Visa na mikasa mbalimbali vya jamaa zangu hawa wachimbaji, leo tulikuwa tunapiga ma'story daah! Wanaume tunapitia mengi sana

minja mgumu

JF-Expert Member
May 9, 2017
204
308
Habari za jioni ndugu zangu nimekaa nikaona tushee kidogo uzoefu mbalimbali ktk utafutaji wa maisha yaweza ikawa shule nyingine bila kujua inaweza kuja kusaidia wengine.

Leo bhana nilikuwa napiga ma'story na Jamaa zangu hawa wachimbaji mmoja akaleta story yake bhana ya kusaka utajiri sasa walikuwa wawili wakafika kwa Mtaalam, walipofika wakakuta watu wengi pale kwa Mtaalam sasa wakati wamefika wakawa wanawauliza waliowakuta pale eti vipi? Mtaalam amewatoa watu au ndo zile za kuvuma halafu mara paap unapolola vyote yule mwenyeji akamjibu ukifuata masharti unafanikiwa cha msingi uwe na moyo mgumu,Jamaa sasa akasema sawa.

Wakalala pale kesho yake wakaenda kuonana na Mtaalam mida ya saa 7 mchana yule Mtaalam akasema ingieni wakaingia mjengoni anasema ktk vile viti aina ya vigoda vilikuwa na ngozi kama ya mtu si mtu wakakaa baada ya dk kama 5 ukimya ukitawala mtaalam akasema mtaweza mnachokitafuta, wakasema tumedhamiria hili babu tumechoshwa na umasikini wetu.

Babu akasema lakini mioyo yenu mbona ya kike mtaweza kweli...?wakadakia babu sisi tumeamua wenyewe tuko tayaribkwa lolote. Sasa yule babu akawaambia watoke nje kidogo halafu atakapoita aingie mmoja atamalizana naye halafu akitoka ataingia mwingine. Wakatoka babu akafanya yake kisha akaita akaingia sasa huyu Jamaa sasa akaambiwa mimi utaniletea hela utakapo fanikiwa ila weka elfu 1000 ya wazee akaweka akapewa fimbo akaambiwa ukitoka hapa usisemeshane na mtu yeyote halafu mlipo kuwa mnakuja na hiyo njia urudi nayo hiyo hiyo ila utakutana na ng'ombe atakuja kwa kukulenga wewe usimkwepe haya kwa kila la heri.

Jamaa akawa anaondoka kifua mbele anajisemesha mbona mitihani midogo hivi halafu ameteseka muda mrefu hivi. Wakati anatembea kama saa 1 na robo hivi ktk pori lile akasikia kama kuna kitu kinakuja kwa nyuma kwa kishindo kikubwa sana akageuka halafu hakuona kitu alipogeuka kuendelea na safari yake akaona nyoka ambayo hajawahi kuiona halafu imesimamisha kichwa ina mlenga jamaa.

Daaah!jamaa akasema haya masihara sasa unaweza kufa inajiona jamaa anasema chocho aliyoingia kulikuwa na miba lakini alipita halafu alipofika akaona sehemu alipo ndo yuko salama ndo akaanza kusikia maumivu ya ile miba na majeraha mengine. Akajitahidi hadi akafika kwao akalala kwanza akili iliyo mwijia hapo nikuwa konda wa daladala lakini maisha yanabadilika atimaye amegeuka tena Kwenye madini.

Yupo mpiga boya ktk duara hapa site.

Najua kuna vituko mbali mbali ambavyo wanaume tumepitia,kama unavyo embu tupe na wewe ili tuburudike na tupate exp..ya hawa waganga wanaotesa watu pasipo kujua wanawatesa.

Nawasilisha karibuni sana JF ni sehemu ninayoipenda sana kuna watu wakikusimulia mikasa yao umaweza ukafikilia movie vile kumbe nikweli.

Tukipata tena muda nitatupia kingine tena,ahsanteni
 
Daaa bora ww umesema kuwa ni rafiki zako, Tuna dada mmoja kazini kwetu kila stori ikianzishwa yeye ilishai kumtokea alipokuwa Tanga
 
Acha POROJO kijana , tafuta pesa hautakua na muda wa kuhadhithiana stori za kutunga
Uko sawa unasema unacho jisikia,haya maisha watu yamewatokea.huwa tunapo maliza kazi huwa napenda kufahamu vijana wenzangu malengo yao hasa ni nni?na pia napenda wanapo pata Pesa wafanye mambo hasa nawashaur sna pia napata mikasa waliyo pitia unajifunza pia.
 
Daaa bora ww umesema kuwa ni rafiki zako, Tuna dada mmoja kazini kwetu kila stori ikianzishwa yeye ilishai kumtokea alipokuwa Tanga
Wapo watu wanamna hiyo,au mmekaa sehemu na jamaa yako mnapiga story anajitokeza kiumbe unasikia aisee..umenikumbusha sehemu frani ilikuwa hivi na vile,kwanza hajui mmeanzia wapi?kisha mnamtazama kama katuni
 
Tafuta pesa uache kujielezea sana
Sawa ngoja tutafute pesa ndg
IMG_20200610_075943.jpg
IMG_20200605_152817.jpg
 
Back
Top Bottom