Mafuta si kwetu tu hata depot ya BP hakuna na ndio sababu unaona tunauza dizeli na mafuta ya taa pekee, alisema mfanyakazi wa Kituo cha BP Fire. Wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wamedai mahitaji ya petroli nchini ni makubwa kuliko dizeli na mafuta ya taa na ndiyo sababu yanamalizika mapema.
Kama ni kweli haya ndio yanaendelea, serikali inayowajibu wa kukagua hifadhi zao zote za mafuta kijiridhisha kwamba mafuta yapo ila wamekataa kuyauza then wawafungulie kesi ya kuhujumu uchumi. Kama hawakuridhika kushushwa kwa bei wangetoa tamko rasmi kwamba hawatauza mafuta na si vinginevyo.
The act mount to econominc sabboutage(spelling haziko sawa) maana wamekataa kwa makusudi ili kucreate demand kubwa na kuuza mafuta kwa bei ya juu.
SHYLOCK HAWA WASHUGHULIKIWE MARA MOJA.
NAKUBALI hoja ya kutaifisha KAMPUNI ZA MAFUTA NA BIASHARA ya usafishaji mafuta nchini.
Zanzibar wanaweza kuanza kwa kujgena kituo cha usafishaji mafuta Pemba na kununua meli moja ya kubeba mafuta na hivyo kuifanya biashara hiyo ya serikali peke yake.
Hapa Bara tuanze kwa kutaifisha OILCOM ambao ndio wanaonesha jeuri na kiburi zaidi na wanaoongoza mgomo wa vituo vya peteroli unaoendelea kote hapa jijini Dar es salaam.
Serikali isifanye mzaha na kina SHYLOCK HAWA -WASHUGHULIKIE mara moja na wasidhani serikali ya Kikwete ni serikali ya kukokotwa na kuburuzwa na kila mwenye kutaka kudhulumu haki za wengine eti!
Mkuu PM,
Binafsi nimeshangazwa SANA na jambo hili na kujiuliza HIVI TUNAYO SERIKALI KWELI? Nafikia wakati nakata tamaa kabisa.
Issue behind vituo vya mafuta wasibambikizwe wahindi etc, wazalendo wengi tena wanasiasa wanamiliki vituo hivyo kwa migongo ya waarab 'wachukua kamisheni' tu.
Hakuna udhibiti wa soko huria Bongo? Pia siwalaumu wafanyabiashara pekee, nawabebesha lawama zaidi EWURA. Inaelekea hawajui walitendalo, maamuzi yalikuwa ya kukurupuka? Kwa manufaa ya nani? Athari ya hali hii ni kubwa sana kwa uchumi wa taifa. Kifupi ni uhujumu uchumi wa taifa kwa kiwango kikubwa sana. Inasikitisha SANA
Makosa kama haya (price fixing) kwa nchi zilizoendelea ni hatia kubwa sana, sijajua sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu hili.
Duuh! Lakini vituo vya SHELL si viko vichache sana kwa Dar?! Kama SHELL wamegoma nafikiri hizo kampuni nyingine kama BP, Agip, GAPCO, TIOT, Caltex, Total, na nyinginezo nyingi tu zinaweza kukidhi mahitaji. Au hapa ulimaanisha SHELI = ANY FILLING STATION??!!
Nimezungumza na mnene mmoja wa GAPCO amenithinitishia kuwa kuna stock ya kutosha ya mafuta katika depot za makampuni yote makubwa. Anasema hata wao (waagizaji) wameshangazwa na kukosekana kwa petroli wakati ipo ya kutosha kwenye stock zao. Wanahisi kuwa huenda it was a case of bad timing on part of retailers ambao walishindwa kuagiza kiasi cha kutosha kuhimili mahitaji wakati wa weekend iliyopita. Lakini amenihakikishia kuwa hakuna haja ya ku-panic kwa sababu mafuta yapo ya kutosha na yameshaanza kusambazwa
Una hisa katika hayo makampuni ya mafuta?
hizo indicative prices unazodai zipo chini una theory gani ya kusupport ur argument?
Mkulu nakuheshimu....
- Mkuu wangu uko karibu sana na ukweli, price fixing inatokea tu kunapokuwa na kampuni moja kuruhusiwa na serikali kuwa na nguvu kubwa ya umiliki wa bidhaa flani bila kuwa na sheria za kutosha kuhakikisha competition katika biashara ya ile bidhaa, hili tatizo lipo kwenye makampuni ya simu Tanzania pia,
- Ukisoma vizuri hoja nyingi kwenye hii thread utagundua kuwa this ishu is too complicated kwetu wananchi, ndio maana hata serikali haina clue on it! I mean kuna mpaka wananchi wanaoshauri serikali ijiingize kwenye biashara ya mafuta!
Sikubaliani na huyo mnene kusema kuwa bad timing ya hao wauzaji, kama ingekuwa kituo kimoja au hata vitatu lakini kwa vituo vingi kwenye maeneo mengi siyo bad timing, nafikiri wanataka ku create scarcity ili wapandishe bei kwa theory ya demand and supply. Hapa Serikali iingilie kati kuondoa tatizo hili na lisirudiwe tena huko siku za mbele. Tulizoe uhaba wa mafuta katika utawala wa awamu ya kwanza lakini tangu awamu ya pili mpaka hii leo tumesahau kabisa matatizo kama haya tunaomba wahusika wayashughulikie kwa nguvu zote.
Mzee niliandika kuwa sorce ni michuzi. Nili-copy na ku-paste. Anyway, TZ Sheli = filling station; Colgate = Tooth Paste; Kiwi = Shoe polish, you name it, bora Kiswanglish kinapanda. Kama hujui hivyo kiswanglish tembelea michuzi blog utakumbana nayo at MICHUZI