Vodacom Tanzania: Kwanini mnataka kunisitishia huduma ya kukopa M-PAWA halafu tena mnaniuliza kama ninahitaji mkopo?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB. Leo ngoja tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu Vodacom Tanzania;

Kwanini mnataka kunisitishia huduma ya kukopa M-PAWA alafu tena mnaniuliza kama ninahitaji mkopo?


Hii message iliingia kwenye simu yangu nikiwa ninakunywa chai. Hauwezi kuamini nilicheka mpaka nikataka kuangusha kikombe cha chai chini.

MFANO KIDOGO.
==========
Just imagine Aisha alikopa pesa kutoka kwa Abdallah kiasi cha 200,000 na kuahidi kulipa pesa hiyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Baada ya mwezi mmoja kufika, Aisha alifanikiwa kulipa kiasi cha 90,000 tu na kubakiza deni la 110,000 kwa maana alifikwa na changamoto kadhaa zilizopelekea yeye kushindwa kumaliza deni lake.

Baada ya miezi mitatu baade Abdallah akaamua kwenda kutoa taarifa Police kwamba Aisha amegoma kulipa sehemu ya deni iliyosalia. Baada ya Aisha, Abdallah na afisa wa Police kukaa meza moja ya mazungumzo wakakubaliana kwamba Aisha ajitahidi alipe walau kiasi cha 5,000 kila week ili aweze kumaliza deni lile kidogo kidogo na endapo atashindwa kufanya vile basi hatua kali za kisheria zitafuata.

Sasa punde baada ya mazungumzo yale kuisha na kila mmoja kurejea nyumbani, Aisha anapokea tena ujumbe wa SMS kutoka kwa Abdallah na kumuuliza kama anahitaji tena kukopa pesa. Wewe unafikiri Aisha na yule askari Police (kama akipewa taarifa hii) watamfikiriaje huyu Abdallah? Is he Okay upstairs?

Pia Soma
=====
Kiingereza kibovu cha Staff wa Vodacom. M-Pawa confirmation message

Hatimaye Vodacom Tanzania wametekeleza "constructive idea" yangu niliyoandika humu JF. They were, at least, supposed to acknowledge my intellect
Nilikopa tuela twa mboga basi ikawa nongwa. Niliandikiwa ujumbe wa kunitishia kupelekwa polisi kwa kosa la wizi wa kimtandao. Pamoja na kuomba muda ili nimalizie deni, barua za vitisho ziliendelea kuletwa kwangu. Nilimaliza deni hilo na sasa kila baada ya siku moja naletewa ujumbe ukiniomba nichukue mkopo toka M-Pawa. Niliapa kwa MIFUPA ya babu zangu, "kamwe sitakopa tena tuela twa mboga toka kwa hawa jamaa "mashailoki".
 
Hee barua tena,,inakuja vip hiyo barua?
Nilikopa tuela twa mboga basi ikawa nongwa. Niliandikiwa ujumbe wa kunitishia kupelekwa polisi kwa kosa la wizi wa kimtandao. Pamoja na kuomba muda ili nimalizie deni, barua za vitisho ziliendelea kuletwa kwangu. Nilimaliza deni hilo na sasa kila baada ya siku moja naletewa ujumbe ukiniomba nichukue mkopo toka M-Pawa. Niliapa kwa MIFUPA ya babu zangu, "kamwe sitakopa tena tuela twa mboga toka kwa hawa jamaa "mashailoki".
 
Majizi hao, siku hizi ukikopa elf 20 wanakata 3,500 hapo hapo na unarudisha ndani ya mwezi. TCRA wapo tu wanaangalia, wale wanaoweza ku-calculate riba tunaomba mfanye mahesabu hapa.
 
Dawa ya deni ni kulipa...
Nimewalipa pesa yao yote jana.

Sasa vp kuhusu integrity pamoja na umakini wao katika kazi? Kama computer systems zinashindwa kutofautisha mteja aliye mdaiwa na yule asiye, kwanini tusiamini kwamba ipo siku watatuongezea madeni yetu?
 
Back
Top Bottom