Kati ya watu wazima waliotoka Misri na kuingia nchi ya Ahadi ni Kalebu na Joshua tu wengine walifia njiani. Musa mwenyewe aliishia kuiona kwa mbali kwa kuonyeshwa na Mungu na kaambiwa hutaingia utafia kwenye mlima huu.
Watoto waliozaliwa jangwani na wale waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 ndio waliingia Kaanani ila watu wazima walifia jangwani.
Lengo kuu la wana wa Israel kuzungushwa miaka 40 lilikuwa wasije wakakumbuka njia na kuamua kurudi nyuma baada ya kukutana na mambo mazito na ya kutisha.
Pia wasije wakafika Kaanani na kuanza kuwafundisha mambo waliyoyajua kipindi wakiwa Misri hasa kuabudu miungu ya kigeni.
Ila hawa watu nao walikuwa vichwa ngumu kunung'unika, kulalamika, kulaumu na kukata tamaa ilikuwa ni kawaida yao,kumbuka mkutano wa Kora walivyomezwa na ardhi, Haruni na nyoka wa shaba, kuvuka bahari ya shamu, walivyokumbuka vitunguu saumu cha Misri.
Hawa hawa walimkosesha Musa aisiingie nchi ya Ahadi akapiga jiwe litoe maji kwa amri yake pasipo kumtukuza Mungu wake, naye Mungu akamkasirikia. (Musa alikuwa na hasira kibinadamu nazo zikamponza).