Vodacom mnatuumiza wateja wenu

Vodacom mnatuumiza wateja wenu

Raia Mtata

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2017
Posts
326
Reaction score
616
Habarini waungwana

Kwanza napenda kusema mimi ni mteja wa kampuni ya Vodacom Tanzania kwa takribani miaka 18, ni kati ya wale wateja wa mwanzo tulioanza kuitumia vodacom tanzania.

Kwa masikitiko napenda kusema nimeacha kutumia huduma za vodacom kwakuwa haziridhishi, vifurushi ghali na ukiweka vinatembea kama upepo.

Jambo lililofanya niandike huu uzi ni kitendo ambacho vodacom wamekianzisha, wanakupa mkopo wa salio huku ukiwa hujaomba, yani sasa hali imekuwa ngumu hadi tunalazimishwa kukopa salio kwa riba? Kitendo hiki kimenikera kwa kuwa vodacom wana huduma so Poor.

Yani bora hata wangekuwa na huduma za kuridhisha tungeweza kupotezea lakini wana huduma so poor halafu wanatulazimisha kuchukua mikopo kwa riba? mjirekebishe watanzania wanategemea vitu vikubwa kutoka kwenu kututendea mambo haya ni kama usaliti.
 
Na ukipiga huduma wa wateja wale wadada wanaonekana wengi hawana experience au wengi wao hawajui kazi zao, mtu unampigia simu anapokea anakwambia wewe huna mkopo, wakati yeye yupo kwenye system na anaona, nikampigia mwengine hapo hapo customer care huyu anajibu kirahisi kabisa eti wewe umekopa mwenyewe nikamwambia ningekuwa nimekopa ningepiga simu hapa ofisini kwenu? They are so Poor
 
Mkuu kama simu yako ina access na watu wengi kama watoto na mke, kuna uwezekano mkubwa wamekopa bila wewe kujua. Jaribu kucheki hilo.
 
Nakubaliana na wewe mkuu ili miradi iende lazima tulazimishwe tu. Unajua siku hizi nimeanza kulipia AZAM, sasa STARTIMES kila siku wananipigia simu eti umesahau kulipia kifurushi cha startimes basi nawaambia sijasahau nimehamia AZAM, wakanipigia tena na tena, mwisho nikaacha kupokea simu yao. Hali kweli imekuwa ngumu mkuu
We unadhan sgr na nyerere h.e.p tutamalozaje mkuu hapa tunawalazmisha tuu

Chagua Tena ccm kwa maisha mabovu mbeleni
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia mbili, lakini wakati hilo tukio limetokea mie ndio nilikuwa na simu na siku nzima simu niliyokuwa nayo mie mwenyewe kwanza watoto wangu wadogo sana mambo haya hawayajui. Wamenichomekea tu mkuu
Mkuu kama simu yako ina access na watu wengi kama watoto na mke, kuna uwezekano mkubwa wamekopa bila wewe kujua. Jaribu kucheki hilo.
 
Mimi naomba msaada jinssi ya kufuta namba kwenye menu ya MPESA unapotuma pesa KIPENGELE CHA CHAGUA KWENYE ORODHA. Kwnye orodha kuna namba za simu sizitambui, nilienda vodashop wakasema hawawezi kuziondoa, nikapiga 100 nao wakasema hawawezi kuzifuta.
 
Mbona contradiction mzee! Mara umeacha kutumia mara unakopeshwa bila kuomba mkopo, mitandao bongo kibao akikuzingua huyu haimia kwa yule, mbona kwenye mademu mnahama halafu kwenye mitandao mnapata tabu?
 
Mkuu,
Nafikiri watakuwa wamezifuta hizo namba baada ya kupeleka mapendekezo yako,maana nimecheki kwenye laini yangu inaniandikia:
There is no beneficiary exist.
Masna hata mm nilikuwa na namba nyingi tu kwenye hiyo orodha ya M-pesa.
 
Mkuu nimekuwa mteja miaka mingi ila nahama, nimeweka uzi huu kwa faida ya wengine na unajua uovu haitakiwi uache uendelee tuwaseme ili wajue kuwa tumeona wizi wao
Mbona contradiction mzee! Mara umeacha kutumia mara unakopeshwa bila kuomba mkopo, mitandao bongo kibao akikuzingua huyu haimia kwa yule, mbona kwenye mademu mnahama halafu kwenye mitandao mnapata tabu?
 
Mimi zipo namba 6 moja tu ndiyo naitambua.
Mkuu,
Nafikiri watakuwa wamezifuta hizo namba baada ya kupeleka mapendekezo yako,maana nimecheki kwenye laini yangu inaniandikia:
There is no beneficiary exist.
Masna hata mm nilikuwa na namba nyingi tu kwenye hiyo orodha ya M-pesa.
 
Wezi wa vifurushi hakuna mifano, GB kufungua what's app masaa 2 imeisha hapo hauja download hata video moja nimeichoka voda, sahizi naifanya kama simu ya mezani labda habari za M-pesa si kwa wizi huu, mpaka niliwafuata nakuwauliza embu angalieni kitu gani natumia hakuna, eti labda kuna mtu alitumia hivi inaingia akilini kweli? Mie naishi na panya wakuiba MB daa, kutumia internet ya voda hapana si kwamaumivu haya, japo nimekuwa nayo miaka mingi kweli.
 
Hizo namba huwa zinajisevu automatic ukituma pesa lazima baada ya kipindi fulani zinapotea.

Back
Top Bottom