Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Pale shule ya msingi kinondoni
Kulikuwa na Walimu wanaitwa
Mwl. Simbani Na Mwl. Shuma..
Ikitokea wametoa adhabu kwa wanafunzi wanaotokea Mitaa ya Msisiri B
Maeneo Ya One Nil Area Nondo na Jerusa.. au Around Mwananyamala Hospitali..
Walimu walikuwa wanabadili njia kurudi makwao..
Shuma alikuwa anakaa Mitaa ya Ujiji
Simbani Tandale
Walikuwa hawakatizi njia ya msisiri B kupitia Kamanyola..
Maana walikuwa wanaogopa kufanyiziwa...
Mkuu nimeku PM mda tu...fanya uje
 
Kuna siku walikuja bongo movie mitaa ya makaburin pale sikumbuki vizur ila chuchu hans na cloud nais walikuwepo na kivits cha pink hivi wakaenda kufanya shooting ktk ya makaburi wazawa wakapata fursa kwanza wakafatwa wakaulizwa nani kawambia hapa ndio location? Aliyewapa idhini ya kupiga picha makaburi ya watu nin nani dah wakachanganyikiwa pale huku wandewa wameizunguka vits powerwindo, redio, taa za nyuma zikaondoka...wale wasanii wakaomba msamaha pale wakasema wanafata kibali kumbe ile kuwauliza uliza ilikuwa kuwazuga tu kule vijana wanifanyia kazi vits
 
Bigwa nae mkubali Jamaa anaitwa mchafu anakopi nyingi mzee wa kutoa mkwaju
Mchafu anaweza kuja kijiweni kwenu kavalia kofia kubwa IPI msimtambue halafu anasema 5000 kwa 5000 kuzuia goli ktk michezo mitatu. Yule jmaa katembea mpka vijijini wanamjua hilo jina kawala sana watu pesa kuzui goli
 
Mchafu anaweza kuja kijiweni kwenu kavalia kofia kubwa IPI msimtambue halafu anasema 5000 kwa 5000 kuzuia goli ktk michezo mitatu. Yule jmaa katembea mpka vijijini wanamjua hilo jina kawala sana watu pesa kuzui goli
Kweli kamanda ila kavuta kama miezi 3 hivi nakubali kuliko hata mangezi akiwa Na arosto ya fegi hata ukiweka jero anapitia
 
umesahau na Nyarugusu f.c, siku ikipigwa game kagera ranger vs nyaragusu, uwanja wa makurumla hakukaliki, nimesoma karume pr, kitaa kagera mikoroshini
nakumbuka
MZEE KINESI alikuwa analoga sana kipindi cha pili mpira uvunjike mechi irudiwe aingize ela
nakumbuka Mechi flani ABAJARO na KAGERA kma sikosei mpira suluhu kupiga penart hataki anadai eti muda umeisha giza kumbe ana lolote anataka mechi irudiwe apate ela
ABAJARO watoto wa sinza walikuwa wanajifanya wanaela sana wamechukua kombe la kinesi wakaleta MZIKI na Solothangs akawa ndo anaimba
 
Bila kumsahau mtuma salamu maarufu na mshiriki wa kipindi cha chemsha bongo...Mohamed Kiyaiyai..mzee wa niambrieeeee...kutoka KomaKoma .
Huyu alikuwa anazinguana sana na Misanya Bingi...yaani akipiga simu anaanza kutaja washikaji walioko pembeni yake kama kumi hivi halafu ndio aanze kuwatumia salamu watu watatu...yaani ndani ya sekunde 60 anakuwa keshatuma salamu kwa watu zaidi ya 15 hivi....Misanya Bingi alimshtukia akawa anamgongea kipusa na kumkata hewani.
Halafu misanya alikuwa anamkomesha kwa kugonga kipusa kama dakika moja hivi...yaani ukitafsiri ni kama vile alikuwa anamporomoshea mitusi kwake na kwa ndugu na masela wake.

Yaani huu utundu wa wabongo ungekuwa ni wa kutengeneza vyombo vya anga mwezini tungekuwa tushahamia.
niambrieeee hiyo sio ya watoto wa vingunguti hao timbereeeeend kwa kina makala hiyo mdogo wake mamaasakina na mshikaji fulani hivi mdau sana wa twanga
kiyaiyai yeye swaga yake ndo hiyo sekunde kumi tu kashataja watu 10 kwa uwiano wa sekunde 1 jamaa noma sana
 
Tulikuwa tunapiga sana msuli kipindi kile kuna alqed ya kina sadalah,lijoh,loko,chiundo, nk na ile ya kina kawale,mkute,chozi, nk
mimi nilikuwa ile ya kina kawale FARIDA chozi nk kwa ticha MAIKO pale CCM UJIJI tulikuwa na kina ROGERS wa shule ya kisiwani na wenzake ila kuna nyingne ya mr. k alikuwa anakaa kwa MZEE DIZAMIRE pale msikiti wa malamala karibu na luku ila yeye alikuwa anajua sana MATH
 
Pale maeneo ya msufini palikuwa na uwanja mkubwa sana unatumika ktk maswala mbali mbali km siasa, maulid ( madras)...jioni unakuta kuna cha ndimu gemu za ligi ya mbuzi unakuta vibinti micharuko na wakina mama na watoto mgongoni unasikia "usiniumizie uyoooo" hizo ligi wanacheza watu na ndevu zao ila mpira wa cha ndimu (sio gozi) hapa ndio alipotokea bondia CHEKA alikuwa golikipa kipaji chake cha ngumu kilikuja kuoneka kinondoni mahakamani(kambangwa) kuna kitu kinaitwa MTU BEE....gemu zikiisha huo uwanja unageuka sehem ya biashara samaki, vitumbua, chai n.k....biashara zikimalizia wanaingia wazee wa kazi NGETA hapo kuna kila aina ya wizi usije kukatisha eneo ilo msufini kuanzia saa tano usku UMEKWISHA
Jamaa yangu walikuwa pamoja na kina Cheka kinondoni.
 
Back
Top Bottom