Vocha ya Airtel ya Tshs 1000/- ....... !!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vocha ya Airtel ya Tshs 1000/- ....... !!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by trachomatis, Mar 3, 2012.

 1. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Miezi miwili iliyopita nilikuwa jijini Dar...
  Nilinunua vocha tajwa nikaikwangua(scratch),bahati mbaya ikakwanguka vibaya... Nilipowapigia kitengo cha huduma kwa wateja na kueleza tatizo langu,walisema niende kwenye ofisi za Airtel zilizo karibu na mimi.

  Nilipouliza kama nikiwatajia "serial number" ya vocha hiyo hawawezi kunisaidia,walinijibu hawawezi zaidi ya ushauri wa kwenda kwenye ofisi za Airtel.
  Ingawa nikiwa Dar,naishi Kinondoni,Block 41,sikuona ulazima wa kufunga safari ya kwenda kuomba kubadilishiwa vocha hiyo. Niliona ni usumbufu kwa mteja.
  Nilikuja kuigawa kwa watoto wiki mbili zilizopita. Wao walifanikisha kuingiza tarakimu zilizoharibika,wakafaidika nayo.

  Jana nilinunua tena ya thamani hiyohiyo,ikaharibika vibaya mno! Nikaitunza na nikaamua kununua nyingine na kumwambia muuzaji anikwangulie.. Jirani yangu naye alifika na kuagiza vocha ya aina hiyohiyo akakwangua vibaya naye pia. Naye akalazimika kununua nyingine.

  Nikatoka hapo nikaenda kwenye duka lingine lenye kutoa huduma ya tigo pesa,airtel money,na m-pesa. Nilipohadithia kisa changu,dada mmoja alidakia na kusema alipata kuona mtu akipata hasara ya sh 2,000 kwa vocha aina hizo. Na bwana mmoja naye alisema yeye amepata balaa kama hilo mara sita!

  Je wenzangu mmepata masahibu kama yetu?
   
 2. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bado......
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Mimi bado,ila nakupa ushauri: Tafuta mtandao mwingine. makampuni yote ni majizi, wizi ukizidi hapa unahamia pale. ndio bahati ya kuwa na alternative. najua utapata shida ya kuhamisha namba na mazoea, lakini katika vibaya ulivyonavyo chagua afadhali!!!
   
 4. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Au we unatumia zaidi zile za jerojero.. zile hazina shida nadhani..
   
 5. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Na hawa Airtel ni wadhamini wetu humu JF..

  Siongei kwa nia mbaya.. Ila waangalie namna ya kuhandle wateja wao...
   
 6. Arabii

  Arabii Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani hiyo vocha ni balaa mi nimeshapata hasara mara 3 nimewahama.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  kwangueni taratibu hizo vocha, nguvu za nini ?
   
 8. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Sana yaani...
  Mimi nafikiria niamue lipi niache lipi!
   
 9. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Labda wakwangua kwa kitu cha ncha kali, karatasi zao siku hizi ziko laini.
   
 10. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Bado mnanunua vocha tu? Weka hela tigo-pesa, m-pesa, Airtel-money etc na jinunulie airtime mwenyewe.
   
 11. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Za airtel, si ndiyo...?

  Maana nguvu ninazoapply kwenye vocha za Airtel za sh 500/- na ninazoapply kwenye vocha kampuni nyingine kwa mfano ni zilezile..
   
 12. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Sawa..lakini kwanini za Airtel,na hasa za buku?

  Na pili,nimeshaikwangua vibaya,je bado nilazimike kuwafuata kwenye ofisi zao? Is that fair..?!
   
 13. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ushauri mzuri.. Nashukuru..
   
 14. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  ....ata mimi tatizo kama hilo la kukwangua vocha hadi namba futika limenipata,na nimeipeleka hiyo vocha ofisi ya aitel leo ni siku 7 bado hajantumia salaio...
   
 15. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ambao hawajakutana na tatizo hilo,nadhani wana personality tofauti sana..
   
 16. chubulunge

  chubulunge Senior Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  oky tumewasikia tutayafanyaia kazi matatizo yenu, hamia airtel wewe jamaa na marafiki zako
   
 17. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  We customer care?
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  ukiwa na coin unakwangua lightly, sio utumie miguvu mpaka jasho linakutoka. Si kwa airtell tu bali mitandao yote
   
 19. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana, ila kwa kuwa sasa umeshalijua tatizo, chukuwa tahadhari au mwachie anayekuuzia aikwangue kisha akusomee namba tu.
   
 20. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Trachomatis, unajua humu JF kuna watu wamezoea mizaha na hata kama jambo hawalijuia maadamu wana access na mtandao basi wataweka utumbo wao. Kama ingalikuwa katika mazungumzo basi ningaliwaita waropokaji.

  Hoja yako ni ya kweli. Na kiuchumi inamadhara makubwa.

  Siku alipokuwa anazikwa Mar Regia, nalinunua vocha za 1000/= mbili pale Moro mjini. Zote zilichubuka nikashindwa kuingiza. Nilipomwambia mwenye duka akaniambia hajui kwanini zinachubuka, kisha akanishauri niende ile ofisi ya Airtel Moro. Nilifanya kama nilivyoelekezwa.

  Nilipofika pale ofisini, mhudumu kwa wateja (kijana wa kiume) akaniambia hana namna ya kunisaidia zaidi ya kuzichukua zile vocha na kuwajulisha Makao Makuu, wao wataniingizia muda wa hewani kwenye simu yangu. Akaniomba nimpe zile vocha. Akabandika kwenye karatasi na kando yake akaandika namba yangu ya simu.

  Nikiwa namuhoji maswali mazito, ndipo akanionyesha karatasi nyingine 4 ambapo @ ilikuwa na wastani wa vocha 30-40 zimerudishwa. Pia kukawa na kopi 6 za namna ya karatasi hizo ambazo zile zenye vocha halisi alikuwa ametuma Dar. Akanambia kuna vocha zilizoletwa zina matatizo, hivyo wameitambua batch husika na wameizuia kuisambaza. Na zile zilizoingia sokoni hawajaanza kuzirudisha.

  Hadi leo hii hiyo 2000/= hawajanirudishia. Niliwahi kuwapigia customer service nikawatajia serial no. zake wakaniambia nisubiri sekunde chache nisikate simu. Mara simu ikakatika, sikukata mimi. Toka hapo kila nikiwapigia naishia kwenye kale kawimbo tu. Sipokelewi.

  Wiki iliyopita nilinunua vocha pale maeneo ya Manyanya. Ilikwanguka tarakimu tatu. Nimeitunza hiyo vocha ('cause that is money). Nangojea siku nitakaposaidia kwa hizo mbili, naunganisha na hiyo.

  Sasa hebu tufikiri ni kiasi gani zipo kwenye mzunguko? Ni kiasi gani cha pesa ya watz kinapotea kwa huduma sifuri?

  Airtel wanatakiwa kulishughulikia hili mapema kwa umakini na kuhakikisha halijirudii.
   
Loading...