Vodacom washusha bei kuongea sasa sh 1 kwa sekunde

Ha ha ha !!! Customers wengi walishasepa kiaina na kuingilia tiGo!!! Afadhali wameshtuka mapema!!

Sure.
Nilikuwa na jamaa zangu wasiokubali mabadiliko, kwa sasa nashangaa wametupa laini zao za Voda, wameingia tigo.
 
Wala hakuna hasara watakaopata kwani baada ya uwekezaji gharama za kuendesha sio za kutisha sana. Katika mataifa mengine, simu kutoka mtandao mmoja ni bure kabisa (zero), kinachokuwepo ni garama ya kukuunganisha tu. Say unalipa kama Tsh 100 kuunganishwa halafu unaongea bure, wakati kwenda kwenye mitandao mingine unalipa gharama ya kuunganisha na kama Tsh 80 kwa dakika. Sasa ukilinganisha mataifa yanayoweza kuchaji viwango vya chini hivyo kuwa garama ya kuwalipa wafanyakazi wao ni kubwa kuliko Tz, kwanini Voda wapate hasara?
 
FCC kazi yao ni kusimamia kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki na si kuzuia ushindani.

Hiyo ni kweli. Lakini kama haya makampuni makubwa 'yataamua' kushusha bei to the minimum kwa ajili ya kuzuia new entrants into the telecom market, nadhani in the end itazuia ushindani wa haki na hivyo ultimately consumers ndio watakoathirika.

Wanaweza kupunguza bei sasa kwa sababu tu kuna tishio la new entrants, lakini tishio hilo likiondoka (kwa vikampuni vidogo kufa au kushindwa kuingia kwenye biashara), watarudisha bei zao juu.
 
SMU waonekana darasa la biashara walifahamu. Bila shaka ulikuwa unaongelea madhara ya dumping price. Hiyo ni bei inayolenga kunyonga washindani wako kibiashara; na wala si kumsaidia mteja. Makampuni makubwa yanaogopwa kwa sababu hiyo. Hivyo FCC wana kazi kufanya hapo kulinda vikampuni vidogo, na vyenyewe viweze kuleta ushindani..
 
Mi Voda nilisha sahau hawa wezi sana wanawanyonya sana wabishi wasio elimika.

cha ajabu ni kwamba wana wateja wengi zaid mbali na kuwa na gharama kubwa.kaka mtu halazimishwi kuwa mteja wa voda.

always customers are out there inategema unatumia njia gani kuwavuta kuja kwako.!
 
Hapo safi, Tigo express yourself
Kama sio juhudi zako tigo... voda wangeshusha lini .. oo kama sio ....
 
Vodacom wizi mtupu jaribu kupiga voda kwenda voda kama hutaumia na rate zao za mafisadi 34seconds =190Tsh how comes mnasema wameshusha bei????? au wewe ni promota wa vadacom
 
Wakuu,

Nina uhakiak Zain wanahaha sasa hivi!!!
This is a blow to them.
Watumiaji tupige miruzi tu, tuendelee na ka-tiGo ketu mpaka washuke.

Safi sana wazee wa-kujiexpress.....
 
Na mm niliacha kutumia Voda toka 2006, Voda wizu mtupu
Mimi niliingia kwenye mtandao wa Vodacom toka 2001 hadi leo niko Vodacom, naona hapa wanatufanya tuzidi kubaki Voda.

Lakini hawa jamaa wa Vodacom sijui kama hiyo huduma itadumu kwa muda mrefu. Labda ni njia ya kuwafanya waliokimbia mtandao huu kurudi.

Ok, ngoja tusikilizie.
 
jamaa ni mafisadi hadi wa maneno kwanza hawana wateja million saba wanasema wanawateja million saba kwa ajili ya publicity tuu lkn in deap ni uzushi mtupu.
 
Vodacom yazindua 'HABARI NDIYO HIYO'
VODA1
 
Hii nayo ni nzuri lakini wanapaswa kucontrol congestion make mara nyingi jamaa wanalalamika kuwa wakipiga cm "connection error". All the same ni msaada kwa walio wengi!
 
Wabongo bwana! Eti wametuibia muda mrefu. Mlisikia wamekuja kutoa msaada wa mawasiliano? Na mjue tu kuwa hakuna hasara hapo. Ni lugha ya biashara tu. Voda idumu.
 
%5Cvodacom.jpg

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya simu za mikononi za Vodacom nchini, Ephraim Mafuru akionyesha bango kuashiria gharama mpya za kupiga simu za kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Mwananch icommunication Ltd jijini Dar es Salaam jana Kulia ni Mkurugezi wa Uhusiano wa Vodacom nchini Mwamvita Makamba na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL. Sam Shollei.

Boniface Meena

WATEJA wa huduma za simu zinazotolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania wameongezewa unafuu baada ya kampuni hiyo kupunguza gharama za kupiga simu na sasa kuwa Sh1 kwa sekunde.

Huduma hiyo mpya ijulikanayo kwa jina la 'Habari Ndiyo Hiyo' itakuwa endelevu na isiyo na kipindi maalum na itawawezesha wateja zaidi ya milioni 7 wa Vodacom kupiga simu kwa gharama nafuu, Vodacom ilisema jana.


Kabla ya Vodacom kuamua kutoa huduma hiyo, mteja alikuwa akipiga simu kwa gharama ya Sh4 kwa sekunde, lakini huduma mpya itafanya gharama upigaji simu ipungue kwa asilimia 300.


Mkuu wa kitengo cha mahusiano na Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba alisema jana kuwa huduma hiyo si promosheni kwa kuwa nia yake ni kuongeza mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano nchini na kumuongezea mteja unafuu katika mawasiliano.


“Wateja wa Vodacom watapiga simu kwa gharama nafuu... kwa mtazamo wa wengi ni jambo lisilowezekana kwa kuwa sokoni tumekuwa tukionekana kutoa huduma kwa gharama za juu," alisema Makamba.


“Lakini Watanzania wengi hasa walio vijijini hawawezi kutumia simu kutokana na gharama kuwa juu na hivyo kutokana na maombi yaliyotolewa bungeni, tumeona ni vyema tufanye hivi ili kurahisisha mawasiliano.


"Tumeamua kuchukua uamuzi huu wa kutoa huduma kwa gharama za chini na pia tutaendeleza huduma nyingine kwa lengo la kurahisisha mawasiliano."


Alisema huduma hiyo ni kwa kupiga simu tu, lakini huduma nyingine za Vodacom zitabaki kama zilivyo na kueleza kuwa itakuwa ni hasara, lakini ni muhimu katika kuboresha mawasiliano nchini.


Alisema kiwango hicho cha malipo kwa wateja wa Vodacom ni mwendelezo wa utoaji wa huduma na promosheni zinazoambatana na zawadi mbalimbali ambazo huwafanya watumiaji kuwasiliana kwa urahisi.


Makamba alisema licha ya kutambulisha huduma hiyo, kampuni hiyo itaendelea kutoa promosheni zake nyingine kama Cheka Time na Vodajamaa.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18709
 
Mmefanya vema sana Voda
mmetusaidia sana wateja wenu kupunguza makali ya kununua Vocha
Big up
 
Gharama hurudi kama awali ifikapo saa 11 jionio hadi saa 3 usiku. Sasa kama si promo ni nini?
 
Back
Top Bottom