Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Mwambie anipigie ni mimi mama yake!!mwambie sina simu ila nimeona picha zake kwenye simu ya kupalaza ya khamisi/mwambie amenenepa sana ..mwambie nimeona gari lake ni zuri sana !!ila mwambie mama yake bado naishi kwenye lile banda pamoja na kuku/mwambie nimeumwa sana ila nikapona bila hata kutumia dawa/mwambie mzee juma bado ananidai pesa zake nilizokopa ili nimlipie ada amechukua kile kishamba nilichokuwa nakitegemea kufidia deni lake/mwambie mimi mama yake nimebaki pekee yangu tangu baba yake afariki sina hata wa kunisogezea kuni motoni/mwambie leo nimetamani sana nyama[emoji24] zile mboga zilizoota zenyewe upenuni zimenichosha mpka mdomo umekuwa mchungu/mwambie wale vijana walitaka wanipige eti mimi mchawi eeh/mwambie mama yake nimekuwa mzee sana nahesabu siku tu aje hata nishike mikono yake nimuoneshe mipaka ya nyumba yetu/!!salio limeisha mwambie mama anampenda sana[emoji24]!ila huku kijijini nimebaki pekee yangu wenzangu wote wameenda mjini kusherekea kwa watoto wao...

[emoji117]Tuwapende mama zetu wale tulojaaliwa kuwa nao hadi leo waliotangulia mbele za haki tuwaombee kwa mola awaweke mahali pema peponi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
View attachment 2789696
Tuwapende mama zetu wale tulojaaliwa kuwa nao hadi leo waliotangulia mbele za haki tuwaombee kwa mola awaweke mahali pema peponi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maokoto
20231023_042102.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom