Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,052
- 12,925
Waafrika alieturoga alituweza sana.
Mwaka jana Vodacom ikateua raia mwanamama mmoja kutoka Kenya kuja kua mkurugenzi wake, maneno yakawa maneno kua kwani tumekosa mtanzania wa kushika hizo nafasi na mambo kede kede, serikali ikamnyima kibali cha kazi. Dada wa watu akaendelea na maisha yake huko kwao Kenya.
Sasa Vodacom wameteua mwarabu kutoka Misri kua mkurugenzi wake, zile kelele za mwaka jana hazisikiki tena, maana yake hatutaki waafrika wenzetu ila tunataka watu wenye ngozi nyeupe. Kwanza tunaweza kumnyima mkenya kibali cha kufanya kazi Tanzania ila tukampa mwarabu wa Misri, sijui akili za wapi hizi.
Kwa hiyo ikifika kwa ngozi nyeupe hadithi za wazawa zinakufa, ila ikiwa ni mweusi mwenzetu hadithi za wazawa wapewe fursa ndio zinaibuka.
Binafsi hua sikubaliani na hoja ya uzawa, kwenye ulimwengu ulioendelea watu wenye uwezo binafsi wanataftwa kutoka kila mahali wakafanye mabadiliko na kuongoza taasisi za nchi nyingine. Uingereza ilimkodi Gavana wa benki ya Canada ili awe Gavana wao awasaidie kurekebisha uchumi, mkuu wa Google ni mhindi na mifano iko mingi.
Hoja yangu ni kwamba, kwa nini mkenya tulimkatalia kwa hoja ya uzawa alafu tumekubali mwarabu wa Misri?