Viwango Hivi Vya Elimu Vimepitwa na Wakati!

katika definition nyingi za siasa nilizokutana nazo binafsi hii ndio iliyonikaa na nimeipenda inaenda hivi, siasa inatokana na kwa kuwa binadamu ni viumbe vinavyopenda kuishi kijamii. kwa hivyo jamii ili ifanikiwe inahitaji muongozo na muelekeo utakao tumia vizuri resources ambazo zinahitajika kwa wote.

Hivyo there are bound to be conflicts on how to use those resources which are short of supply. Hiyo ni kazi ya wanasiasa kujua jinsi gani ya kuweza kusambaza resources katika jamii, kwa nani na kwa kifungu kipi. Hivyo siasa ni mchanganyiko wa kujua jinsi ya kuweka maaumuzi katika jamii na namna ya kuchagua maamuzi ambayo wakati mwingine ni magumu kumridhisha kila mtu. kwa mtaji huo ni muhimu wanasiasa kuweza kuwa wabunifu kuja na mbinu za kuweza kuuridhisha Umma kutokana na tulichonacho katika ardhi (economics come into play). Kinachohitajika ni better muongozo, uendeshaji, mbinu za uzalishaji, kuchota akili, ushindani wa mawazo na little conflict (uhuru wa kuuliza, aka direct partricipation politically). Hapo tu unahitajika ujuaji wa masomo kama manne hili mtu aweze jua whats the score in simplicity.

Kwa kuwa siasa ni hivyo, basi tunahitaji na jumba la kuweza kuweka wawakilishi hili sauti za wengi zisikiwe through representation, in modern times the house of reps is also a legislature therefore decisions are made which affect the whole by a handful of executives kwa kweli jumba hili alistahili mtu asiejua kinachoendelea mule ndani. Just imagine the shyt that went into our parliament from ufisadi to poor policies on our resources. Hata watu wanashindwa kum-baini kwamba Mkullo ana anachokijua. Halafu humo kweli tuweke akina MC sijui nani, hell no huwa nashangaa kuona viongozi wakuu wa chama wakiandanamana na Bongo flava mc's. KHAAA!
 
Kwa baadhi ya nchi za watu "elimu" ingekuwa ni kigezo basi dunia hii isingepata akina Luis Inacio Lula da Silva na akina John Major.

Mimi nathamini zaidi uwezo wa mtu. Na elimu ya darasani si uwezo wa kuwa kiongozi. Elimu ya darasani si uadilifu. Elimu ya darasani si uelewa wa matatizo yanayowakabili watu.

Napendelea zaidi viongozi, wawe na elimu ya darasani au ya maisha, wanaojali watu wao.

Nitamchukua mtu muadilifu asiye na "elimu" siku yoyote muda wowote dhidi ya Andrew Chenge na midigirii yake sijui ya Harvard na wapi huko....
 
Ukweli ni kwamba BUNGE NI MZIGO wa kinyesi tu. Tunajaribu kukwepakwepa tu na kufanya sugar-coating ..aarrgg, miafrika bana.
 
Tuna kazi kubwa sana mbele yetu (sisi tulioenda shule)..............kuthibitishia Watanzania kuwa kuna tofauti ya aliyeenda shule na asiyeenda shule...............THATS A FACT................tusiwalaumu hata kidogo wananchi...............kwa sababu hawaoni tofauti...........na hili ndilo suala linalokuzwa na MAJAMBAZI CCM............kwani limeachia wezi wa elimu "kupeta".............na wasomi wa CCM kubariki ufisadi...........

Kweli kabisa Mkuu Mwawado...................tusipochukua hatua madhubuti.............hasara yake ni kubwa sana..............

Ogah;you make my day! na sina cha kuongeza na ulichoongea ni kweli tupu na hali ndiyo ilivyo;HAMNA TOFAUTI YEYOTE YA UWAJIBIKAJI KATI YA WABUNGE WASOMI NA WASIO WASOMI !

Kama kungeonekana utofauti wa maendeleo kati ya majimbo yanayoongozwa na wasomi na yale yanayoongozwa na watu wa darasa la 7 basi likely majimbo mengi yangeiga nao kutaka kupata wabunge wasomi ili wakombolewe!

Mfano;Rufiji imewahi kuongozwa na wabunge wengi wasomi,je fikra za Mbunge msomi Prof Mtulia zimeweza kuwapa dira jinsi ya kuwaokoa kwenye lindi la umaskini watu wa Rufiji pengine zaidi ya Mbunge wa Buchosa aliyemaliza darasa la 7 tu Samwel Mchele Chitalilo?Kumbuka hawa wabunge wote 2 walikuwepo bungeni kwa miaka takribani 10 na sidhani kama wana tofauti yeyote kwa wapiga kura wa majimbo yao kuwadumiza kimaendeleo!

Elimu sio vyeti tu bali ni mambo mengi sana yanabidi yaangaliwe!
 
Khee!! Miafrika bana kwa kupapatikia elimu ya wazungu tu haijambo. Haya hilo libunge lenu lililojaa maprofesa, madokta, mawakili "wakali" kama kina Mkono (lol), wasomi wa Harvard kina Chenge na wengenieo mpaka sasa limefanya nini cha maana? Mbona nchi yetu bado maskini wa kutupwa? Ingekuwa elimu ni ya muhimu hivyo basi kwa Afrika Nigeria ingekuwa kama Marekani....go figure!!!!

Total bullshit. Nionyeshe umakini wa kuchambua mambo ulioonyeshwa na 'wasomi" walioko bungeni. Acheni dharau na hizo elimu zenu za madarasani. Hata maisha nayo ni elimu.

Nyani Ngabu;

You have some good points lkn jinsi ya lugha ya kutumia kutufikishia ujumbe wako ndiyo nahisi kuna kasoro;Je hauwezi kutumia lugha ya "kizalendo"kutufikishia ujumbe wako zaidi ya lugha hizi "negative" ulizotumia kumjibu mwana JF mwenzako Keil?
 
Khee!! Miafrika bana kwa kupapatikia elimu ya wazungu tu haijambo. Haya hilo libunge lenu lililojaa maprofesa, madokta, mawakili "wakali" kama kina Mkono (lol), wasomi wa Harvard kina Chenge na wengenieo mpaka sasa limefanya nini cha maana? Mbona nchi yetu bado maskini wa kutupwa? Ingekuwa elimu ni ya muhimu hivyo basi kwa Afrika Nigeria ingekuwa kama Marekani....go figure!!!!

Total bullshit. Nionyeshe umakini wa kuchambua mambo ulioonyeshwa na 'wasomi" walioko bungeni. Acheni dharau na hizo elimu zenu za madarasani. Hata maisha nayo ni elimu.

Mkuu wangu NN nimesema wazi kwamba kwa mfumo wa Bunge tulio nao hata wakienda wasomi bado hawawezi kutoa michango iliyo constructive. Sababu nimeitoa kwamba ni Bunge la CCM, maana ni afadhali hata Bunge la zama za Chama Kimoja, kuliko hiki kiini macho. Nilisema hivi:

Sometimes it is frustrating na ninawashangaa hata ma-Dr na ma-Prof ambao wanakimbilia mjengoni ili hali mwisho wa siku wanapitisha madudu tu mpaka unajiuliza hivi wabunge waliopitisha miswaada hii wameenda shule kweli?

Kwa hiyo hata mimi sijaona michango ya ya hao wasomi na nikawashangaa kukimbilia Mjengoni ambako wanakwenda kujidhalilisha tu kwa kuunga mkono vitu ambavyo baadaye wakija kuvisoma hata wao wenyewe huwa wanajishangaa kama kweli walipitisha.

Kwa maneno mengine Bunge la sasa ni la waganga njaa, once kukitokea mabadiliko ya kweli huo mchezo wa kupitisha pumba ili kulinda sembe yao utaisha, wataanza kufanya kazi waliyotumwa na wananchi. So, for the time being hata wakienda ambao hawajasoma, it is OK, maana uwe na uelewa ama huna uelewa mwisho wa siku wote wataunga mkono hoja.
 
Kwa baadhi ya nchi za watu "elimu" ingekuwa ni kigezo basi dunia hii isingepata akina Luis Inacio Lula da Silva na akina John Major.

Mimi nathamini zaidi uwezo wa mtu. Na elimu ya darasani si uwezo wa kuwa kiongozi. Elimu ya darasani si uadilifu. Elimu ya darasani si uelewa wa matatizo yanayowakabili watu.

Napendelea zaidi viongozi, wawe na elimu ya darasani au ya maisha, wanaojali watu wao.

Nitamchukua mtu muadilifu asiye na "elimu" siku yoyote muda wowote dhidi ya Andrew Chenge na midigirii yake sijui ya Harvard na wapi huko....

Speaking of Lula, Brazil ipo katika BRIC, Lula si "msomi", Tanzania na Kikwete wetu "msomi" tuko wapi ?

Juzi Lula (asiyesoma) kaja bongo, katoa msamaha deni la Brazil dola za Marekani milioni 240 kwa rais wetu "msomi" Kikwete.

So much for "usomi"
 
SIASA ni profession ambayo haitatui matatizo ya jamii kisayansi, maana kimsingi haina hiyo expertise, lengo lake ni kuweka watu fulani juu kwene pyramid 'kisheria' halafu basi. Haijali sayansi kutatua matatizo ya watu, bali sayansi ya spins ili kughilibu watu na kuwafanya waamini kwamba wale watu waliopo juu kwene pyramid wapo kwa ajili ya kuwatumikia, which is actually the opposite in real sense.

Bunge ni sehemu ya ghilba hiyo, ambapo mwananchi anashawishiwa kwamba ati mbunge akiongea kwa sauti ya juu zaidi kule mjengoni basi matatizo yao ya kijamii yatatoweka kama kwene senema..So little these gullibles can see whats in front of them. Mwananchi anashawishiwa kwamba mwasiasa anao muarobaini wa kujenga barabara, kuleta hospitali, kuleta umeme na maji etc etc, huku akisahaulishwa ukweli ulio wazi kwamba masiha bora yanaletwa na mtaalam husika na katu mwanasiasa hakuwahi kuvumbua hata baiskeli ya mbao!

With this same silly mentality, watu wazima wengine wanaitwa 'baba' au 'mama', tena some of them ni 'wasomi' (i suppose these ones should have know better) wanaamini kabisakabisa na kuketi kitako kusikiza 'Dr.Mkwere' akiwasimulia kwa umahiri hekaya za barabara za hewani, wanasahau lililo muhimu zaidi, ambalo ni ku-demand mikakati ya kuongeza mapato ya serikali ili kuweza kujenga hata hizo barabara za vumbi walau zipitike walau kipindi kile cha mavuno tu!

Sasa naskia kizunguzungu ngoja niendelee na ratiba zingine, ukikaa kusikiza hoja za mifrika itakukirihi tu!
 
Hivi katika taifa la watu milioni arobaini hatuwezi kupata watu wenye combination ya elimu, uchapakazi, streetsmart (as others did put it), innovative, visionary etc. mpaka tucompromise na graduates wa grade seven?

Hiyo failure ya the so called wasomi wa CCM inaweza kuwa ni justification as to why bora viongozi pasipo elimu? Failure ya CCM ni systematic of which an individual hata uwe na akili kiasi gani bado ni ngumu kufanya mambo kwa faida ya taifa.

All in all walio wengi kwenye hilo group ni watu wenye hela kibongobongo na kwa sababu ubunge CCM is at a price haijalishi who comes to buy. Hivi wakuu mnawafahamu vizuri matajiri wa kibongo wasioenda shule? I guess some of the comments wouldn't be this way.
 
Kwa baadhi ya nchi za watu "elimu" ingekuwa ni kigezo basi dunia hii isingepata akina Luis Inacio Lula da Silva na akina John Major.

Mimi nathamini zaidi uwezo wa mtu. Na elimu ya darasani si uwezo wa kuwa kiongozi. Elimu ya darasani si uadilifu. Elimu ya darasani si uelewa wa matatizo yanayowakabili watu.

Napendelea zaidi viongozi, wawe na elimu ya darasani au ya maisha, wanaojali watu wao.

Nitamchukua mtu muadilifu asiye na "elimu" siku yoyote muda wowote dhidi ya Andrew Chenge na midigirii yake sijui ya Harvard na wapi huko....

We must run while they walk!!!

Tanzania hata katiba yetu leo bado ina matatizo mengi, tunashindwa kuandika mikataba mizuri yenye manufaa ya nchi, sheria zetu zote ziko shaghla baghla, bunge letu linapeleka kwa rais miswada yanye makosa, nchi bado inaongozwa kisiasa zaidi kuliko kuongozwa kitaalamu. Tunapokuwa na watunga sheria wasiojua wanachokifanya, tutazidi kubaki na matatizo haya. wakaati akina major walikuwa kwenye mifumo ambayo inajitosheleza sana kiasi kuwa mbunge alikuwa na wataalamu wa kumsaidia, sisi hatuko hivyo. Mbunge anachugukua hela zote za kulipia wataalamu na wasaidizi wake na kuziweka mfukoni mwake bila kuwa na mtaalu yeyote na wala hakuna anayemwuliza mbunge huyu katumiaje hela hizo.

....................We must run while they walk!!!!!!!!!

Mbunge wa darasa la saba mwenye elimu ya ngumbaru (kujiendeleza) hatufai katika Tanzania ya leo. To the best tungekuwa na wabunge at least wa kuanzia Form 6.
 
Elimu ni kuondokana na kutokujua ili kupambana na changamoto au mazingira. Ni vema kuchanganya elimu ya darasani (formal) na isiyo ya darasani (informal). Na elimu (informal & formal) aina mwisho. Ni muhimu kwa wagombea ubunge kuwa na elimu ya darasani pia kwa angalau form IV ya Div. II (au III). Udiwani: darasa la saba na urais: Good Masters au bachelor not less than GPA 3.5. Na wote wawe wame-graduate kutoka kwenye shule na vyuo vya humu nchini ukitoa open university!
 
Hizi ndio elimu za wabunge wateuliwa wa CCM
 
Attachments

  • ELIMU ZA WABUNGE WA CCM.doc
    242.5 KB · Views: 102
Ogah,

Tofauti kati ya mwizi kama Chenge na mtu kama Mzindakaya ambaye hajaenda shule ni nini ? Mimi ninachoona mtu kama Chenge "aliyeenda shule" anakuwa arrogant tu katika wizi wake kuliko mtu kama Mzindakaya. Na anaweza kupewa dhamana kubwa zaidi na kuharibu mambo mengi zaidi, eti kwa sababu tu "kasoma". Msomi wa kweli anaweza kuchukua rushwa ? Hivi kama tunataka kuweka standards za usomi kweli (achana na hizi longolongo za certification ambazo yeyote anaweza kuzinunua) mtu yeyote anayepita ubunge si atakuwa amekuwa disqualified usomi by default ?

Ndiyo maana mimi nakazania kuonyeshwa uwezo wa watu katika matendo, na kuacha hizi habari za usomi wa makaratasi. Kuna watu walioitafuna nchi yetu vilivyo na kuturudisha nyuma kimaendeleo kama wasomi ?

Generally speaking usomi unaongeza uwezo wa kuchambua mambo, lakini hii si irrefutable rule, kuna sehemu usomi unaongeza arrogance na hauleti tija, wasomi wanakuwa na dharau (Mkapa, Thabo Mbeki etc) na kwa sababu hii si lazima usomi - naongelea formal education, mtu anaweza kuwa kakua na Wahadzabe huko akawajua vizuri kuliko "msomi" yeyote na akawa more qualified kuwawakilisha- si lazima msomi mwenye formal education akawa ndiye muwakilishi mzuri kabisa.

Ndiyo maana nawaambia, niambieni hawa watu wamefanya au hawajafanya nini, msiniambie wana/ hawana degree/ cdertificate gani.

Thabo Mbeki na usomi wake wote alikuwa arrogant aliyeamini katika pseudoscience mpaka hakuamini kwamba kuna uhusiano kati ya HIV na AIDS, huyo Jacob Zuma, buffoon ambaye hajaenda shule, amekuwa rahisi zaidi kusikiliza watu kwa vile anajiona si msomi, na kwa sababu hii tayari kashaanza kuonyesha matokeo mazuri katika vita dhidi ya UKIMWI South Africa, you tell me anayewafaa wananchi hapa ni msomi au huyu "buffoon" ambaye hana western education ?

Again, elimu ni nini? elimu inapimwaje ? Je elimu ni madarasa uliyopitia? Inapimwa kwa ma certificate uliyopata ?

Exactly! Ni yale yale yakujiona kuwa waliosoma nio bora kuliko waliowapeleka shule. Hawa walichaguliwa na watu ambao wanaona wangewafaa zaidi, irrespective ya usomi wao. Unaweza kukuta waliishachagua wasomi wakaona adha yao. Hawakaribiki, wanajiona kuwa wao wanawafanyia fadhila waliowachagua na wanaona ubunge ni hatua ya kufikia wanakotaka kufika. Tunataka wawakilishi wa kweli wa waliowatuma, ambao loyalty yao itakuwa kwa hao waliowatuma na sio kingine. Hii infatuation na "formal education" ndiyo kwa kiasi kikubwa imetufikisha hapa. Labda sasa ni zamu ya wasiosoma lakini wenye uchungu na nchi yao kujaribu. Wasomi wabaki kuwa technocrats na wanasiasa wawakilishi wa wananchi.

Amandla....
 
Kwa kweli kuna haja ya kuweka viwango vya elimu vinavyoeleweka kwa mtu kuweza kugombea ubunge. Hivi hawa wataenda kuchambua mikataba ya madini bungeni wataielewa? Au miswaada inayoletwa bungeni imeandikwa kwa kiingereza, hawa watakuwa wanachangia nini?

Kuna sababu ya kubadilika kwa kweli.

Lakini si bunge letu ni la kustamp to misuada, hivyo elimu au si elimu si hoja.
 
Khee!! Miafrika bana kwa kupapatikia elimu ya wazungu tu haijambo. Haya hilo libunge lenu lililojaa maprofesa, madokta, mawakili "wakali" kama kina Mkono (lol), wasomi wa Harvard kina Chenge na wengenieo mpaka sasa limefanya nini cha maana? Mbona nchi yetu bado maskini wa kutupwa? Ingekuwa elimu ni ya muhimu hivyo basi kwa Afrika Nigeria ingekuwa kama Marekani....go figure!!!!

Total bullshit. Nionyeshe umakini wa kuchambua mambo ulioonyeshwa na 'wasomi" walioko bungeni. Acheni dharau na hizo elimu zenu za madarasani. Hata maisha nayo ni elimu.

NN,

Kwa kuwa wasomi waliopewa dhamana mpaka sasa (the likes of Mramba, Chenge etc) wameusaliti umma wa wa Tanzania kwa kufanya madudu yanayowanufaisha wao, hakujustify kabisa kuwa formal education haina maana kabisa linapokuja suala la kuchagua viongozi wetu!

Hao kina Chenge (na wasomi wengine waliotusaliti), wanajua pumba na mchele ni upi, lakini kutokana na kukosa maadili na uroho, uchoyo wao wametumia elimu yao kuweka mifumo inayowanufaisha wao binafsi! Sasa tukisema kwamba tupeleke Bungeni hawa watu wenye informal education, I assure you hawa watukuwa daraja au rubber stamp ya kupitishia midudu kibao ya wasomi wachache watakao ingia mjengoni!
 
Hawa Waheshimiwa walikuwa na degree ngapi?

Rashid Kawawa

Edward Sokoine

Karume Snr.

E.t.c
 
Kwa mantiki hiyohiyo si ni vema pia tukaweka kiwango cha elimu kwa wapiga kura? Maana kama ni tatizo hapa ndio lipo kubwa zaidi na kwa hakika linaweza kutatua hilo la pili!

Haki ya kuchagua au/na kuchaguliwa ni haki ya kila mmoja wetu, uwe na 'msomi' ama la.
 
NN,

Kwa kuwa wasomi waliopewa dhamana mpaka sasa (the likes of Mramba, Chenge etc) wameusaliti umma wa wa Tanzania kwa kufanya madudu yanayowanufaisha wao, hakujustify kabisa kuwa formal education haina maana kabisa linapokuja suala la kuchagua viongozi wetu!

Hao kina Chenge (na wasomi wengine waliotusaliti), wanajua pumba na mchele ni upi, lakini kutokana na kukosa maadili na uroho, uchoyo wao wametumia elimu yao kuweka mifumo inayowanufaisha wao binafsi! Sasa tukisema kwamba tupeleke Bungeni hawa watu wenye informal education, I assure you hawa watukuwa daraja au rubber stamp ya kupitishia midudu kibao ya wasomi wachache watakao ingia mjengoni!

Hivi darasa la saba au ngumbalu sio formal education? Nielewavyo mimi formal education ni elimu yeyote iliyokuwa institutionalised. Mtu yeyote aliyeingia darasani, akafundishwa kufuatana na syllabus ana formal education. Hata Fundi Mchundo mwenye grade test ana formal education.

Tunachopinga wengi si formal education bali dhana kuwa kipimo cha uwezo katika siasa kuwa formal education peke yake. hakuna mtu, hata Nyani Ngabu aliyesema kuwa nafasi za wabunge ziwe za wale waliomaliza darasa la saba peke yao. Tunachodai ni kuwa na wao wapewe nafasi ya kutoa mchango wao katika nyanja hii. Kama hao wasomi wanaona kuwa hawafai basi waingie ulingoni kushindana nao badala ya kukimbilia kuwa-legislate nje ya ulingo. Kama hao wenye elimu ya chini watajiunga na hao maprofesa kuwa raba stemp nao watatoswa bila ya kujali elimu yao. Kipimo kitakuwa utendaji wao, period. kama wataonekana wapungufu watoswe. kama vile wasomi walio pungufu wanavyostahili kutoswa.

Amandla....
 
Back
Top Bottom