VIVA Uda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIVA Uda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 8, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,875
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  VIVA UDA! In this day and age when private bus operators and schoolchildren appear to be at constant loggerheads, the erstwhile state-owned commuter bus company seems ever-ready to put social responsibility before outright profit, as shown here where pupils are allowed their own entrance door while other adult passengers rush for the other door. This scene was captured on camera in Tandika, Dar es Salaam early yesterday morning.
   
 2. D

  Darwin JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hizi ndio karaha zakutokua wastaarabu.

  Ukiangalia watu wanaotaka kuingia kwenye basi sio wengi ukilinganisha na ukubwa wa basi lakini watu wanagombania mlangoni.

  Kule tulikosoma ULAYA hata kama watu ni wengi kupita basi lakini utawaona wakimwacha aliye mbele aingie kwa usalama ndio wafuate nafasi zao nao wakiachwa kuingia kwa usalama.

  Itachukua muda hadi watanzania wawe wastaarabu kwenye kupanda mabasi.
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Oct 8, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hayo mabasi hayazidi 20 dar nzima huku gongola mboto liko moja tu
   
 4. D

  Darwin JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mwanzo mgumu
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Oct 8, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Heee! hivi UDA imefufuliwa au?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,875
  Trophy Points: 280
  Inaelekea hivyo Mkandara. Sikuhitaji kusoma mara mbili mbili maana hiyo rangi ya basi tu ilinihakishia kwamba hii ni 'uda mpya' kama utakumbuka ile UDA iliyokufa mabasi yake yalikuwa na rangi tofauti na hilo basi.

  Ni mategemeo yangu itapewa msaada mkubwa kutoka serikalini ili kupunguza matatizo ya usafiri Dar na matatizo yanayosababishwa na daladala katika kunyanyasa wanafunzi na kuvunja sheria za barabara kila kukicha.
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Badala ya kuwa Shirika la Umma chini ya Serikali kuu, UDA imilikiwe na Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam au iwe chini ya mkuu wa mkoa!
   
 8. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kama bado itakuwa mali ya umma itakufa tu, mafisadi watakula kila kinachokusanywa na baadaye watashindwa kujiendesha, ni vema wakafikiria kuhusu public private partinership
   
 9. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona mimi naona kitu tofauti????. naona watu kama wapo kwenye biashara ya mahindi. sioni basi lolote
   
 10. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hata mimi naona mgambo wa jiji hapa anamkwida mtu anauza mahindi....au ndio UDA lenyewe hilo?
   
 11. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  jana jioni lilikuwepo UDA hapa, si unajua basi lile labda limesogea kituo kingine ndiyo maana halionekani kwikwikwi
   
 12. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Freetown upo sawa.... naona Mkuu Bubu alighafilika kidogo manake picha zote zilikuwa kwenye Thisday (nadhani nipo sawa Mkuu Bubu).... UIle ya UDA ilikuwa up to jana na leo naona wamebadilisha wameweka hiyo ya askari wa manispaa ya Ilala wakifanya manyanyaso (oops, shughuli yao ya kunyang'anya wachuuzi vilivyo vyao)....

  Kurudi kwenye point kama Mkuu Darwin alivyosema "Mwanzo mgumu" wakuu... Kikubwa ni kuwapongeza UDA kwa jitihada wanayoonyesha katika swala la usafiri wa wanafunzi albeit difficulty situation waliyonayo kama kampuni!! Lakini unajua wao wakiweza pata mtirirko mzuri then watakuwa wameweka bench mark kwa wengine kufuata.... Hongereni sana Wakuu wa UDA na tunawatakia mafanikio....

  Wale wa madaladala, igeni mfano uliowekwa manake hata kwenu hakuna mwanga at the end of the tunel (rapid transit project na mambo ya mabasi makubwa)... lakini hamuwezi jua kama mkiiga ya UDA na ikawa na mafanikio labda SUMATRA etc wataweza buni namna ya ku-co exist nanyi mkawemo ndani.... Just a thought!

  Naomba kuwakilisha!!
   
 13. D

  Darwin JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wewe Bubu acha ujanja, hebu rejesha ile picha tuliyokua tunaongelea.

  Umetufanya tuwe wajanja sasa, siku nyingine tutazi quote post zako ili ulichoweka usibadilishe.
   
 14. D

  Darwin JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii sio picha ya jana aliyoweka Bubu
  [​IMG]
   
 15. o

  okon JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 305
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  labda picha ya basi ipo nyuma ya picha ya wakwidaji!!!! angalieni kwa makini hata darubini tumieni!
   
 16. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sawa kabisa kama mlivyosema wenzangu kwamba hakuna ustarabu wa kuingia ndani ya basi ukizingatia watu ni wachache. Lakini nimeangalia na kutafakari hasa ni kwanini imekuwa hivyo, nilichokuja kubaini ni kwamba hapo wanafunzi hawaamini kama wameachiwa huru kuingia ndani ya basi wanadhani bado wako katika mapambano na "vipanya" Students are all the time alerted.
   
 17. D

  Darwin JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huna bahati,
  Ungeona hio picha ya kwanza ungejua ninachoongea.
  Kugombea basi hata kama watu wachache na huku wakijua wataenea wote sio kwa wanafunzi tu.

  Muambia Bubu ataka kusema arejeshe ile picha utakuja kuelewa ninachosema.

  Ni tabia ambayo watanzania wameijenga sana hasa jiji la Dar.
   
Loading...