MAISHA YANGU YAPO HATARINI;WAKILI DKT NSHALA RUGEMELEZA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
"Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yetu Tanzania" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWa Habari
"Kuna maagizo kutoka ndani yanayosema,Mimi nikionekana niteketezwe,nimalizwe,niuawe,na jina langu liwe refu lianze na Marehemu Rugemeleza Albert Kamwagwa Nshala" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza
"Kama wenye dhamana watapenda Mimi niondoke,niitwe Marehemu basi yatawapata makubwa,vizazi vyao mia nne na arobaini vitakwenda kuteseka na kujibu juu ya jambo hili" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.
"Siko tayari kupigishwa magoti,kunyamazishwa au kukandamizwa na mtu yeyote ambaye kikatiba na Yeye ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mimi" Wakili Dkt. Nshala Rugemeleza.
"Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko,sitatishiwa na binadamu mwenzangu anayeumbwa kama Mimi,anayeenda chooni kama Mimi,anayeumwa kama Mimi,anayekufa kama Mimi"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.
"Nimetumia lugha nyepesi sana,na laini kwa walichotufanyia viongozi wetu,kama ingekuwa ni huru na kawaida basi viongozi wetu wangekuwa mbele ya sheria muda huu tunavyozungumza" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza.
"Mfumo wetu ni ule ambao hata Rais akikukanyaga unasema ooh ahsante kwa kunikuna" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza
"Sitasalimu amri,nitaendelea kupinga ugawaji huu wa rasilimali za nchi yetu,nitasimama na maneno yangu" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza
"Mkataba huu mbaya kuwahi kutokea Rais anahusika Moja kwa Moja kwa sababu sahii yake ipo mwisho wa jedwali la mkataba,Marais uwa hawasaini lakini yeye kasaini"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza#MkutanoWaWaandishiWaHabari
"Bunge la mwaka 2017 lilitunga sheria kuhusu mikataba ya rasilimali zote zipite bungeni,ila mkataba wa bandari unasema Dp World haiusiki na sheria hiyo" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza
"Mkataba huu unalimbikiza Mali zote za nchi hii kuhusiana na bandari kwa kampuni binafsi ya DP World,sheria inasema tulinde maliasili kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavyo,hiki ndicho kilichotufanya tunyanyuke tupinge" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza
"Kama nasema uwongo nashika biblia yangu Mimi ni mkristo,nianguke chini Mungu achukue uhai wangu" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.
"Nimesoma digrii yangu ya kwanza Udsm,digrii ya pili Havard,nikaenda kusoma digrii ya tatu Yale na PhD Havard baada ya kutoelewa lugha iliyozungumzwa kwenye mgogoro wa Bulyakhuru" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.
"Tuna haki ya kulinda maliasili za Taifa kama zipo hatarini,sio kama mkubwa hakosei,Bandari ni mali ya Watanzania wote, tuna haki kuhoji au hata ikiwezekana kwenda mahakamani kama Mali za nchi zinauzwa"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.
"Naipenda nchi yangu Tanzania,nipo tayari kuifia nchi yangu,na kama huu ni mwisho wangu basi nasema kwa herini tutaonana Paradiso" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.