Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,676
- 729,841
Huu ni mjadala mmoja mpana sana ukianzia kwa Mungu mwenyewe, lakini ambaye hapa hatutamjadili yeye wala wale wasaidizi wake wanaoitwa malaika.
Hapa ni kuhusu hawa wanaosumbua uzao wa Mungu kila uchao...! Namaanisha mizimu, vinyamkera, mashetani, vibwengo, majini na majini.
Hawa ni viumbe roho hawana umbo maalum hawana sura maalum wala mwonekano rasmi! Wao huvaa umbo na sura yoyote kulingana na matakwa na mazingira husika!
Inawezekana kabisa baadhi yetu wakauliza kuwa ni kwanini sasa kuna picha zake? Jibu ni kwamba zile ni picha za kufikirika kulingana na kile wahanga wanachokiona au kukutana nacho! Simulizi zao na kumbukumbu ya kilichowatokea.
Hivi si viumbe vyema hivyo mara nyingi hujitokeza ama kujipambanua kwa sura na mwonekano 2a kutisha na pia huja na kupotea kiasi kwamba ni ngumu kabisa kupata picha zao halisi
chukulia mfano wa wale wanaobanwa na majinamizi usiku kila mmoja ukimuuliza atakupa picha tofauti na hii inatokana na ukweli kwamba yale matukio yaweza kuwa si halisi bali kutokana na kumbukumbu ya matukio yasiyokamilika au viumbe roho vinavyokutokea usingizini.
Leo hii au hata sasa ukimwambia mtu nionyeshe uchawi utaishia kuonyeshwa matunguli pembe mavumba shanga nk
Tumekuwa na mabishano mengi sana hapa jukwaani mengine yenye kujenga mengine yenye kuudhi nk mpaka kufikia wengine kudai ithibati lakini wakaishia kupewa darasa kwasababu ishu za kiroho hazina ithibati za kisayansi kwahiyo wanajukwaa nawaombeni sana siku nyingine tunapojadili hizi habari za kiroho hao viumbe nguvu zake nk tusiwe wagumu wa kuelewa hasa kwenye ishu za picha ushahidi mwonekano na taswira