Vituko na vioja vya wadada wa benki

Pamoja na huduma mbovu za baadhi ya wafanyakazi wa benki labda wateja wengine nao wana matatizo. Au wengine mnaenda benki tofauti kila siku?
Benki yako(yaani una akaunti hapo muda mrefu) lazima utakuwa unajulikana na wahudumu wengi tu na mnaweza kuwa marafiki kitu ambacho kitakusaidia kupata huduma nzuri ambayo unastahili kuipata hata ukiwa huna rafiki.
Mimi ninapo-bank nawajua wahudumu wote hadi branch manager kwa sababu hii labda ndio maana napata first class service,wafanyakazi wote wa bank hadi walinzi wa security company wananifahamu na ni 'marafiki'
Habari ya kuibiwa hela na teller ukishafahamiana na hawa watu haipo,tena muda mwingine unakuta foleni kubwa au system down unamuachia hela anakugongea tu muhuri system ikiwa fresh anamalizia transaction.
Tuwaheshimu wengine na sisi watatuheshimu.
Huyo ni yule anaepanga foleni masaa mawili kudiposit 10,000 wakati kuna wakala kibao mtaani kwake
 
Sasa unafikiri kila mtu ana muda wa "kufahamiana" na mtoa huduma wa ofisi wa kila taasisi anayopita? Wengine muda ni mali na tunazo ofisi zetu pia nazo zina viyoyozi kama za hao bank tellers wenye nyodo na hata kama hazina viyoyozi zinalipa vyema kuliko visenti vyao uchwara na bado tunawaletea biashara na hatuna nyodo. By the way ni miongozo ya bank gani inaagiza ili upate huduma nzuri (ambayo ni haki yako) ni lazima uwe na urafiki na hao mahousegirl wao (bank tellers sijui)? Nakosa muda hata wa kumpigia mama mzazi nianze kupoteza muda kujipendekeza kwa KIMA ambaye hana adabu na bila mimi hana sababu ya kuwepo hapo alipo? Wajiheshimu na kuheshimu wateja bhana, heshima kitu cha bure na kwenye kazi kama zao ni kitu cha LAZIMA hata kama ana ugomvi na bwana wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Go back and read what I wrote again.
 
Hahah...unachosema ni kweli kabisa. hata mimi ndo utaratibu wangu. kila Bank ninayoenda lazima ni-recruit marafiki na tips za hapa na pale. yaani kama naenda Bank nampigia simu ananijazia bank slip na mimi naenda kumalizia signature. mpaka branch manager wanakuwa washikaji kwani nilikuwa nawatoa tips. sometimes nilikuwa nampigia manager achukue hela kwenye A/C yangu ampe teller aniletee ofisini......ukiwajuana na watu raha sana...
Sasa ajabu humu mtu anafiki ukienda pale unapoteza muda kutafuta marafiki kumbe inakuja automatically kwasababu unaenda mara kwa mara na watu ni wale wale. Mimi almost tellers wote na bank manager wananijua jina,ila mimi namjus jina mmoja tu.
 
Sasa ajabu humu mtu anafiki ukienda pale unapoteza muda kutafuta marafiki kumbe inakuja automatically kwasababu unaenda mara kwa mara na watu ni wale wale. Mimi almost tellers wote na bank manager wananijua jina,ila mimi namjus jina mmoja tu.
Kufahamiana na watu muhimu sana. kuanzia Bank, Police, Mahakamani na Hospitalini. ukiweza kutengeneza network kwenye taasisi hizo zote...unakuwa salama bin salimin...
 
Wahurumieni tu, wakati mwingine wanakuwa washaingiziwa mishedede na vitu vimetuama kunako

time will tell
 
Sasa mpaka ufahamike ndio upatiwe heshima yako ! Hii haijakaa sawa
Mkuu kufahamiana huku kunakuja na mazoea ya kuonana kila siku na mutual respect. Kuna watu wana nyodo nafikiri umesoma comments humu na ha hao tellers ni binadamu ukiwaletea nyodo nao wanakupotezea tu. Kuwa friendly uone kama watakusumbua. Tumia same technic hata kwa traffic police nakuhakikishia fine utazisikia tu, be friendly.
 
Sijuwi tuanzie wapi?! Kucheza na simu wakati uko kwenye Queue, kujifanya wako busy kwenye PC kumbe wana browse tu au kucheza games, kujizungusha zungusha bila kujali wateja wanasubiri huduma, kuwaongelesha wenzao wakati wanahudumia wateja, majibu yasiyotosheleza sababu wengi hawana vyeti wala kupewa mafunzo ya kibenki, kila kazi ni pole pole kuliko konokono, ni shida kwa kweli, mie bado nina uhakika wengi wao wamesaidiwa tu, kama ndugu, rushwa, rushwa ya K, n.k. Bure kabisa...
 
mbona kuna dada crdb mtwara mchaga hivi mweupe ni tellers,she is so kind and honest yaani ni mdada poa sana
 
Back
Top Bottom