Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Messenger RNA

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,102
3,022
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Vijana tunapitia mengi ya kukatisha tamaa, lakini leo niwape machache ya vituko vya sahili nilivyowahi kuviona kwa macho yangu.

1. Tuliitwa kwenye usahili mikoa ya nyanda za juu kusini, basi kwa furaha na kujiamini nikapaki vitu huyooo nikafika siku moja kabla nikaripoti na nikakuta watu wengine, siku ya pili yake tukawahi sana tu,basi wakati tunaendelea kusubili wasahili wakafika na gari aina ya cruiser wakashuka kama saba hivi, sisi tukajua wote ni wasahili, lahaula kumbe wengine ni wasahiliwa kama sisi na tuligundua baada ya kuona wanakuja kukaa kwa wasahiliwa. Baada ya usahili matokeo nakuachia utabiri mwenyewe.

2. Tuliitwa kwenye usahili wa serikali basi wakati tunaendelea kusahiliwa basi kuna kijana sijui wa mkubwa gani akawa ameondoka eneo lile, basi unaambiwa alitafutwa balaa na mwisho wa siku matokeo yumo.

3. Kuna siku tunasubiri usahili, kuna vijana wakawa wanasema wameagizwa kuja hapo kama utani vile, aisee haikuwa utani matokeo yalitujulisha.

4. Tumefanya usahili, matokeo watu ambao hawakuwepo kwenye usahili ndio waajiliwa.

5.Umetoka umejiandaa na kile ulichosomea mfano mechanical engineering na vile vitu vinavyoendana na umejiandaa haswaa,unaingia wanaanza kukuzodoa,mara huyu aulize mambo ya demokrasi yaani ni ujinga tuu maadamu wakukere tu maana hawana mpango na wewe ni vile umekuja acha wapoteze tu muda, inakera acha tu.

Dah mambo ni mengi sana, ushauri wangu vijana msio na connection mkaze sana na kumuomba Mungu, lakini naamini kila kitu kinawezekana.

Kama una kisa ni ruhusa kuweka.
 
Dah mkuu inaonesha maisha yako ni interview tu mwanzo mwisho

Nimemaliza zangu fom foo 2012

Interview ya jeshi nilienda tukawa tunaitwa kwa makundi sasa kufika pale tunajiandaa kwa maswali (maana tulijinoa kweli kweli) nashangaa tunaulizwa tarehe za kuzaliwa huwezi amini tuliambiwa maneno makavu pale kila mmoja... binafsi niliambiwa umri umezidi siku 3 wengine mpaka siku moja

Ikawa kazi ni hiyo kila kundi linaloitwa mnapewa maneno hayo ya kukatisha tamaa mnaambiwa mkatafute shughuli ya kufanya au fani ya kusomea (ikumbukwe wale watu wao waliowakusudia walishaitwa mwanzo na maswali ya ki interview wakaulizwa)
 
Pilot
Aircraft engineer
Marine and nautical engineer
Drilling Engineer
Well completion engineer
Fishing engineer
Mining Engineer
Robotic and Automation engineer.
Cyber security expert.
Software developer.
Artificial Intelligence expert.
Reliability and Mechanical Engineer.
ROV operator.
Automation engineer.
Instrumentatio engineer
Electric Engineer.
Mechanical Engineer.
Civil Engineer
nk, nk, nk.

Taifa halitoi direction kwa vijana wasome nini, matokeo yake vijana huishia kutia huruma na kunyenyekea wapumbavu.
 
Kuna haja ya serikali kuboresha mfumo wa elimu ili watu wasome vitu watakavyoweza vifanyia kazi hata kama wasipopata ajira.
 
Mimi nakumbuka mwaka 2009 nilienda kufanya interviewe kwa ajili ya kujiunga na jeshi la magereza, basi bwana mtoto wa bwana jela alikuwa anaitwa tobby sasa sijui tobby alipoenda kula chakula cha mchana akapitiwa na usingizi?🤔🤔🤔 Interview haikufanyika mpaka mtoto tobby alipopatikana.
 
Nilienda njombe interview za Tanroad weight brigde operator

Matokeo hayakubadikwa wakapigiana simu usiku, asubuhi na mapema wakaitana usaili wa oral

Vijana tusikate tamaa
Mimi nakumbuka mwaka 2009 nilienda kufanya interviewe kwa ajili ya kujiunga na jeshi la magereza....basi bwana ..mtoto wa bwana jela alikuwa anaitwa tobby sasa sijui tobby alipoenda kula chakula cha mchana akapitiwa na usingizi?..........interview haikufanyika mpaka mtoto tobby alipopatikana.......
 
ila kuna michezo ya kipuuzi na kishamba mno huwa wanaifanya mibuyu ya baadhi ya wasailiwa.

wewe unajua kabisa huyu ntambeba na atapita,kwanini kila mtu aone na ajue hilo!!!unakuta jitu linashuka kwenye gari la moja ya maboss wa usaili,sijui ndio kuvimba au ufala tu!!!

wahi mapema kaa na wenzako kule chini ya mti,mambo mengine niachie mimi.mnavuruga watu kisaikolojia tu.

2011 tunafanya interviw wilaya fulani,nafasi zetu wavulama walihitajika 12,wasichana 2.
tulifika kwenye interview tuko kama 60 hivi na wanawake kama 6 hivi,pigwa dana dana ya kwenda na kurudi kama miezi 2 hivi bila interview,siku inakuja kufanyika,wanatokea wanawake wawili ambao hatujawahi kuwaona na ndio hao wanachukuliwa,moja lilitoka kwa dc nadhani alikuwa analila.

mmoja kati ya wale mabinti tuliokuwa tunakuja naye alilia sana,mpak tukakusanyana kumbembeleza yaani,dah.
 
Wangekuwa wanaacha kusumbua watu,unakuta mtu ameazima nauli au kapewa na mama yake maskini ili akomboe familia matokeo ni kuwa anaona kabisa wanaopewa kazi ni wale ambao hata usaili hawakufanya,inauma sana.
 
Za juzi juzi tu hapa sensa pale kinyerezi.

Walioitwa zaidi ya elfu moja. Interview ilifanyika siku mbili. Jana matokeo yanatoka wasimamizi wa maudhui nafasi 5 na teham 1 tu

Screenshot_20220728-084838.png
 
Poleni mno generation hii, mtaumia sana na dawa ni kupanua wigo wa kuhangaika, kipindi cha nchi Ina heshima na adabu kulifanyika interview ya vijana kwenda kujifunza urubani wa ndege za jeshi na ufundi (601 na 603 KJ),waliletwa wataalamu kutoka China waendeshe hii interview, ilikua fair na kuhuzinisha kama hukupita hata awamu ya kwanza, urefu na wengi waliishia pale ,na looo pia walichunguza kwa maumba kama ulishatembelewa!!kwenye tigo jamani tumepitia mengi hapa duniani
 
Pole kwa kuliwa tigo mkuu....uache ufara..
 
Dah mkuu inaonesha maisha yako ni interview tu mwanzo mwisho

Nimemaliza zangu fom foo 2012

Interview ya jeshi nilienda tukawa tunaitwa kwa makundi sasa kufika pale tunajiandaa kwa maswali (maana tulijinoa kweli kweli) nashangaa tunaulizwa tarehe za kuzaliwa huwezi amini tuliambiwa maneno makavu pale kila mmoja... binafsi niliambiwa umri umezidi siku 3 wengine mpaka siku moja

Ikawa kazi ni hiyo kila kundi linaloitwa mnapewa maneno hayo ya kukatisha tamaa mnaambiwa mkatafute shughuli ya kufanya au fani ya kusomea (ikumbukwe wale watu wao waliowakusudia walishaitwa mwanzo na maswali ya ki interview wakaulizwa)
:D:D jamaa yangu mmoja alienda kufanya usahili wa Polisi,aliambiwa wewe form 6 mzima unataka nafasi ya Polisi,hatutaki wasomi sisi
 
Back
Top Bottom