Injini ya meli kubwa iliharibika na hakuna mtu aliyeweza kuitengeneza, kwa hivyo waliajiri Mhandisi Mitambo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30.
Aliikagua injini kwa uangalifu sana, kutoka juu hadi chini. Baada ya kuona kila kitu, mhandisi alishusha begi lake na kuchomoa nyundo ndogo. Aligonga kitu kwa upole.
Mara injini ikawa hai tena. Injini imerekebishwa kwa dakika tuu!
Wiki moja baadaye mhandisi huyo alimweleza mwenye meli kwamba gharama ya ukarabati wa meli hiyo kubwa ilikuwa dola 20,000.
"Nini?!" Alihamaki mmiliki. "Hujafanya chochote. Tupe mchanganuo wa kina."
Jibu ni rahisi: Gonga kwa nyundo: $2 Jua wapi pa kugonga na ni kiasi gani cha kugonga: $19,998
Umuhimu wa kuthamini utaalamu na uzoefu wa mtu...maana hayo ni matokeo ya mapambano, majaribio na hata machozi. Ikiwa nitafanya kazi kwa dakika 30 ni kwa sababu nilitumia miaka 20 kujifunza jinsi ya kufanya hivyo kwa dakika 30. Una deni kwangu kwa miaka, sio dakika