Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,218
- 829,210
- Thread starter
- #169,621
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 45 nchini Kenya, John Rugala (45), amefariki kwa kujiua baada ya Mke wake kuripotiwa kukataa kumpikia kuku akiwa nyumbani kwake Uriri, Kaunti ya Migori nchini Kenya.
Msaidizi wa Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Nyaobe John Atonya amesema Mwanaume huyo alijifungia ndani ya nyumba yao kabla ya kujichoma moto, taarifa za awali zinaonesha kuwa Mkewe hakutaka kupika mboga hiyo kutokana na kuku huyo kuwa ni mali ya Binti yao.
Inadaiwa kabla ya kujiua John alimfukuza Mkewe nyumbani na baada ya tukio Wananchi walikimbilia eneo hilo kwa nia ya kuzima moto lakini juhudi zao zilifeli.
Mwili wa marehemu umehamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Migori Level Four kusubiri uchunguzi huku Polisi wakitoa wito kwa Wanandoa kutafuta njia mbadala za kutatua migogoro yao.
Sent using Jamii Forums mobile app