kaburunye
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 674
- 73
Wadau nimejaribu kufuatilia ofa ya Vodacom ya cheka time nikagundua hawa jamaa wanafanya uhuni. Kwa mfano ukinunua muda wa cheka time wa shs 400 unatakiwa upate dk 10 za maongezi na SMS 15 lakini hawa jamaa hawakupi dk 10 za maongezi km wanavyodai. Ikitokea umepiga simu kwa mtu chini ya dk 1 (kwa mfano sekunde 5 tu) wao wataihesabu kama dk 1. Kwa maana nyingine ukipigia watu 10 tofautitofauti na kila mmoja ukatumia sekunde 20 jamaa watahesabu dk 10 za cheka time zimeisha wakati umetumia sekunde 200 tu ambazo ni kama dk 3 na sekunde kadhaa. HUU NI UHUNI WA HALI YA JUU.