Japo Mtaani kuna mambo


, Kuna mwanamke anamsema mwanamke mwenzie kuwa Katia Aibu, kisa kajifungua mtoto Mchafu ana maukoko ya mwanaume mwili mzima




,
Ana amin kwamba Na kuna hizo iman, kuwa mwanamke aki sex akijifungua ndani ya siku chache mtoto atatoka na Maukoko yaan mashahawa ya mwanaume..
Sio kweli kabisaaaa.
Sex mnaruhusiwa kufanya ni salama kabisa kama mimba yako haina matatizo.
UTANDO HUU UNA KAZI GANI?
Kuelewa kazi ya utando huu, fikiria kwanza ngozi yako hasa ya vidole inavojikunja unavokua umeiweka kwenye maji kwa muda,
Mfano wakati unaoga au unafua lazima itakuwa na makunyanzi. Maji yanasababisha kitu kama hicho pia hata kwenye ngozi za watoto.
Na tukumbuke mtoto anakaa kwenye maji maji ya kwenye mji wa mimba kwa muda wa week 40 basi kipindi chote hiki utando huu unafanya kazi ya kuilinda ngozi ya mtoto isitengeneze makunyanzi na kuwa laini.
FAIDA NYINGINE ZA UTANDO HUU
Mbali na kuwa losheni inayolainisha ngozi ya mtoto utando huu unafanya kazi nyingine zifuatazo:
1. Kumkinga mtoto na maambukizi. utando huu unasaidia kumkinga mtoto na maambukizi ya bakteria,una viambata vinavyozuia radikari huru (ant oxidants) na ant bacteria
2. Inasaidia kuzuia michubuko ya ngozi wakati mtoto anazaliwa. (lubrication)
3. Inasaidia kubalance joto la mtoto.
Mtoto akizaliwa na hayo mafuta mafuta, kazi zake ndio hizo hapo juu.
Sent using
Jamii Forums mobile app