya Mungu iliyo ndani yako, ama inakupa maona fulani, taarifa fulani, kukuonya usifanye jambo fulani, au kukuonyesha jambo fulani litakuja kutokea in future.

Jee Voices From Within ni Sauti ya Nani?, Ni Sauti ya Mungu, Shetani, Sauti Yako?. Mungu na Shetani ni Nani?.
Tuanze na Mungu, Mungu ndie Muumba wa Vitu vyote, japo kuna hoja kuwa kila jambo lina mwanzo na lina mwisho, hairuhusiwi kutatafakari Mungu alianzaje, bali inaelezwa kuwa Mungu hana mwanzo wala hana mwisho, ni Alfa na Omega. Na inaelezwa Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote, wengi wakidhani hata shetani Mungu ndie alimuumba!. Inaelezwa tuu kuwa shetani mwanzo alikuwa ndiye malaika mkuu, the 2nd in command baada ya Mungu.

Japo haijaandikwa popote, something is telling me mwanzo wa Mungu ndio huo huo mwanzo wa shetani, source of powers za Mungu ndio the same source of powers za shetani, ila Mungu ana nguvu zaidi ya shetani.

Kama ni kweli Mungu ndio aliumba kila kitu akiwemo shetani, halafu Mungu akampa shetani mamlaka ya kuwa the second in command, haiwezekani shetani aumbwe na Mungu, apewe nguvu na Mungu, halafu shetani huyo ataka kumpindua Mungu na yeye ndiye awe Mungu!. Simple logic inaelekeza shetani hakuumbwa na Mungu, bali mwanzo wa Mungu ndio mwanzo wa shetani, source of powers za Mungu ndio the same source of powers za shetani, ukiondoa uwezo wa kuumba life, yaani creation and taking back life, everything God can do, the devil can do, hivyo kuna maono mengi, mambo mengi, miujiza mingi, inafanywa duniani watu wakiamini ni kazi ya Mungu, kumbe sio kazi ya Mungu bali ni kazi ya shetani, na kuna mpaka dini, watu wanaabudu wakijua wanamwabudu Mungu kumbe wanamwabudu shetani disguised as God!. Hivyo sio kila ndoto mtu unayoota ni maono kutoka kwa Mungu, na sio kila sauti unayoisikia from within ni lazima ni sauti ya Mungu, nyingine ni sauti yako tuu na nyingine ni sauti ya shetani!.

Mungu Yukoje, Yuko Wapi, Anaishi Wapi, Shetani Yukoje, Yuko Wapi na Anaishi Wapi?.
Katika mafundisho mengi ya dini hakuna popote tumefundishwa Mungu yukoje, wengine wakisema Mungu ni Mwanga, Light, kinazungumzwa tuu kiti cha enzi. Mungu anasekana yuko juu mawinguni, anaishi kwenye pepo, yaani peponi. Na baada ya shetani kuasi, alifukuzwa peponi akatupwa duniani.
Ile siku Mungu anamuumba binadamu, inasemekana alikuwa yeye Mungu, Neno, na Roho Mtakatifu, wakasemezana na tuumbe mtu kwa mfano wetu, hivyo sisi binadamu tumeumbwa kwa udongo kwa mfano wa Mungu. Mara baada ya Mungu kutuumba kwa kufinyanga udongo, alitupulizia ile pumzi ya uhai, sio wengi wanajua kuwa kule kuumbwa kwa mfano wa Mungu sio kwa maumbile bali kwa uhai. Ile pumzi ya uhai Mungu aliotupulizia, life force, ni ametumegea Umungu wake na kutuwekea sisi, hivyo ule uhai wa binadamu, ni Mungu ndani yetu, watu wanaodhani Mungu anaishi mbinguni, hawajui kuwa Mungu anaishi ndani yetu, omnipresence, kila kiumbe chenye uhai, kwa upande wa binadamu, ule uhai ni Mungu, hivyo ile sauti unayoisikia ndani yako ikikukataza usifanye jambo fulani, ni sauti ya Mungu ndani yako. God is Spirit, ni Roho. The same way Mungu ana exist ndani yetu kama Roho, shetani naye ana exist kama pepo chafu, akijitahiti kuingia ndani ya miili yetu ili kuchukua nafasi ya Mungu. Mambo yote mema na mazuri yanayofanyika duniani yanafanyika, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo, ni kazi ya Roho ya Mungu iliyopo ndani yetu na mambo yote mabaya yote na maovu yote yanayofanyika duniani kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo, ni kazi ya mwovu shetani!.
Ndani ya miili yetu, Mungu na shetani, wana co exist pamoja, ila binadamu akifanya jambo jema, shetani anakasirika, na binadamu akifanya jambo baya Mungu anajitenga naye.

Voices from Within Sio Utabiri, Sio Ubashiri, Ni Maono Tuu Ndio Ukweli Halisi Ila Sio Lazima Yatokee!.
Huu sio utabiri, sio ubashiri, na sio trend reading, ni maono tuu, mtu anasikia sauti unaambiwa kitu bila kuambiwa sababu, mfano unapotaka kusafiri moyo ukasita, kisha ukasikia kilichotokea, ndipo unagundua sababu. Wanawake wengi wanapokuwa approached na wanaume malaghai, hao wanawake they need love, wanaume malaghai they just need sex, sasa anapoku approach anakuja kwa hoja kwa kukwambia "I love you" na kwa sababu wewe mwanamke you need love, utafurahi. Wanawake wote wanapodanganywa "I love you", mara nyingi conscious zao huwa zinajulisha kuwa unadanganywa!. Mwanamke who needs love anapoambiwa "I love you", wewe kama binadamu, you can't tell for sure if "he real loves you or he just needs you for sex feast" mtu anaku approach for lust anakuambia I love you, ni ngumu ku distinguish real love na infatuation, love and lust, ndio maana wanawake wote wanakuwa approached, hata kama na wewe unampenda, don't rush to say yes, ili ujiridhishe kwanza kwa kujisikilizia voices from with if he real loves you!.

Unapotaka kufanya jambo, Ile sauti from within inayokuambia no, very soft and gentle voice, ndio sauti ya Mungu, na ile sauti kubwa inayukushawishi kwa kelele ikukumbia fanya tuu, kubali tuu, nenda tuu, ndio sauti ya shetani. Sio kila kitu unachosikia ni lazima kitokee, vingine havitokei lakini vikitokea ndipo unakumbuka.

Hata aliyepanga kuumua Tundu Lissu, kwa kuwaza tuu kumuua mtu ni wazo la kishetani, lakini Mungu aliingilia kati kupitia dhamira ilimkataza, kama Tundu Lissu tatizo lake ni uropokaji tuu, kuna sauti ilimwambia mwache tuu aendelee kuropoka, si ataropoka mchana tuu na usiku atalala. Hata wale watekelezaji wa mpango ule waliomiminia risasi 40!, 16 zikampata, nao pia dhamira iliwasuta, hivi kweli unawezaje kumuua binadamu mwenzio?, ila kama wauaji wale walipewa amri halali, wao hawana makosa yoyote kwasaba wao walikuwa wanatimiza wajibu wao, ndipo Mungu akaingilia kati, risasi zikamiminwa Mungu akamponya Lissu.

Kabla ya tukio lile, kwanza Lissu alisikia sauti, akawa makini, aka notice kuna gari linamfuatilia, badala ya ku do the right thing, kwa kuripoti kwa vyombo husika, yeye alifanya press conference na kujulisha media. Naamini nikifanya mahojiano na Lissu na dereva wake, nikiwauli kuhusu sauti, watakumbuka waliambiwa kila kitu lakini walipuuza hivyo yakatokea. Kwa vile there is no guarantee maono gani ni sauti ya Mungu, au la, the best thing ni ukisikia tuu sauti, usipuuze!.

Jee Maono ni Lazima Usikie Wewe, Vipi Akisikia Mwingine?.
Maono ni utaratibu wa Mungu aliyoko ndani yako kukuonya, Mungu anaweza kuongea na wewe kupitia fikra, kwa mawazo, kwa maneno au kwa matendo kupitia ishara fulani fulani, au hata kupitia kwa wengine, kama Mungu alivyonena kwa vinywa vya manabii. Mfano hai ni mimi mwenyewe.
haya chini ni mastori tuu unaweza kuruka.
Mimi nilianza malovee mapema tuu nikiwa sekondari, na hili japo sio zuri lakini sio vibaya kulisema ili kufundisha wengine. Mimi na dingi wangu tulikuwa kama marafiki, sio unajua tena Wasukuma, hivyo trips nyingi za dingi akienda na mimi, hivyo vi intro vya huyu ni anti wako, nilivipata vingi by then sina hili wa lile. Nilipokuwa kijana na mimi nikaanza kufolenisha, dingi akiona anatoa maxi!. Tabia mbaya za sisi wababa hurithisha tabia mbaya watoto wetu, hivyo sisi kama wazazi tuwe makini sana na mienendo yetu, baba ukiwa mhuni, mtoto atakuwa mhuni, mama ukiwa muachiaji, binti yako atakuwa muachiaji!.

Peak ni wakati ya jeshini JKT, wenyewe tukijisifia "kata funua". Baada ya hapo nikaingia chuo, TSJ, na foleni ndefu ili kuna mtoto, class mate, katoka familia bora kapenda kafa kaoza!, ile tumemaliza tuu chuo na ndoa juu. Wakati wa maandalizi ya harusi, Mzee Mayalla keshatangulia mbele ya haki (RIP), mama akaniita na kuniambia amesikia sauti ikimwambia usioe huyu mke sio!. Mtu umependwa kufa utasikia?. Kwa vile mather ni mlokole hili jambo akalifikisha kanisani wakafunga na kuomba ili kumuuliza Mungu, atoe sauti au ishara. Mama hakusikia kabisa, ila kuna mmoja wa hao wamama waliofunga na kuomba alisema yeye amesikia sauti kuwa nioe tuu. Hivyo mama akanikubalia kwa kusema japo yeye ameomba sana hakusikia, ila Mungu anaweza kuongea kupitia watu wengine. Nilioa, tena kwa harusi kubwa enzi hizo Mtangazaji maarufu, honey moon London, na kumalizia New York, nikasettle Washington DC, and that was the end, kilichofuatia ni history, ila I was warned sikusikia!. Ndoa nyingi zinazovunjika, wanandoa huwa wanasikia sauti kabla ikiwaambia dont, wanakaidi tuu na kinachofuata ni divorce!.

Ukiwa mwandishi ili kufanya kazi kwa haraka ni getting there first, hivyo usafiri wangu ulikuwa bike. Baada ya kuendesha bike for 15 years, big bikes, naenda nayo popote, Arusha, Tanga, Dodoma, kuna wakati Nane Nane ya kwanza ilianzia Morogoro, nikiwa TBC nilikuwa naenda Moro asubuhi na kurudi Dar jioni.
Siku moja the fateful day, Nane Nane ya 2008 nikapanga kwenda Dodoma na bike kama kawaida,yangu, by that time tayari nimenunua gari la PPR, ni gari yangu ya kutembelea Marcedes Benz E Class, wife ana gari Rav 4, hadi watoto wana magari!, lakini mimi na bike, bike na mimi!. Wife akaniambia roho yake imegoma, this time niende na gari, nilimgomea na kusema nimeride for 15 years bila tatizo, why not!, sikusikia, nikaendelea na safari!, kwani Dodoma nilifika!.
Hivyo tusidharau maono hata kama hukuyasikia wewe mwenyewe.
Hitimisho.
Hiki kinachofanywa na Bunge la Marekani kwa rais wao, jee kingeweza kufanywa na Bunge la Tanzania, suppose ni kweli rais Magufuli anakiuka Katiba?.
Hoja kama jee ni kweli rais Magufuli anakiuka katiba au laa, bado sio hoja kwasababu mamlaka peke yenye uwezo wa kutafsiri sheria kama kwa kuzuia mikutano ya siasa, rais Magufuli akiuka katiba ama laa ni Mahakama Kuu pekee, na so far hakuna mtu yoyote au chama chochote kilicho omba tafsiri ya kisheria ya uamuzi huo wa rais Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa kama unakiuka katiba au laa, lakini pia kwa vile Spika ajae kwa mujibu wa maono haya ni Dr. Tulia Akson, hata rais Magufuli akikiuka katiba, Bunge la Dr. Tulia, tena kwa kuzingatia litakuwa ni Bunge la chama kimoja CCM, litaweza kumwajibisha rais?.

Alhamisi Njema.
Paskali
 
Nb: Ukumbuke tu iwapo ikatokea Ndugai akakuita tena Dodoma, ujue utaenda ukiwa na pingu mikononi. Maana hatakuvumilia tena kama wakati ule! Yule mheshimiwa naye amekua kama mkuu wa kaya siku hizi, huwa hataki kabisa kuambiwa mawazo tofauti na yale anayo yawaza yeye.

All in all, Katiba yetu chakavu ya mwaka 1977, ndiyo inayomtia kiburi Rais wetu afanye apendavyo! Sijamshangaa aliposema Katiba siyo kipaumbele chake. Kwa hulka na aina ya misimamo na maamuzi yake, hawezi hata siku moja kuendana na Katiba inayomnyima au kumpunguzia mamlaka!
 
pasco mayala anasema eti ile ndoto ya lema ilikuwa ni ndoto ya shetani khaaaaa huyu nguli wa habari naye katekwa ama anaogopa kwenda dodoma akiwa na pingu mkononi, anaamua kuuma na kupuliza asionekane mbaya?
Hata ile sauti kuwa "Chadema hawajitambui" ulikuwa sio sauti ya Mungu Bali ya shetani. Tens yaweza kuwa ya shetani mkuu mwenyewe Lucifer.
Tumeyaona majibu ya mkutano mkuu na kuona kuwa ni chama kinachojitambua kuliko vyama vyote vilivyo sajiliwa kwa Mutungi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom