Vodacom acheni wizi aisee mtatuua kwa presha

Lemme say this

JF-Expert Member
Nov 4, 2023
397
1,064
Yani mtu unastress zako za hapa na pale unahangaika kupambana na maisha ya kila siku ili mradi mkono uende kinywani

Una biashara yako umekwama sehemu flani, ukaamua kuchukua buku ukanunue bando uingie JF uombe ushauri na kupata uzoefu tena buku uliotafuta kwa jasho lako aisee yaani you got heated by the sun all day long just to earn that thousand shilling

Unaingia dukani kununua vocha yako unaingiza namba chap then unaclick *149*01# kujiunga bando la buku mara unashtuka kenge flani anaefanya kazi kampuni ya voda anakwambia salio lako halitoshi dadeki
Na ukicheki salio unakuta 8 hundred wakati few minutes ago ulikuwa one thousand kabisa hapo means 2 hundred wamebeba

Sasa hiyo 800 unanunua bando gani? Na ukitaka kuongeza vocha tena ili kiasi kitimie let's say 500. Hawa jamaa wanapita na 200 nyingine bila ubishi ata ukibaki na hiyo 800 utaishia kununua bando la jero tu ubaki na 300 na hiyo 300 usipotumia mpaka kesho yake watapita nayo tu

Ukiimpigia customer care walahi kama we mchawi dakika moja si nyingi ushamroga tayari haki ya mama

Just imagine vijaña wa hovyo a.k.a walaumu CCM a.k.a "wife kaninyima papuchi" takriban millioni 5 wanakatwa 200 means voda wanapata billioni 1 yà dhuluma aisee

Hakuna mitandao ya hovyo kuwahi kutokea ulimwenguni kama ya hapa TZ
Tigo? Noo!!..… Airtel? a little but nooo!!..... Halotel? yereuwiiii..... Vodacom? Hell nooo!!

Bora ata Airtel kule angalau kuna nafuu ila sio voda aisee voda ni hatari kwa afya ya binadamu na stress za hapa na pale, kama unamatatizo ya presha nakushauri kaa mbali na voda mana uta-dead mapema

Juzi tu hapo mzee na siasa zake katoka kuvurugwa na CHADEMA akaniita

"We kariz! ebu nenda hapo kwa dogo fasta ukaninunulie voda ya buku"
Akanipa five thausand na mie nilikuwa na shida ya vocha ila mzee akanikatalia plus maneno ya hapa na pale si unajua siasa bhana
Nikaona isiwe shida nikamletea vocha yake nikakaa zangu nacheki muvi mara nasikiia paaah!!! Samsung ya mwezi jana hiyoo imeenda asikwambie mtu mzee aliongea kichina dadek, God bless CHADEMA!!

Sema nyie voda tunaishi nanyi kibishi tu mana hakuna namna ila daah Mungu anawaoña tu
 
Kama huwa sio mdaiwa jaribu kuwa unapitia mlango wa M'Pesa kununua vifurushi, buku lako peleka kwa wakala na uwekewe
 
Yani mtu unastress zako za hapa na pale unahangaika kupambana na maisha ya kila siku ili mradi mkono uende kinywani

Una biashara yako umekwama sehemu flani, ukaamua kuchukua buku ukanunue bando uingie JF uombe ushauri na mara nasikiia paaah!!! Samsung ya mwezi jana hiyoo imeenda asikwambie mtu mzee aliongea kichina dadek, God bless CHADEMA!!

Sema nyie voda tunaishi nanyi kibishi tu mana hakuna namna ila daah Mungu anawaoña tu
Hata sijasoma ila kufa tu Mzee
 
Mimi huwa nashangaa kutumiwa message za promo za makampuni mapya ya kubeti ingawa nh kweli nabeti.

Ukiwauliza voda wanakwambia sisi hatujatoa namba yako kwa makampuni ya kubeti labda uwapigie wenyewe wakuondoe (wanakupa namba).

Sasa cha kujiuliza, makampuni mapya ya kubeti wanapata wapi namba za wabetiji kama sio voda wanauza taarifa za wateja ambao huwa wanadeposit kwenda kwa makampuni ya kubeti!
 
Aiaeee ila kwa upande wangu nafurahia.
Niliacha kutumia voda sababu hiyo nikawa naiacha tuu sasa wakaaza kuni miminia ofa sijakaa sawa una mb 500 mara dk 20 yani kwa wiki sikosi 2 hadi 3 gb na dk hadi nakosa pakupeleka kuna muda hata sms haiji nikiangalia salio naona kuna mb buku

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mimi huwa nashangaa kutumiwa message za promo za makampuni mapya ya kubeti ingawa nh kweli nabeti.

Ukiwauliza voda wanakwambia sisi hatujatoa namba yako kwa makampuni ya kubeti labda uwapigie wenyewe wakuondoe (wanakupa namba).

Sasa cha kujiuliza, makampuni mapya ya kubeti wanapata wapi namba za wabetiji kama sio voda wanauza taarifa za wateja ambao huwa wanadeposit kwenda kwa makampuni ya kubeti!
Wanatuuza tu sijui wanatuona sie slaves
 
Jaribu kuondoa internet bila bundle. Internet iwe ni mpaka uwe na bundle tuu. Hii itakusaudia isitumie vocha yako baada tuu ya kuweka. Piga 149*01 then self service then bundle usage then utaona...
 
Back
Top Bottom