BRUCE LEE
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 2,096
- 1,332
Habari zenu wanaJamvi natumia nafasi hii kuwataarifu kuwa kwa muda mrefu nimekuwa mteja na mtumiaji mkubwa wa huduma za mtandao wa simu wa Vodacom Tanzania, ingawa simu yangu ina uwezo wa kutumia line mbili lakini mimi nimekuwa na simcard moja tu ambayo ni ya vodacom.
Nimekuwa mteja wao muaminifu kwa miaka mingi sana hasa katika huduma za vifurushi vya intanet. Leo nakiri na kusema ukweli bayana kuwa nimechoshwa na wizi kubwa wa MBS unaofanywa na vodacom dhidi yangu ingawa sijui na kwa watumiaji wengine wa mtandao huu.
Sichelei kuuita ni ufisadi kwa kuwa mimi nimekuwa na utaratibu wa kununua kifurushi cha intanent cha kanda ya ziwa ambazo wao huto mb1024 kwa siku kwa sh.1000. Mbs hizo zilikuwa zinanitosha kabisa kwa matumizi yangu ya internent ambayo sanasana ni kusoma na kujibu emails za wateja wetu pamoja na kuperuzi katika vyombo vingine vya habari na JF ikiwemo.
Nasikitika sana kua tokea mwaka huu umeanza kila nikinunua kifurushi hicho na nikiingia hotspot ili nipate intanet kwenye laptop yangu, hata nisipotumia ndani ya muda usiozidi masaa mawili naambiwa nimeishiwa na mbs za intanent. Nikajitahidi kuvumilia na kujitafakari kwa kina huku nikiweka mitego mbalimbali ya kutambua tatizo nini...
Jana nimenunua hicho kifurushi na usiku baada ya kucheki balance nikazima data nikalala leo asubuhi naamka ile naingia online baada ya dakika 5 nikaambiwa mbs zangu zimeishia ambazo usiku zilikua ni 856.
Baada ya kuona hivyo nikajiridhisha kua naibiwa na pia pengine sipo peke yangu hivyo basi nikaonelea nitoe taarifa kwa umma ili kila mtu achukua maamuzi stahiki.
Mpaka dakika hii nimewachukia sana vodacom na hasa ukizingatia pia wameanza kutumika kisiasa mpaka kukubali kwenda kutoa ushahidi mahakamani kuhusiana na kesi za wateja wao na huu wizi wanaoniibia mchana kweupe nimeamua kuondoka katika mtandao huu rasmi kuanzia leo tarehe 30 mwezi 1 mwaka2017.
Nawasilisha.