Vodacom washusha bei kuongea sasa sh 1 kwa sekunde | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom washusha bei kuongea sasa sh 1 kwa sekunde

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lukwangule, Mar 23, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vodacom Tanzania katika kushawishi matumizi zaidi ya simu za mkononi imeshusha bei ya upigaji simu ambapo sasa wateja wa Voda kwa Voda watapiga simu shilingi moja kwa sekunde.
  Kwa hesabu za haraka haraka punguzo hilo ni zaidi ya asilimia 200 na wenyewe wanasema litatengeneza hasara lakini watafurahi kama watanzania wengi wataingia katika mtandao.
  Akitangaza biashara hiyo mpya ambayo haihitaji kujisaili inayotarajia kuanza leo saa sita mchana, katika chumba cha habari cha magazeti ya serikali ya Daily News na HabariLeo,Ephraim mafuru ambaye ni Mkurugenzi wa Matangazo alisema ni lengo kufungua zaidi matumizi ya simu ambayo ni muhimu kwa maendeleo hasa vijijini.
  Mafuru ambaye aliambatana katika safari ya kuzindua huduma hiyo na Mkurugenzi wa mahusiano ya jamii mwamvita makamba alisema hasara hiyo itafidiwa na hudjma nyingine za Vodacom ambazo zote zimelenga kuwa karibu na watanzania.
  Huduma nyingine ni kama za fedha, intaneti na pia za ATM.
  Ikiwa na wateja milioni saba na zaidi katika soko lenye jumla ya wateja milioni 13,Vodacom wanasema kwamba wanatoa nafasi zaidi kwa watu kuanza kutumia simu za mkononi kwa maendeleo yao.
  Huduma hiyo itawezesha wateja zaidi ya milioni saba wa kampuni hiyo kunufaika na huduma hiyo ambayo itakuwa endelevu .
  Mwamvita naye alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo kutaongeza mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano nchini.
  Aliongeza kuwa kampuni hiyo imewekeza kwa miaka 10 nchini, hivyo kwa kipindi hiki ambacho ni cha Mapinduzi ni wakati muafaka kwa vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali, wafanyabiashara wadogo na wa kati, wakulima, wanafunzi, wafanyakazi kuendelea kutumia mtandao huo na kufaidika na huduma zake.
  Licha ya kuanza huduma hiyo kampuni hiyo itaendelea kutoa promosheni zake za “Cheka Time na Voda Jamaa”.
  Kuhusu huduma za mkongo wa mawasiliano, alisema
   
 2. L

  Lukwangule Senior Member

  #2

 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280

  hivi kweli rostam anawapenda sana wa tz kiasi cha kukubali hasara ili wabongo wafaidi mawasiliano ya bei nafuu??
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Yesu ni Bwana!..HALELUYA!
  Bwana ameona unyonge wa mjakazi wake!
  Asante TIGO kwa kuonyesha njia ya ukombozi!...
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  duuu 200%.....balaaa ila itasaidiaa kuleta maendeleeooo.....hasa vijijiniii
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi Voda nilisha sahau hawa wezi sana wanawanyonya sana wabishi wasio elimika.
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ndo fanida ya soko huria kama ni kweli, Vodacom walikuwa hawana ujanja zaidi ya ku lower tarrif zao. Asilimia kubwa ya watumiaji wa simu mijini walishaikimbia Voda ukiacha corporate customers.

  Thanks to tiGO and Zantel kwa ku lead market kwa lower tarrifs!!

  Na bado..........naamini tiGO watakuja na tarrif ya centi 30 kwa sekunde, ndopo hapo makaburu wa Vodacom na Zain watakapo restructure kampuni zao na kuwa force kuwa price competitive kama wenzao wa tiGO na Zantel!!
   
 8. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu akukumbuke we nani??? Vodacom wamelazimika ku lower tarrif kutokana na mapato yao kuanza kudorora!

  Mpaka mafisadi wanatumia tiGo na Zantel siku hizi!!

  Mkuu ila RA alishauza share zake pale Vodacom......baada ya wadau kuanza 'majungu'!!
   
 9. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280

  Kimsingi Voda walikuwa hawana ujanja wa kuendelea kung'ang'ania kutoza wateja wao gharama za juu ilhali wateja wanaukimbia mtandao wao. Wateja sasa wanajaa Tigo na Zantel. Zamani Voda na Zain ndio waliokuwa na coverage kubwa mikoani, lakini kwa sasa hata makampuni mengine nayo yamejitanua sana mpaka vijijini. Ndo hapa kichwa kilipowauma watu wa Voda.
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Watupe basi na kale Ka- Tuzo millionea .................Mbona hakatulengi sisi.................
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa mwendo huu kuna baadhi ya kampuni zitakufa. Fair competition commission inabidi wakae chonjo!
   
 12. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Waache kujishaua hapa. Eti watapata hasara!

  Does it mean Tigo were running at loss with their 1 sh per sec service that started long tym ago?

  To hell with their profit or whatever they say.

  Kampuni za simu wanatunyonya sana. Si tu watumiaji hata workers wana-deserve to be payed better if u look at what they (companies) earn.

  Shame on them makaburu!
   
 13. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ni kweli.....Voda na Zain zinaweza kufa kwa Tanzania kwa sababu kwa zaidi ya miaka 10 wamekuwa wakipata faida kwa kucharge bei kubwa huduma zao na sio kujifunza ku manage running costs.

  Muda mfupi ujao tutaanza kusikia rightsizing (kupunguza wafanyakazi) inafanyika katika makampuni haya. Ndugu zetu mlio huko mkae mkao wa maumivu anytime kuanzia sasa! Kupunguza bei kwa 200% sio mchezo..........

  Ingawa wameweka mkakati wa kuwakamua watanzania kwenye huduma zao zingine ili kufidia hasara itakayotokea. Mimi hili haliniumizi sana kwa sababu walalahoi wengi hawatumii hizi additional product zao, kazi kwa middle class and above especially corporate customers!!
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hizi kampuni kubwa tayari kwa sehemu kubwa wamesha invest vya kutosha. Hizi ndogo/mpya the likes of sasatel, hits etc ni vigumu sana kustawi kwenye environment yenye vita ya bei (price wars) au kama baadhi ya hizi kampuni kubwa/kongwe zitaamua/zimeamua kushirikiana (illegally) kupanga bei.
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha Kibweka hizo huwa zinarudi kwao
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wabetuibia muda mrefu hawa!
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280

  FCC kazi yao ni kusimamia kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki na si kuzuia ushindani. Shida inakuwa, iwapo makampuni ya simu yatakaa na kupanga bei za huduma zao ili kuwaumiza wateja, hapo ndipo FCC wanatakiwa kuingilia kati na kuwaadhibu. Upangaji wa bei (price fixing) kwa washindani ili kuumiza walaji ni makosa.  Umegusa pabaya.
  Voda na zain hawajui kutumia kidogo walichonacho kwa umakini. Njia mojawapo ya kupunguza matumizi ni kupunguza idadi ya magari yao, wana magari mengi mno pasipo sababu za msingi. Gharama za kuyahudumia magari haya hulipwa na wateja kwa kuwakamua zaidi, hivyo kuwaongezea mzigo.  Kwa jinsi kampuni kubwa kubwa za simu zilivyojiimarisha kimiundombinu na kibiashara, usimamaji wa uhakika kwa Sasatel na kampuni nyingine changa ni kazi sana.
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha !!! Customers wengi walishasepa kiaina na kuingilia tiGo!!! Afadhali wameshtuka mapema!!
   
 19. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  SAnte tiGo kwa msimamo wenu maana wamejifunza kwenu
  kwa mtini jifunzeni
  alisema yesu
   
 20. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ushauri wangu wa bure jamani

  wale washikaji zetu ambao wameajiriwa na hawa makaburu waanze kurusha CV haraka iwezekanavyo, kuweni karibu na magazeti hasa ze gadian la ijumaa pamoja na mitandao ya ajira manake kinachofwata hapo ni dizasta....yani hao wawekezaji hawajaja kuuza sura bongo they are here to make chapaa...

  huo ndo ushauri wangu wa bure jamani,

  wenu katika bwana

  zionTZ
   
Loading...