Viwango Hivi Vya Elimu Vimepitwa na Wakati! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viwango Hivi Vya Elimu Vimepitwa na Wakati!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwawado, Aug 16, 2010.

 1. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Ndugu Wanabodi,

  Katika Mchakato wa kutafuta wagombea Ubunge kupitia Chama Tawala (CCM), kumetokea mwamko mkubwa kutoka kwa wananchi wa kawaida kutaka ridhaa ya kuwawakilisha wenzao Bungeni. Katika Mchakato huo kumetokea watu wa rika, rangi, dini na makabila tofauti. Utofauti huo wa wagombea unaonyesha ni kiasi gani demokrasia inakuwa Nchini kwetu.

  Kilichonishangaza Mimi,ni kiwango cha Elimu cha baadhi ya Wagombea waliopitishwa katika kazi hiyo muhimu ya Kutunga Sheria. Naomba nisionekane mbaguzi hapa, lakini ni ukweli usiopingika kuwa ni vyema tuchague watu wenye kiwango kizuri cha Elimu ili kuweza kukimbizana na mwendokasi huu wa maendeleo. Kiwango cha Elimu ya Msingi si kiwango kizuri kwa kazi ngumu ya mijadala na Utungaji sheria.

  Naomba Tume ya Uchaguzi (NEC) iweke utaratibu wa kutangaza angalau kiwango cha Elimu ya Kidato cha sita. Vinginevyo tutakuwa na kundi la Watunga sheria wasio na uelewa wa wanachosimamia.

  Hapa chini nimejaribu kuweka Majina ya Wagombea Ubunge waliopitishwa na NEC/CC ambao kiwango chao cha Elimu ni shule ya Msingi na kuna mmojawapo hana kabisa Elimu ya darasani.

  1; Deo Sanga (Jah People) (Njombe Kaskazini)
  2; Jamal A Tamim (Muhambwe - Kigoma)
  3; Lameck O Airo (Rolya - Mara)
  4; Moshi S Kakoso (Mpanda Vijijini - Rukwa)
  5; Stephen Ngonyani (Korogwe Vijijini - Tanga)
  6; Livingstone J. Lusinde ( Mtera - Dodoma)
  7; Hussein Nassoro Amar (Nyang'wale - Mwanza)
  8; Luckson Ndaga Mwanjale (Mbeya Vijijini) - Hana Formal Education.
  9; Mahmood Abuu Juma (Kibaha Vijijini - Pwani)
  10;Aeshi Khalfany Hillary (Sumbawanga mjini - Rukwa).

  Mniwie radhi kama nitakuwa nimewakwaza baadhi ya watu/wagombea katika bandiko langu hili.Lakini kwa mustakabali wa Taifa letu naomba tujadilane kwa hili.
   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu, si angalau hawa hawajaficha kiwango chao! Heri hawa kuliko ma Ph.D feki waliojazana kivbao. Na pengine hawa jamaa watakuwa karibu zaidi na wananchi waliowatuma hasa ukizingatia kuwa hawatakuwa na ndoto za uwaziri!

  Amandla....
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli kuna haja ya kuweka viwango vya elimu vinavyoeleweka kwa mtu kuweza kugombea ubunge. Hivi hawa wataenda kuchambua mikataba ya madini bungeni wataielewa? Au miswaada inayoletwa bungeni imeandikwa kwa kiingereza, hawa watakuwa wanachangia nini?

  Kuna sababu ya kubadilika kwa kweli.
   
 4. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ngoja tusubiri muziki wao pale watakapokuwa wanatunga sheria..........full madudu......the only way ni wananchi wa maeneo husika kuwapiga chini ..hatuwezi kuwa na bunge la vilaza...
   
 5. m

  mndebile Senior Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Sep 4, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu mie nakuunga mkono kabisa kwenye suala la elimu lazima lipewe kipaumbele, kama ofisi za serikali hata mfagia ofisi wanataka angalau au amemaliza kidato cha nne, vivyo hivyo kwa katibu kata/tarafa/dereva. Inakuwaje mbunge awe darasa la saba? kama ana kipaji akakioneshe kanisani au msikitini nako kuna watanzania wengi wanahitaji msaada wake, bunge naamini ni sehemu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na tunataka angalau wawakilishi wetu wawe na kiwango kizuri cha elimu si lazima shahada lakini angalau kidato cha nne.
  Kama mtindo ndo huu kutakuwa na maana gani ya kusoma, kama watunga sheria na wadhibiti wa serikali ndo hao tunawajaza darasa la saba? au hizo miswada na mambo mbalimbali yatakayo kuwa yanafanyika bungeni wao watakuwa wasindikizaji tu au vipi? wakitegemea akina Mwakyembe, Zitto ndo wawakilishe wao?
  Hii kitu mie siungi mkono kabisa na hii inatokana na katiba yetu kuwa na mapungufu kibao maana inaruhusu mtu wa namna hiyo kuwa kiongozi kama atachaguliwa au kuteuliwa.
   
 6. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Mjadala kama huu tulisha uweka hapa JF na ukazua maelezo meeengi. Wengine wakitetea hilo eti kama sehemu ya uwakilishi na wengine wakianza hata kuhoji maana ya elimu. Ni kukaa darasani au kufahamu mazingira yanayokuzunguka.

  Yote haya yanahitaji mjadala ingawa ktk dunia hii njia moja inayotumika kupima viwango vya elimu inaeleweka. Hayo mambo ya kutoingia shuleni halafu ukadai umeelimika ni sawa lakini kuna vikwazo vya nini unaweza ukaelimika juu yake ukiwa nje ya darasa. Kuna mambo huwezi kujielimisha bila kuingia darasani hata uishi miaka 100+.

  Lakini pia tujiulize wale wenye degree za viwango vyote kwa nini wananchi wawaone hawafai kiasi hicho? Lakini hii pia inaweza ikachangiwa na kuruhusu sifa ndogo kiasi hicho. Eti kujua kusoma na kuandika. Ukisha shusha sifa kiasi hicho basi ... Ukisema hata wabakaji wanaruhusiwa, pamoja na kufahamu kabisa kwamba wananchi wanawachukia, lazima utegemee kwamba watakuwemo tuuuu kwa sifa hiyo!

  Ugomvi wangu mkuu kuhusu hii kazi/wajibu/au..., hii ya ubunge ni mshahara na marupurupu yake. Haya ndo tatizo. Hayalingani na sifa ya waombaji au washindi. Mtu anayepatikana kwa sifa ya kujua kusoma na kuandika tu unamlipa milioni 7 + marupurupu? Kiasi kwamba zaidi ya asilimia ~95 ya wabunge wakikosa ubunge hawawezi pata ajira inayoweza kuwalipa hata robo ya mshahara wanaopata sasa hivi.

  Ndo maana inakuwa ni kufa kupona!

  Kama kweli kazi hii ni ya watu hata wa elimu ndogo kiasi hicho lazima tukubali kwamba mshahara huo siyo stahili yao.
   
 7. m

  matejoo Member

  #7
  Aug 17, 2010
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu aliwahi kuniambia elimu ya Tanzania mwisho wake ni ubunge akimmanisha it is the ultimate goal of many if not most elites. Kwa bandiko hili naona ubunge ni mwanzo wa elimu haswa kwa huyo asiye na formal education kabisa. Ukiondoa bureaucracy tunazojiwekea wenyewe, mimi nadhani hakuna sababu ya kumzuia mtu kwa kuwa eti "hakusoma". Hii ikiendelea na marupurupu kupunguzwa kidogo itatusaidia kidogo kupunguza "enthusiasm" ya wasomi kukimbilia bungeni na kuacha kufundisha vyuo vikuu, utabibu etc.

  Pia kwa nchi kama Tanzania kuwaita wabunge "watunga sheria" ni hoja isiyo na mshiko sana. Infact hawatungi, wanapitisha. Kazi yao kubwa ni "kuisimamia serikali" na hili limeendelea kuwa tembo mweupe kwa muda mrefu. Halitokani na kiwango cha elimu. Those with PhDs are the firs to chicken themselves ili wapewe vyeo. The bottom line is let these guys LEARN by DOING!
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hapo tusi walaumu wagombea hao bali tuilaumu educational system yetu. Kwa mfano nchi kama Japan kiwango cha chini cha elimu ambayo serikali ina kazania ni mpaka kiwango ambacho ni equivalent na form four yetu huku. Marekani nao mwanafunzi yoyote akisoma kwenye public school ni bure kuanzia msingi mpaka high school. Hii imefanywa makusudi ili kiwango cha chini cha watu wengi walau kiwe juu. Sasa sisi kwetu watoto wengi ambao ni masikini wana soma bure mpaka la saba tu ambayo kwa makusudi tumeamua kuuita shule ya msingi (meaning ukisha fikia kiwango hicho basi walau elimu yako tayari ni msingi). Matokeo yake ni kwamba wengi wanaishia la saba. Tunge weka priority kwamba watu walau wasaidiwe na serikali kusoma hadi form four au form six basi baada ya muda uta kuta kwamba watu wengi wana walau elimu hiyo na wale ambao wata kuwa na elimu chini ya hiyo upeo wao uta onekana kwa wapiga kura. Sasa wapiga kura wengi wameishia la saba au chini akitokea mgombea aliyeishia la saba si wata muona ni msomi tu kwa macho yao?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 17, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Kiwango cha elimu ambacho ningependelea mimi kiwe moja ya sifa za kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika pamoja na kuwa na akili timamu.

  Bunge ni la wote na ni muhimu liakisi watu wote kwa ujumla hata wale walioishia darasa la saba ili nao wajisikie angalau kuna watu wanaowawakilisha ktk hilo jumba la watu.

  Kwa nini muwe wenyewe tu mliosoma hizo shule zenu? Kwani maisha sio elimu? Hebu acheni hizo bana.

  Msitake kabisa kuniambia kuwa watu wasio na elimu ya kidato cha sita au wale wasio na shahada kuwa hawana mchango katika mustakabali wa nchi yetu. Hao wasomi wametufikisha wapi leo hii na hayo madigirii yao?

  Man get the hell outta here....
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ahh..hapo mtajarudi palepale kwene conclusion kwamba mchezo wa siasa ni maigizo tuuuu, hata uugeuze kichwa chini miguu juu, kushoto kuweka kulia and vice versa, kusini kueke kaskazi and vice versa, bado utagundua mchezo wa siasa hau-make sense hata chembe.

  Nilishajiuliza mara kwa mara kwamba mfumo wa bunge letu tukufu (really??) ni kama ngomani tu kila mtu anajiingilia na kujitokea zake bila kuwa na criteria zozote za kitaalam, sasa hii ni premise ya wazi kwamba bunge lazima tu litafika mahali litabakia kubwata tu maana halina meno (mamba bila meno??) ya kusasambua mambo yanayohitaji muktadha wa utaalam na usomi..ndio unapokuja kushangaa mbunge maamuma anautaalamu gani wa kufumua bajeti? au anaweza vipi kuisimamia serikali inayoajiri watu wenye taaluma zao??

  Ukifikiria saaaana utaishia kuwa chizi tu..
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Elimu ni nini? Na elimu inapimwaje?

  Eelimu ni madarasa? Elimu inapimwa kwa degrees na certificates ?

  Tuambie hawa watu wamefanya au hawajafanya nini, usituambie hawajafikisha au wamefikisha viwango gani vya elimu, viwango ambavyo vinaweza hata visiwe relevant katika mazingira yetu.
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hao wote walioorodheshwa ni hao waliopendekezwa na ccm bado hawajawa wabunge. Kuna wengine kati ya hao nina hakika kuwa hawawezi kuingia mjengoni, mmoja wao akiwa huyo wa Mbeya vijijini!!
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Aug 17, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Mimi nataka watu walio pragmatic na wenye virtue. Nataka watu wataoleta common sense solutions za matatizo yanayotukabili.

  Sasa I could care less na hayo madigirii. Give me somebody who can solve problems. Afterall, don't underestimate the strength of knowledge obtained from the school of hard knocks.
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kabla hatujaenda mbali nadhani tutafakari nini hasa maana ya bunge na kazi za bunge?
   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tuna kazi kubwa sana mbele yetu (sisi tulioenda shule)..............kuthibitishia Watanzania kuwa kuna tofauti ya aliyeenda shule na asiyeenda shule...............THATS A FACT................tusiwalaumu hata kidogo wananchi...............kwa sababu hawaoni tofauti...........na hili ndilo suala linalokuzwa na MAJAMBAZI CCM............kwani limeachia wezi wa elimu "kupeta".............na wasomi wa CCM kubariki ufisadi...........

  Kweli kabisa Mkuu Mwawado...................tusipochukua hatua madhubuti.............hasara yake ni kubwa sana..............
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lakini kwenye uchaguzi mdogo alishinda, una uhakika gani kwamba mwezi Oktoba atashindwa kupita?
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Ogah,

  Tofauti kati ya mwizi kama Chenge na mtu kama Mzindakaya ambaye hajaenda shule ni nini ? Mimi ninachoona mtu kama Chenge "aliyeenda shule" anakuwa arrogant tu katika wizi wake kuliko mtu kama Mzindakaya. Na anaweza kupewa dhamana kubwa zaidi na kuharibu mambo mengi zaidi, eti kwa sababu tu "kasoma". Msomi wa kweli anaweza kuchukua rushwa ? Hivi kama tunataka kuweka standards za usomi kweli (achana na hizi longolongo za certification ambazo yeyote anaweza kuzinunua) mtu yeyote anayepita ubunge si atakuwa amekuwa disqualified usomi by default ?

  Ndiyo maana mimi nakazania kuonyeshwa uwezo wa watu katika matendo, na kuacha hizi habari za usomi wa makaratasi. Kuna watu walioitafuna nchi yetu vilivyo na kuturudisha nyuma kimaendeleo kama wasomi ?

  Generally speaking usomi unaongeza uwezo wa kuchambua mambo, lakini hii si irrefutable rule, kuna sehemu usomi unaongeza arrogance na hauleti tija, wasomi wanakuwa na dharau (Mkapa, Thabo Mbeki etc) na kwa sababu hii si lazima usomi - naongelea formal education, mtu anaweza kuwa kakua na Wahadzabe huko akawajua vizuri kuliko "msomi" yeyote na akawa more qualified kuwawakilisha- si lazima msomi mwenye formal education akawa ndiye muwakilishi mzuri kabisa.

  Ndiyo maana nawaambia, niambieni hawa watu wamefanya au hawajafanya nini, msiniambie wana/ hawana degree/ cdertificate gani.

  Thabo Mbeki na usomi wake wote alikuwa arrogant aliyeamini katika pseudoscience mpaka hakuamini kwamba kuna uhusiano kati ya HIV na AIDS, huyo Jacob Zuma, buffoon ambaye hajaenda shule, amekuwa rahisi zaidi kusikiliza watu kwa vile anajiona si msomi, na kwa sababu hii tayari kashaanza kuonyesha matokeo mazuri katika vita dhidi ya UKIMWI South Africa, you tell me anayewafaa wananchi hapa ni msomi au huyu "buffoon" ambaye hana western education ?

  Again, elimu ni nini? elimu inapimwaje ? Je elimu ni madarasa uliyopitia? Inapimwa kwa ma certificate uliyopata ?
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa nature ya kazi za Mbunge, elimu ni muhimu sana. Tunapokuwa na Mbunge ambaye hana formal education ama ameishia darasa la saba ni hatari zaidi. Miswaada ya sheria ya ikienda Bungeni hawaichambui kwa umakini, siku sheria ikishindwa kufanya ndiyo utawasikia wanaanza kupiga kelele na kulalamika kwamba sheria hii ni mbaya au ina mapungufu.

  Pamoja na hayo, hata wakipendekezwa wagombea wasomi, kwa mfumo wa Bunge tulilo nalo bado ni kazi bure, kwani ni Bunge la CCM. CCM siku zote wakiona wabunge wao wamekuwa mbogo huwa wanaitana chemba kwanza, wakitoka huko wanalinda maslahi ya serikali kwa kutumia wingi wao.

  Sometimes it is frustrating na ninawashangaa hata ma-Dr na ma-Prof ambao wanakimbilia mjengoni ili hali mwisho wa siku wanapitisha madudu tu mpaka unajiuliza hivi wabunge waliopitisha miswaada hii wameenda shule kweli?

  Mfumo wa Bunge ukibadilika tutaweza kuwa na Bunge effective ambalo litakuwa linahitaji watu wenye uelewa mkubwa wa mambo mbali mbali na hivyo kuwa na michango ambayo iko constructive. Lakini kwa hali iliyopo sasa, hata wakienda wasomi bado ninaona ni sawa na wale ambao hawajasoma maana mwisho wa siku wataunga mkono hata madudu ya ajabu.
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Aug 17, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Khee!! Miafrika bana kwa kupapatikia elimu ya wazungu tu haijambo. Haya hilo libunge lenu lililojaa maprofesa, madokta, mawakili "wakali" kama kina Mkono (lol), wasomi wa Harvard kina Chenge na wengenieo mpaka sasa limefanya nini cha maana? Mbona nchi yetu bado maskini wa kutupwa? Ingekuwa elimu ni ya muhimu hivyo basi kwa Afrika Nigeria ingekuwa kama Marekani....go figure!!!!

  Total bullshit. Nionyeshe umakini wa kuchambua mambo ulioonyeshwa na 'wasomi" walioko bungeni. Acheni dharau na hizo elimu zenu za madarasani. Hata maisha nayo ni elimu.
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Tatizo linakuja, hapa tunaongelea kuweka absolute requirements, je mtu ambaye hana formal education maana yake hana education? Je inawezekana mtu akawa hana formal education kwa sababu moja au nyingine lakini akawa na education? Hivi kuna ma prodigy wangapi, ma business tycoons wangapi wenye common sense na street smarts tu wanaoweza kufanya vitu kwa ufanisi mkubwa tu. I think we need to have more people who can see the big picture, and not necessarily technocrats, kama technocrats wabunge wanaweza kupewa staff iliyojaa technocrats. Na hata kama tunahitaji wabunge fulani wawe technocrats, certainly si lazima bunge zima lijae technocrats, tunahitaji ku balance sophistication ya technocrats na simple common sense ya watu walioelimika ka kupitia shule ya maisha, tukitaka kila mbunge awe na midigrii baadaye tutapata bunge lililojaa wasomi ambao wote wameondoka vijijini wakiwa na miaka 16 na hawajarudi tena, ameenda kuishi mijini na Ulaya, wamerudi wamekuwa wazungu weusi, ukiwauliza matatizo ya Wahadzabe wataanza kukufungulia mitabu ya wazungu wanavyosema, lakini kumbe Wahadzabe tunao hapa hapa nchini mwetu na mtu kama unawajua vizuri unaweza kujua matatizo yao bila hata ya degree.

  Ndiyo maana mimi nasema, mbunge wa darasa la saba ambaye kasha jihusisha na kutatua matatizo ya wananchi ni bora kuliko mbunge mwenye PhD ambaye anajiona ukubwa ni haki yake na vihela mnavyomlipa ni vijisenti tu, na anayeweza kuingiwa arrogance ya kuiba zaidi kwa sababu yeye msomi.

  Huwezi kuweka mtego wa panya utakaowanasa wanaotakiwa na wasiotakiwa katika hili, tuwaachie wananchi waamue wenyewe. Ama sivyo kesho tutasema wabunge lazima waweze kuongea Kiingereza etc etc.

  Upuuzi mtupu.
   
Loading...