Vodacom Tanzania MD, Hisham Hendi resigns

View attachment 1881283

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na Novemba Mosi, 2021 itakuwa siku yake ya mwisho baada ya kuitumikia kampuni hiyo yenye wateja katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika taarifa yake Vodacom imeeleza kuwa Bodi ya wakurugenzi iko katika mchakato wa kumpata mrithi wa Hendi, ambaye ameitumikia kampuni hiyo kwa miaka mitano, na pindi atakapopatikana na kuidhinishwa atatangazwa.

“Katika miaka mitano ya Hendi, Vodacom imeendelea kuwa kuongoza katika soko katika utekelezaji wa mikakati ya kidijitali ambayo imesaidia nchi kuwa na mifumo jumuishi ya kifedha kupitia ubunifu wa huduma za kifedha kwa njia ya simu,” amesema Jaji Thomas Mihayo ambaye ni Mwenyekiti wa bodi.

Jaji Mihayo aliongeza kuwa Hendi ambaye anakwenda kuwa mkuu wa biashara wa Vodafone nchini Hispania, amekuwa ni msukumaji mkuu katika kufanikisha uwekezaji wa kuwafikia mamilioni ya Watanzania ambao awali hawakufikiwa na huduma za simu (hawajaunganishwa).

Akizungumzia kuondoka kwake Hendi amesema anafurahi fursa inayomsubiri Hispania lakini anatambua isingewezekana kama si fursa aliyoipata Tanzania katika kipindi cha miaka mitano, miwili na nusu akihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji.

“Nimefanya kazi na timu nzuri na ninaacha wazawa ambao ni viongozi waandamizi wanaofanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Ninafurahi kuhudumu katika taifa hili kubwa. Uzoefu wangu hapa nchini ndiyo imefanikisha hatua hii, Kwa kweli najivunia. Naondoka Tanzania kama balozi wa nchi,” amesema Hendi.

Miongoni mwa mafanikio aliyoyapata Hendi katika kipindi chake ni kampuni hiyo kutajwa miongoni mwa kampuni 100 bora zaidi barani Afrika
kulingana na mtaji wa soko mnamo 2020, Kufanikisha kuorodheshwa kwa kampuni hiyo katika soko la hisa la Dar es Salaam.


Habari imechacha hii. Lete mpya
 
Baada ya kampuni kuuzwa wameamua watimke wakaanzishe hiyo yao huko southafrika sio?
 
Back
Top Bottom