M-Pawa wanatoza riba kubwa na wanasumbua kwa SMS zao

Next in Line

Member
May 16, 2023
31
33
Hawa M-pawa wanakushawishi ukope. Kabla hawajakutumia hela uliyomba kukopa, wanakata riba yao kabisa. Kwa hiyo, kama ulifikia kiwango cha kukopeshwa 100,000/- kwa mfano, utaishia kupata kwenye 80,000/- ikiwa ni kwamba wamechukua 20,000/- upfront kwa mkopo wa siku 30.

Kiwango cha riba hiki ni kikubwa sana. Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na kwamba mkataba wa mkopo ni siku 30, baada ya siku 4 au 5 tangu ukope unaanza kupokea SMS za kukukumbusha kulipa mkopo, na wakati mwingine hizi sms zinakuja saa tisa usiku.

Swali:
1. Mkataba wa mkopo ni kwa siku 30 na riba umekwisha chukua, si mtulie mpaka hizo siku 30 zifike?

2. Je, taasisi husika na mambo ya Microfinance institutions wameridhia hii riba kubwa ya aina hii?
 
Back
Top Bottom