Vizuizi vinavyomfanya mtu ashindwe kuoa/kuolewa kwa wakati Kimaandiko

Slas Nature

Member
Oct 18, 2013
36
72
Habari za wakati huu ndugu zangu.! Naamini kila mmoja yu salama akiendelea na harakati za maisha, kwa wale wenye changamoto kadha wa kadha za kimaisha basi Mungu akakutetee.

Leo nimependa kukushirikisha baadhi ya vizuizi vinavyomfanya mtu ashindwe kuoa au kuolewa kwa wakati kwa mujibu wa maandiko.

Karibu tujifunze.

1. Historia mbaya (Urithi mbaya)
Wako watu ambao wanatoka katika familia au koo zenye historia mbaya katika katika masuala ya ndoa. Unaweza kuta asilimia 80 ya wasichana kwenye familia au ukoo wote huzalia nyumbani kabla ya ndoa au wengine huishi na wasichana bila kuoa na ukichunguza utagundua tatizo hilo si lako tu hata ndugu zako pia wanalo. Maandiko yanasema

1 Petro 1:18
[18]Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu"

Hivyo kuna mwenendo usiofaa ambao unaupokea kutoka kwa baba zako (wazee waliokutangulia) ambao kama usipokombolewa basi utajikuta unaishi katika mwenendo huo huo usiofaa wa baba na babu zako.

2. Kuishi maisha ya dhambi kwa makusudi.
Mungu huwa anapenda kuwafurahisha watoto wake na kuwabariki na kuwatendea mema. Anapenda muda wa mtu ukifika wa kuoa au kuolewa basi akusogezee mtu sahihi kwako ambaye anajua mtatengeneza familia bora kwa utukufu wake. Na ndio maana maandiko yanasema;

Mithali 19:14
"[14]Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA."

Lakini Mungu anashangaa anapomuona mtu ameamua kuishi maisha ya dhambi kwa makusudi bila kujua kwa kufanya hivyo anajikwamisha yeye mwenyewe kwa kukosa baraka zile njema ambazo Mungu amekusudia, maisha ya dhambi yanakufanya ukose mema ambayo Mungu amekukusudia, utachezea watoto wa watu na kuharibikiwa na kama ni msichana basi utatumiwa na kutelekezwa na mwisho unaweza kuishia pabaya zaidi. dhambi huonekana ni tamu kwa nje lakini huaribu mwili, nafsi na roho na kukutenga na uso wa Mungu, Si kwamba Mungu hataki kukubariki lakini aina ya maisha uliyochagua yanamzuia kukubariki na kukupa mke au mume bora kutoka kwake.

Isaya 59:1-2
[1]Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
[2]lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Mkono wake unaweza kukuokoa na sikio lake sio zito kusikia maombi na haja ya moyo wako lakini... dhambi na maovu yanamfanya asikutazame na kukusaidia.


3. Mashambulizi ya nguvu za giza
Shetani huwa hapendi watu wafanikiwe, huwa anatafuta kila mbinu kuhakikisha anakuzuia usifanikiwe bali uishi maisha ya dhiki, taabu na shida.. Watu wengi hushambuliwa na nguvu za giza na kuwafanya washindwe kuoa au kuolewa kwa wakati na hata ikitokea umeoa au kuolewa basi maisha yako ya ndoa yatakuwa mabaya na kuona bora usingeoa au kuolewa, baadhi ya mashambulizi hayo hudhihirika katika ndoto (ndoto za kuota unazini) na kujikuta unaunganishwa na roho za kipepo zitakazofilisi uwezo wako wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi. Maaandiko yanatueleza..

Yohana 10:10a
[10]Mwivi(shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;

Ina maana shetani anaweza kuiba baraka zako (za mume au mke) au akaua kabisa usiolewe au akaharibu hata mahusiano uliyonayo.. na ndio maana baadhi ya watu wamekua wakianzisha mahusiano na baada ya muda yanaharibika (yanavunjika) na anaanza tena upya., ni kuumizwa, kuacha na kupenda tena kisha kuumizwa na kuachwa tena.

Ni maombi yangu kwako ukatafakari maisha yako na kuamua kubadili baadhi ya mambo ili Mungu akusaidie.

Mungu akinipa nafasi tutaendelea na sababu nyingine kadhaa zilizobaki.

Bwana na akubariki.
 
Habari za wakati huu ndugu zangu.! Naamini kila mmoja yu salama akiendelea na harakati za maisha, kwa wale wenye changamoto kadha wa kadha za kimaisha basi Mungu akakutetee...

Leo nimependa kukushirikisha baadhi ya vizuizi vinavyomfanya mtu ashindwe kuoa au kuolewa kwa wakati kwa mujibu wa maandiko...
Mtu akilokoka pia huchelewa kuoa au kuolewa, sijui kwanini? Je ulokole ni level fulani ya ukichaa au jamii yetu imeamua tu kudharau au watu wanao jifanya wameokoka
 
Mtu akilokoka pia huchelewa kuoa au kuolewa, sijui kwanini? Je ulokole ni level fulani ya ukichaa au jamii yetu imeamua tu kudharau au watu wanao jifanya wameokoka
Natamani nijibu ila duh!

Anyway,nitarudi
 
Back
Top Bottom