Kwa taarifa yko Kama ulikuwa hujui...
Kabla magari hayajawa deal, Askari wa Usalama Barabarani walikuwa wanakamata baiskel...
Na makosa yaliyokuwa yanakamatisha ni haya
1. Kama haina Kengele
2. Break
3. Bedal imebaki msongo(imebaki chuma tu kwenye kikanyagio).
4. Kibati (Ushuru wa Halmashauri)
5. Tairi kipara
6. Haina taa.
7. Ina taa ila haina Dynamo.
8. Dynamo haifanyi kazi
9. Ukiendesha umevua shati...(ugangwe au ubabe)
10. Ukiendesha hujavaa Makubasi
Faini yake ilikuwa kati ya Shilingi 5 mpaka Sh 20... Nyakati hizo Baskeli mahiri ilikuwa ni Phoenix ilikuwa inauzwa Sh.1500 na hizi Swala, Gazebo, shangsheng na nyingine zilikuwa 659-800 tu
Sasa siku ukimsikia mtu anakwambia familia yao ilikuwa maskini mpaka hawakumudu kununua hata baskeli basi hizo ndio zilikuwa bei za baskeli...
Halafu kuna wale Askari wa Usiku na Usiku wa Manane, wenyewe wlikuwa wanakamata zisizo na taa tu... Faini yao ilikuwa 50 -200....
Wahenga tu ndio wataelewa hii.
Sent using
Jamii Forums mobile app