Viumbe roho havina sura maalum

Viumbe roho havina sura maalum

Sijui nimeingia huku kutafuta nini, mwee[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Mkuu Mshana jr. kwanza natanguliza samahani kwani nalohitaji unifungulie pazia japo hata kwa kifupi linahusiana na haya mambo ya roho ila langu lipo tofauti kidogo.Napia natanguliza samahani kwa wanajukwaa wote kwani jambo lenyewe kidogo linatisha.Mkuu Mshana jr.niruhusu niendelee.
 
29a1df6999ccd2df53e480f30a2f2ae2.jpg

Huu ni mjadala mmoja mpana sana ukianzia kwa Mungu mwenyewe, lakini ambaye hapa hatutamjadili yeye wala wale wasaidizi wake wanaoitwa malaika.

Hapa ni kuhusu hawa wanaosumbua uzao wa Mungu kila uchao...! Namaanisha mizimu, vinyamkera, mashetani, vibwengo, majini na majini.

Hawa ni viumbe roho hawana umbo maalum hawana sura maalum wala mwonekano rasmi! Wao huvaa umbo na sura yoyote kulingana na matakwa na mazingira husika!

65fe9ef2993ea6449f39c6c1240cbfeb.jpg

Inawezekana kabisa baadhi yetu wakauliza kuwa ni kwanini sasa kuna picha zake? Jibu ni kwamba zile ni picha za kufikirika kulingana na kile wahanga wanachokiona au kukutana nacho! Simulizi zao na kumbukumbu ya kilichowatokea.

Hivi si viumbe vyema hivyo mara nyingi hujitokeza ama kujipambanua kwa sura na mwonekano 2a kutisha na pia huja na kupotea kiasi kwamba ni ngumu kabisa kupata picha zao halisi

a8967a52032fc53467ae8bb2fe29de66.jpg

chukulia mfano wa wale wanaobanwa na majinamizi usiku kila mmoja ukimuuliza atakupa picha tofauti na hii inatokana na ukweli kwamba yale matukio yaweza kuwa si halisi bali kutokana na kumbukumbu ya matukio yasiyokamilika au viumbe roho vinavyokutokea usingizini.

Leo hii au hata sasa ukimwambia mtu nionyeshe uchawi utaishia kuonyeshwa matunguli pembe mavumba shanga nk

394d01cdeb6afb675b30f8685bfe5a88.jpg

Tumekuwa na mabishano mengi sana hapa jukwaani mengine yenye kujenga mengine yenye kuudhi nk mpaka kufikia wengine kudai ithibati lakini wakaishia kupewa darasa kwasababu ishu za kiroho hazina ithibati za kisayansi kwahiyo wanajukwaa nawaombeni sana siku nyingine tunapojadili hizi habari za kiroho hao viumbe nguvu zake nk tusiwe wagumu wa kuelewa hasa kwenye ishu za picha ushahidi mwonekano na taswira

007693699cf523174d266ea29156646b.jpg
Hivi ndugu mshana.Vinyamkela na vibwengo ndo vitu gani hv?hua napata picha ya jini,shetani na mizimu kidogo,lakini kibwengo na kinyamkela ni nini hiyo?
 
Katika threads zingine zenye uhusiano na hii hapa hapa JF tuliona kuwa mtu ni mwili jumlisha na roho (ambayo nayo kwa mawazo ya wengi ilimaanisha kuwa ni pumzi ya uhai). Na pia ilionekana kwamba mwili ni tangible and mortal (ushikika na uweza kufa na kuoza) wakati roho ni intangible and immortal (haishikiki na haiwezi kufa). Sasa kama ndivyo hivyo kwa nini hivyo viumbe vinaitwa viumbe roho wakati kwa mujibu wa mada vina umbo (i.e. tangible) ambalo wanaweza kujibadilisha kulingana na mazingira yaliyopo? Vyenyewe havifi (immortal)? Na je sisi binadamu kwa vile nasi tuna roho tuko katika kundi hilo liitwalo viumbe roho?
Hapana hapo kuna tofauti kubwa kati ya viumbe roho na viumbe hai
Viumbe roho havifi na huweza kuvaa umbo lolote lile hivi haviwezi kufa na havina umbo wala sura maalum
Viumbe hai vinaitwa hivyo kwasababu vinavaa mwili rasmi unaotambulika kama kuna uhai maana yake kuna kifo ...hivyo hivi hufa kwa maana ya kimwili
 
Mkuu Mshana jr. kwanza natanguliza samahani kwani nalohitaji unifungulie pazia japo hata kwa kifupi linahusiana na haya mambo ya roho ila langu lipo tofauti kidogo.Napia natanguliza samahani kwa wanajukwaa wote kwani jambo lenyewe kidogo linatisha.Mkuu Mshana jr.niruhusu niendelee.
Naomba kwa heshima kuu uendelee na nakuahidi sitakwazika kwa lolote lile bali nitajitahidi kwa uelewa Wangu kukujibu..! KARIBU...!!!
 
Hapana hapo kuna tofauti kubwa kati ya viumbe roho na viumbe hai
Viumbe roho havifi na huweza kuvaa umbo lolote lile hivi haviwezi kufa na havina umbo wala sura maalum
Viumbe hai vinaitwa hivyo kwasababu vinavaa mwili rasmi unaotambulika kama kuna uhai maana yake kuna kifo ...hivyo hivi hufa kwa maana ya kimwili
Lakini kama viumbe roho havifi ina maana vina uhai. Kwa hiyo navyo vinaweza kuitwa viumbe hai kama ilivyo kwa binadamu ambao uitwa viumbe hai?
 
Hivi ndugu mshana.Vinyamkela na vibwengo ndo vitu gani hv?hua napata picha ya jini,shetani na mizimu kidogo,lakini kibwengo na kinyamkela ni nini hiyo?
Hivyo ni uzao mmoja sawa unapozungumzia kenge na mamba au tunapozungumzia mammals kwenye biology kwamba eti hata popo ni mammal sawa na binadamu
 
Lakini kama viumbe roho havifi ina maana vina uhai. Kwa hiyo navyo vinaweza kuitwa viumbe hai kama ilivyo kwa binadamu ambao uitwa viumbe hai?
Bado kuna tofauti
Hivi vinaitwa viumbe roho kwakuwa havina umbo rasmi..! Hizi ni roho
Vile vinaitwa viumbe hai kwakuwa vinavaa mwili rasmi uharibikao na kuna siku hukoma kuwa hai kwa maana ya roho kujitenga nao
 
Back
Top Bottom