Nikimaanisha dini zetu hizi za muogope Mungu Kwenye Kila jambo na bado binadamu ni washenzi...
Nimesema Wana mambo yao...
Unataka kusema Japan hakuna washenzi? Jamii ya Wajapan ni jamii changamano sana na mifumo yao ya kijamii, kiuchumi na hata kiimani imefungamana mno tangu enzi na enzi. Hata mfumo wao wa elimu ni tofauti sana. Watoto wanafundishwa honor na integrity na ni aibu kubwa kuleta sifa mbaya na kuharibu jina la familia na ukoo. Ndiyo maana wana kiwango kidogo sana cha ufisadi na uhalifu kwa ujumla na hasa mauaji.
Kutokana na kuwa katika "The ring of fire" tangu zama za kale wamekuwa wakihangaika na matetemeko makali ya ardhi ya kutisha, mavolkeno na masunami...huku nchi yenyewe ikiwa ni mkusanyiko wa tuvisiwa tu twingi tudogo tudogo. Kiraslimali wala siyo matajiri. Ndiyo maana wakaanza kuwekeza sana kwenye sayansi na teknolojia tangu enzi na enzi...na leo kitekinolojia ni kama wanaitawala dunia. Scarcity is the mother of invention (siyo kama sisi mtu unatoka tu nje hapo na mshale wako unaua pundamilia mnakula nyama na familia yako kwa mwezi mzima. Ugundue bunduki ili ikusaidie nini?).
Katika dini yao wanafundishwa kuwa mtu mwema na aliyeishi maisha yake kwa amani hapa duniani hafi maana matendo yake yataendelea kuishi hata kama yeye kaondoka. Na kulinda na kulitetea taifa lao ikibidi hata kufa ni heshima ya ajabu. Kuna gharama kubwa ya kuwa Mjapan na tumia kila mbinu na fanya lo lote ili usiwe chini ya mtu mwingine kifikra na kitamaduni. Ndiyo maana Wamarekani walipata shida sana kuwashinda katika vita vya pili vya dunia...Kamikaze.....mpaka ikabidi kuwapiga nyuklia tu ili kumaliza mchezo.
Shida yetu sisi tumeletewa kila kitu - dini, elimu, mfumo wa maisha, "ustaarabu", demokrasia, teknolojia....ndiyo maana kuna mpishano kati ya matendo; na yale tuliyoletewa...Naamini tungeachwa tukajikongoja kivyetu tukapitia zile hatua za maendeleo ya kibinadamu (ujima, ukabaila, ubepari...ujamaa...ukomunisti) tusingekuwa hivi tulivyo leo...bila dini, ustaarabu, teknolojia, demokrasia yetu; na mengineyo...