Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Nimepitia comments nyingi zinaonyesha m'nyamala ilikuwa pasua kichwa enzi hizo. Mliokuwepo enzi hizo hebu mtutoe tongotongo je m'nyamala ilikuwa sehemu balaa zaidi kuliko maeneo kama magomeni, keko au ubungo?

Maana nimewahi kusikia maeneo haya (magomeni, keko na ubungo) yalikuwa na balaa nyingi zikifanywa huko.
Keko kuna balaa toka enzi na enzi mpaka kesho ,keko usiende kuishi kila aina ya usela uko huko ,mchana kweupe unakabwa na watu wanaendelea na shughuli zao ,kijana wa miaka 16 anakushikia panga mchana,keko pasua kichwa watoto na watu wa huko wameshindikana ....keko kuna story tamu hope Uzi wake utafunguliwa

Magomeni pako poa sio kihivyo ,magomeni kagera mpaka Argentina hupenda sana michezo ya ngumi na vijana wengi wameingia huko ndio kwakina Thomas mashali huko kila mtu anajifanyia bondia

Mwembechai,mikumi,mapipa palikuwa hot lkn sio kama keko,mwananyamala,kigogo nk ..binafsi ni mzoefu wa magomeni mapipa mitaa ya suna huku ukitaka druglords ,watengeneza hela feki utawapata ,matapeli ,watoto wa mjini utawapata mpaka watoto waliosumbua miaka ya 2014,2015 kwa jina la panya road utawapata wakazi wa kinondoni wanawafahamu sana hawa

Ila kigogo,keko,Tandale ndio yanashabihiana na mwananyamala ..magomeni utundu upo ila maisha ya huku yapo medium kati kwa kati ndio maana kuna utofauti na mitaa tajwa hapo juu hivyo usela sio sana kama huko ila pachangamfu

Nimepitia comments nyingi zinaonyesha m'nyamala ilikuwa pasua kichwa enzi hizo. Mliokuwepo enzi hizo hebu mtutoe tongotongo je m'nyamala ilikuwa sehemu balaa zaidi kuliko maeneo kama magomeni, keko au ubungo?

Maana nimewahi kusikia maeneo haya (magomeni, keko na ubungo) yalikuwa na balaa nyingi zikifanywa huko.
 
safi sana mkuu,kipindi nchi ina adabu starehe zote zilikuwa maeneo hayo,unaruka zako pambamoto pale vijana,na taratibu unatembea kwa miguu hadi pale Mwananyamala A ,huguswi na mtu yeyote pia nakumbuka michezo iliyokuwa inaandaliwa na club ya Lucky Rangers na wachezaji wengi maarufu walikuwa wanacheza pale,vile vile Mwananyamala hii yalikuwa makazi ya yule mtabiri maarufu VULATA!!!
 
Wakuu ile Sunrise bar siku hizi imekua Kanisa watu wanafanya ibada kila siku.
Halafu nilikua nikienda kupiga zoezi pale uwanja wa Mwananyamala B nakuta kuna zile nguzo kama za uwanja wa Chamazi Complex. Hivi zamani palikuaga na mataa ya mechi za usiku???
Ndiyo watu walikua wanacheza hadi usiku.
 
Unamkumbuka Mzee Ndevu?Mwanae alikufa akijidunga madawa?Maiti ikakutwa na sindano yenye madawa kwenye uume,maana aljidunga sehemu za mwili mpaka mishipa yote ikapotea,akaanza kujidunga kwenye uume
Dah umenikumbusha mbali tena... Namfahamu vizuri aisee
 
...
Mwembechai,mikumi,mapipa palikuwa hot lkn sio kama keko,mwananyamala,kigogo nk ..binafsi ni mzoefu wa magomeni mapipa mitaa ya suna huku ukitaka druglords ,watengeneza hela feki utawapata ,matapeli ,watoto wa mjini utawapata mpaka watoto waliosumbua miaka ya 2014,2015 kwa jina la panya road utawapata wakazi wa kinondoni wanawafahamu sana hawa
Hao panya road walipoanza kusumbua hadi yule mtangazaji akajificha chini ya uvungu wa gari nikapigiwa simu bwana njoo tunasikia panya road watakuja Mwananyamala.

Nikatoka zangu huko nilipo hadi Mwananyamala, tukakusanyana uwanja wa Sparta maarufu kama Makaburini, yaani pale ilikua unaenda kama ulivyo ukifika unakabidhiwa silaha.

Wale wadogo tukasikia wapo eneo linaitwa Peace, tukaanza kuwafuata, tunafika tunaambiwa bwana wameelekea juu kama wanayafuata magenge. Tukasema kama wameiacha kwa kopa basi waende wanapoenda.

Siku kadhaa mbele nasoma kwenye gazeto eti serikali imetenga zaidi ya bilioni moja kupambana na panya road
 
Haha dah inatenga billion kwaajili ya panyaroad vitoto vile

Wale madogo ilikuwa mmoja wao akiuliwa na wananchi wanakusanyika na kwenda kuvamia na kufanya fujo na uzuri wana ushirikiano sana sababu wanajuana kwakuwa wanatembeleana maskani kupiga stori na mambo mengine ,watu wa kinondoni walisema mtoto yeyote wa magomeni suna akionekana kino anapigwa sababu vijana wa huku wengi wagomvi na kwenye vigodoro vya usiku huko kinondoni hufanya fujo na kuiba sasa wakapiga biti yeyote wa magomeni suna akionekana Moscow apigwe sasa kuna dogo wa huku ila wana camp yao wanajiita al shababi alipita huko alivyoonekana watu wakaitana na kumchapa kama mwizi vile dogo akalazwa hospitali ya mwananyamala sasa taarifa wakapewa wenzake kuwa Fulani kapigwa na watu wa kinondoni ..huku kuna makundi 2 al shababi na watoto wa chawa ambao ni pasua kichwa ndio panya road wenyewe plus wakaitwa watoto wa maskani za kigogo,tandale wakakutania huku mtaani ..ukiona wamevalia vipensi vya jinsi wote ,kofia za pama na wengine bagalashia na panga kiunoni na tembea yao utacheka wakakusanyika na kuelekea kinondoni sie tulikuwa tunawachora tu na kusema leo tusubiri taarifa ya habari tuone yatakayojiri nasikia ndani ya dakika watu wote walijifungia ndani walisafisha mitaa yote ya kinondoni kimya wakawa wanaingia wanapouza chips kwenye droo wanachukua pesa wakaelekea huko juu kabisa mwananyamala ,sasa hawa madogo wanakusanyika wa tandale na sehemu nyingi sasa wa tandale wanapita mwananyamala kuelekea kwao wa migo wanarudi migo nk na wakikutana watu huko njiani wanawaibia nk

Sema uoga wa watu tu ila madogo wanakuwa washapuliza bangi wengine Valium hivyo huwaelezi chochote ,badala ya kusikitika inabidi ucheke kuanzia kinondoni, mwananyamala wanasafishwa na vijana wale tena sio wengi kivile watu wanakimbia kimbia na kujifungia

Hao panya road walipoanza kusumbua hadi yule mtangazaji akajificha chini ya uvungu wa gari nikapigiwa simu bwana njoo tunasikia panya road watakuja Mwananyamala.

Nikatoka zangu huko nilipo hadi Mwananyamala, tukakusanyana uwanja wa Sparta maarufu kama Makaburini, yaani pale ilikua unaenda kama ulivyo ukifika unakabidhiwa silaha.

Wale wadogo tukasikia wapo eneo linaitwa Peace, tukaanza kuwafuata, tunafika tunaambiwa bwana wameelekea juu kama wanayafuata magenge. Tukasema kama wameiacha kwa kopa basi waende wanapoenda.

Siku kadhaa mbele nasoma kwenye gazeto eti serikali imetenga zaidi ya bilioni moja kupambana na panya road
 
Iko mwishoni kabisa mwa soko kuna uchochoro mtu akipita hapo hajulikani anaenda gesti au anataka kutokea upande wa pili... Nyingine ilikuwa pale Barabarani kabisa

Kuna jamaa mmoja sasa hivi mkubwa tu ktk awamu hii ya 5 alikuwa anadate mdada wa mitaa ya kwetu sijui mwenyewe alikuwa anaishi wapi kipndi icho kuna siku wamechil uwanjani na yule mdada pale uwanja wa sparta usk km saa tatu wanashikana shikana tukawafata "tukamuliza nani amekupa ruksa ya kukaa eneo ili mda huu? Na unafanya nini hapa Jamaa akawa mnyonge ruka kichurachura akaruka pale akaomba tumuache maana ana mke na watoto akalipa elfu 80 na simu akatoa line simens dole gumba ila alivyoondoka akugeuka nyuma..now yupo kwa JPM huko ila mwanyamala anaijua vizur
 
Back
Top Bottom