Voices from Within: JPM ni Rais msikivu na mwenye huruma, aliyekosea kuapa, atasamehewa, ataapishwa upya na kuendelea na Unaibu Waziri wake

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,507
113,629
Wanabodi,

Hili ni bandiko kuhusu kitu kinachoitwa "voices from within" ni kama "trends reading of some sort.
'Voices from Within" ni kuisikia sauti kutoka ndani yako!.

Sasa baada ya Naibu Waziri wa Madini kushindwa kuapa, na Rais Magufuli kumtumbua pale pale, au papo kwa papo kwa kudhania jamaa hajui kusoma, na akaagiza elimu yake ichunguzwe, kwa vile mpaka sasa yameisha pita masaa zaidi ya 24, bila press release ya Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu kutangaza rasmi utenguaji na replacement, then "the voices from within" is telling me, Rais Magufuli ameupata ukweli kuwa sio kuwa jamaa hajui kusoma, baada ya kuujua ukweli wa kilichotokea kuwa sio kuwa jamaa hajui kusoma, bali ni adrenalin panic attack, na huweza kumtokea mtu yoyote!, hata katika yaleee mambo yetu yale, kama ilivyo kauli ya "mkamia maji hayanywi", yaani unaweza kufika, mahali, jambo umelipania sana, ile kufika Mzee simama, simama na wewe, wapi!, unaishia hola!. Au unapiga mechi kali ili ufunge goli, funga na wewe.

Hivyo naamimi kabisa by now, Rais Magufuli, must have a change of heart, huruma imemuingia, na kwa mane aliyoyasema pale kumhusu mtu huyu, atakuwa ameamua kumsamehe, hivyo wewe kama mwana jf, be the first to know, jamaa atasamehewa, ataapishwa upya na kuendelea na UNaibu Waziri wake!.

Naandika hivi, kwa sababu hata huko nyuma, kuna vitu niliwahi kuviandika kumhusu JPM ni mtu wa namna gani, vile vitu vilikuja kutokea exactly kama nilivyoandika, sasa ili na wewe uweze kuelewa nazungumzia nini, au ulielewe vizuri bandiko hili, lazima kwanza ukalisome bandiko hili.

Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever had. Msikivu, ana upendo na huruma. Atabarikiwa sana. Tanzania itabarikiwa!
Kaangalie nilisema nini na kilitokea nini.

Kwa faida ya wale wavivu wa kufungua links, nawawekea kwa kifupi, nilisema nini kumhusu JPM
"Pamoja na madhaifu yake yote ya kibinaadamu na makosa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo rais Magufuli na serikali yake wametenda, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo, lakini kwa mazuri na mema ambayo Rais Magufuli anayatenda kwa taifa hili, hata yale mabaya na maovu yaliyostahili karma kali, hiyo karma inakuwa reversed kwa mema makubwa zaidi kuliko ule uovu. Hivyo, Nasema kiukweli kabisa na kwa dhati ya moyo wangu kuwa rais Magufuli atabarikiwa kwa mema yake anayolitendea taifa hili, na hata kama kuna uovu, maana yeye sio malaika, uovu huo unaweza kufunikwa na mema yakizidi huo uovu!.

Trends readings zangu zinanielekeza kuwa rais Magufuli, so far, so good, might end up being one the best presidents this country has ever had, save for Baba wa Taifa kutupatia uhuru!. Rais Magufuli ni msikivu sana, ana upendo sana wa kweli, upendo wa dhati, upendo wa ajabu. Ni mtu mwema, mwenye huruma sana, huruma ya kweli na huruma ya ajabu, japo sio kwa wote!, hivyo akiendelea hivi, atabarikiwa sana na Mungu!, Tanzania itabarikiwa!" Mwisho wa kunukuu.

Kujua kule alitenda wema gani, ni lazima utembelee bandiko hilo.

Baada ya Naibu Waziri huyo kushindwa kuapa, rais Magufuli alisema yafuatayo kumhusu mteule huyo.


Ukimsikiliza kwa makini rais Magufuli hajamtumbua amesema

Kwa vile uteuzi unafanywa kwa maandishi kwanza na sio kwa kauli, na utumbuzi pia lazima ufanywe kwa maandishi na sio kwa kauli, hivyo kama kweli rais Magufuli alimtumbua papo kwa papo, taarifa rasmi toka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ingeeleza.

Wakati rais Magufuli akilizungumzia hili, kuna kitu very interesting rais Magufuli amekisema, ambacho ndicho kilichotokea behind the closed doors za Ikulu. Kwa vile kwa mujibu wa Katiba, inaelekeza wakati wa kuteua baraza la mawaziri, rais arashauriana na Makamo wa rais na Waziri Mkuu. Hivyo kilichotokea behind the closed doors, ni kuwa wakati wakichekecha majina, JPM akampa fursa PM na yeye kuleta watu wake, Hivyo PM akaangalia katika wabunge wote wa Lindi nzima, ukimuondoa yeye PM, huyo jamaa ndie the second mwenye a very strong CV, hivyo ni PM ndie kamleta!, kwa sisi wenye jicho la tatu, JPM alipomzungumzia alikuwa aki point accusing fingers kwa PM kuwa huyu ni wa Lindi, mko wawili tuu na PM, hivyo ni kama anamwambia PM, usinilaumu kama hakutakuwa na mwana Lindi mwingine kuweza kuchukua hiyo nafasi.

Hivyo baada ya huyo jamaa kushindwa kuapa, mambo matatu haya yamefanyika jana hiyo hiyo, usiku, ilikuwa ni hakuna kulala
  1. Wale "jamaa" wamemfanyia uchunguzi vyeti vyake ni vya kweli, wakakuta ni bonafide genuine.
  2. Jamaa akafanyiwa uchunguzi ni kweli hajui kusoma, ikakutikana jamaa anajua kusoma vizuri tuu, pale alipigwa na adrenalin panic attack.
  3. PM atakuwa amemuombea msamaha na kumbembelezea, ndio maana leo asubuhi hakuna taarifa yoyote rasmi ya rais kutengua uteuzi huo au kufanya replacement.
Hivyo wewe kama mwana JF, enjoy the JF Advantage, Be the first to know, kuwa Aliyeshindwa kuapa, atasamehewa, ataapishwa upya na kuendelea na kazi yake, na huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Rais Magufuli ni msikivu sana, ana upendo sana wa kweli, upendo wa dhati, upendo wa ajabu. Ni mtu mwema, mwenye huruma sana, huruma ya kweli na huruma ya ajabu, japo sio kwa wote!, hivyo akiendelea hivi, atabarikiwa sana na Mungu!, Tanzania itabarikiwa!.

Angalizo Muhimu Kuhusu, "The Voices From Within" na "Trends Reading"
Wanabodi, naomba kutoa angalizo hili muhimu kuhusu hizi "The Voices from Within" na "Trends Readings", sio lazima zitokee kwa sababu kuu mbili.

  1. Kwa sababu hizi ni sauti, sio kila sauti mtu unayoisikia kutokea ndani yako ni sauti kutoka kwake "YEYE", sauti nyingine unaweza kuisikia ukidhani ni kutoka kwake "YEYE", kumbe sio kutoka kwa "YEYE" bali ni kutoka kwa "yeye". Hivyo unaweza kuisikia sauti na isitokee!.
  2. Inaweza kuwa ni sauti kutoka kwa "YEYE", lakini watekelezaji wakawa wanamtegemea sana "yeye", hivyo "YEYE" akaifanya mioyo yao kuwa migumu, na wakashupaza tuu shingo zao, kama enzi za Farao na Waisraeli, ili kuwaonyesha utukufu wake "YEYE", hivyo haitatokea, na msubirie... utukufu!.
NB. Wakati ukisoma bandiko hili, pia zingatia kitu kinachoitwa Presidential Appointment Powers, yaani rais yuko huru kumteua mtu yoyote, kwa sababu zozote au bila sababu zozote, na yuko huru kumtegengua kwa sababu zozote au bila sababu, na maamuzi ya rais, hayahojiwi na mamlaka yoyote. Hivyo hata rais akiamua kumtengua kwa kushindwa kuapa, bado rais atakuwa yuko right, ila huku kutakuwa sio kumtendea haki mtenguliwa huyo

Mungu Mbariki Rais Wetu Dr John Pombe Joseph Magufuli andelee kuwa mtu wa huruma, upendo na kusamehe kwa kuisikia sauti yake "YEYE" na sio "yeye"!.
Mungu Ibariki Tanzania,

Paskali
 
Naona umeanza safari ya kusifu mapeeema kama 2015-2020.

Safari hii mzee kashapata somo kubwa sana, he doesnt buy cheap praises anymore.

Na juzi kawachana mawaziri kabisa kwamba sitaki mfanye kazi huku kamera zikiwa nyuma, kama unafanya kazi itaonekana tuu sio lazima utupostie.

Nyie CCM mnafuata mkumbo ndio maana haishangazi kina Silinde wanalamba teuzi na nyie mmetoa macho tuu sababu ya akili zenu mgando kama hii post yako.
 
Hapa nipo kwaajili ya kusoma tu comments ili nione jinsi wachangiaji wanavyo mshukia Paskali....😂😂😂
Ila bro Paskali nawewe umezidi, daili unamsemea JPM wakati alisha sema kwama wanayo rezevu ya kutosha na pia hata yeye "hata yeye hana raha na mke wake"
 
Back
Top Bottom